Bongotunacheza
JF-Expert Member
- Dec 7, 2018
- 983
- 2,306
Sio kweliMambo unayosema yote ni zaidi ya hiyo ada unayoikandia..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kweliMambo unayosema yote ni zaidi ya hiyo ada unayoikandia..
Mkuu acha saundi na fiksi. LIKUD Alianza utopolo huu wakulazimisha watu wasipeleke watoto wao English medium mwaka huu.Nilifuata ushauri wa Likud Nina watoa watoto wangu shule ya English Mediums.
Niliwatoa mwaka jana katikati. So mwaka huu mzima watoto wangu wamesoma Kayumba.
1. Kwa mwaka huu mzima pamoja na kumalizia kibanda changu na kununua kiwanja kingine,nimeweza kuhifadhi shilingi milioni 8 na uchafu.
2. Hili limewezekana kwa sababu nimewatoa watoto wangu shule ya English Medium.
Nilikuwa nasomesha watoto wa3. Mtoto mmoja kwa mwaka ada tu ni milioni mbili, bado hajaweka usafiri na vikorokocho vingine tuseme ukihesabu na hivyo inakuwa milioni 3 na ushee.
So kwa watoto watatu maana yake ningekuwa nimetoa milioni kumi halafu pia nisingekuwa na akiba yani sasa hivi ningekuwa naumiza kichwa ntapata wapi hela za kuwalia wanangu.
But :
1. Nimehamia kwangu. Watoto wangu wanaishi nyumbani kwababa yao. Nisinge wahamisha hadi muda huu ningekuwa sijajenga wala nisinge kuwa na kiwanja cha ziada wala hiyo milioni nane.
2. Nina kimilioni nane changu ambacho kufikia mwakani mwezi wa kumi na.mbili kwa mipango niliyo iweka itakuwa imezalisha mara kumi yake.
3. Watoto wangu wanasoma shule kifalme. Wanaenda kwa miguu umbali wa kama dakika kumi. Wanakula vizuri, wanalala pazuri, wanavaa vizuri, shuleni wana sare pea tano tano viatu pea tano tano mabegi pea 3 tatu kila mmoja.
Nawasimamia vizuri.
Wanafanya vizuri darasani.
Nimewawekea programme za kitaaluma : home tuition; English, Hesabu na Sayansi plus programme za kitaaluma kupitia kwenye Tv ya nchi 40+ ambayo pengine nisinge weza kuinunua kama wangesoma shule ya Em coz hela yote ingeishia kwenye ada.
Asante sana Likud.
Watanzania wenzangu wenye kipato cha kawaida fikirieni mara mbili. Wacheni kujistress na ada kwenye shule za EM wakati uwezo wenu ni wa kuunga unga.
Kusomea EM at least uwe na networth ya kuanzia walau milioni 150 plus.
Katoa ushauri kwa wenye vipato vya kuungaunga wenye uwezo waendelee kusomesha huko, hajawakatazaHizo English medium kuna watanzania wenzako wameajiriwa huko na wanaendesha maisha yao na kuhudumia familia zao.
Kampeni na ushuhuda huu si afya Kwa taifa.
Wahenga walisema usiige kunya kwa tembo utapasuka msamba!Hujagusia maendeleo yao kitaaluma na ubora wa elimu, unakagua madaftar ya watoto wanachosoma shuleni
Ameanza 2023 mkuu, sema 2024 ndio emeweka nyuzi nyingi zaidi.Mkuu acha saundi na fiksi. LIKUD Alianza utopolo huu wakulazimisha watu wasipeleke watoto wao English medium mwaka huu.
Mwaka jana hadi mwanzoni wa mwaka huu nyuzi zake zilikuwa za lindi na mtwara.
Usituchukulie poa watu humu jamvin tuko makini kufuatilia mambo.
Uumbwaaa Chaliifrancisco
Nyau de adriz
Hujagusia maendeleo yao kitaaluma na ubora wa elimu, unakagua madaftar ya watoto wanachosoma shuleni
Soma vizuri Uzi wangu sijaacha kituHujagusia maendeleo yao kitaaluma na ubora wa elimu, unakagua madaftar ya watoto wanachosoma shuleni
Sahihi kabisa mkuuEnglish Medium schools ni money making scheme kwa wamiliki wa hayo mashule..standard ya elimu ni ileile....unapambana huku chini ili mje kujazana at university level...mkishapata degree zenu mnarudi mtaani kuzungusha bahasha. Kama mzazi unajijua huna biashara, makampuni au assets unazotaka mwanao/wanao waje wazisimamie au waziendeleze basi usijisumbue kumpeleka mwanao huko English Medium. Ni upotezaji wa fedha....hizo 4/5M unazolipa kama ada ya mtoto ili asome EM schools ni bora ukamfungulia fixed deposit account mwanao ili akimaliza masomo apate mtaji wa kuanzia maisha yake mtaani.
KabisaHizi shule za kina Junior ukicheza nazo zinakufirisi kimya kimya.
Unakuwa unazitafutia ada tu. Mambo mengine ya muhimu yanasimama
Duh kama vile umeumia mwenzako kutunza milioni 8 kwa mwaka mzimaporojo
una tatizo la ufahamu mkuu mie niumizwe na porojo za mtandaoniDuh kama vile umeumia mwenzako kutunza milioni 8 kwa mwaka mzima