Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Stanley Mitchell had bmw 7 series 735 ya 2011 ni bei rahisi?? unadhan unaweza ipata na bajet yako?? bmw ni kampuni jamani sio aina na gari ukiandika bmw andika ja model yake maana kwa sentensi yako hapo ni sawa na kuwa umeandika umeaandaa milion 13 lakini unasema toyota za 2011 ni bei rahisi wakati hela yako haifiki hata asilimia 10% ya kununua v8 used ya 2010....
 
Mkuu ungekua unafatilia huu uzi kwa makini toka mwanzoni hapa tukiongelea "BMW" tunamaanisha "bmw 3 series e90" ndo mana nikasema just "bmw ya 2011" nikimaanisha 3er ya 2011...

Pia hakuna mahali nimesema toyota ni bei rahisi huezi kuamini sijui bei ya gari yoyote ya toyota labda ist kwasababu sijawai kua interested na toyota yoyote hata iwe prado au v8 uliyoitaja...nafata moyo wangu mm hata uweke iyo V8 kwa bei chee siwezi kuacha German hata iwe kwa bei ghali.... inshort huezi kunikuta naongelea toyota mimi ndo mana nashangaa umesema nimesema mambo toyota wakati ilo neno nina miezi sijawai kulitamka....

Pia iyo milioni 13 sio bajeti yangu ya kununua gari iyo A4...
nimesema hivii iyo 13m ni kodi ya A4 ya 2008, ya 2007 ndo 10m na 2009 kodi yake ni 15.9m, 2010 ni 17m na 2011 kodi ni 13.4m
kwaiyo ujue kua bajeti ni Kodi plus CIF.....

Halafu nilivosema naona ni "bei ndogo" nilimaanisha kwa bajeti yangu na ukilinganisha na mwaka wa gari naona bei ni ndogo
mfano hapo huezi kukuta audi a4 ya 2010 au 2011 ukaipata kwa dola 4,000 ila 3 series ya miaka iyo unaipata kwa dola 4,000 or less
 
Hata kama una OBD scanner kama mtu hajui jinsi ya kutatua tatizo haita saidia.

Kwa mfano ECM (computer ya gari) itasema tuu kunatatizo kwenye MAF circuit (mass air flow sensor) na kuonesha error code P0101 na kuwasha taa ya check engine light wakati tatizo linaweza kuwa ni vumbi linalofanya sensor isisome vizuri.

Ukisafisha hiyo sensor na alcohol na ku-clear code utakuwa umeondoa tatizo. Sasa utaona limitations za hizo scanner...zenyewe zinakupa tuu eneo ambalo tatizo linaweza kuwa.
 
Kulinunua sio tatizo,tatizo ni kulifanya liendelee kukaa barabarani, upatikanaji wa spea ni mgumu kwa bongo pia ni ghali,unaweza kuwa na pesa lakini ukakosa spea bongo mpaka uagize toka nje!!
Hivi ni kitu gan kinamfanya mtu anunue gari?
1. Upatikanaji wa spea?
2. Uhitaji wa gari?

Maana sielewi, kila gari ikitajwa watu mbioo uoga wa upatikanaji na ughali wa spea. Mara ulaji wamafuta.

We need to change our mindsets atheeee
 
True fact mkuu, na ndio maana gari zao zipo allover the world. Pia adaptation imekuwa rahisi kwa gari zao maana gharama za uendeshaji zipo reasonable kwa raia wengi.

European brands zipo na superficial technology pamoja na performance ila zinasumbuaga sana na mazingira ya kwetu huku na usiombe likianza kukusumbua utatoa hela mpaka useme nini hiki?!
Gari ina umeme tu kila mahali yani, kakitu kadogo kanaweza kakakufanya ulipark gari kwa miezi na mara zote inataka uwe na mfuko wa uhakika ili kuweza ku maintain.

Taa za check engine hazitakuacha salama ndio maana waliyoyatumia wanaona heri toyota tu service ya gharama kubwa haizidi laki 6 kwa toyota ila kwa hao jamaa ni si chini ya 2.5 million *****.
 
Kama nissan umeimudu sina shaka Beamer utaiweza vyema.
 
Wengi wanatafta sifa tu, mwisho wa siku wanalialia na magu alivyobana *****.
 
Sio Tanzania tu hata huko yanapotoka hayo magari resale value yake ipo chini sana tofauti na Toyota. Wazungu wenyewe wanakiri yani sio utani. Utanunua gari mpya dola laki moja na hamsini ($150,000) baada ya mwaka mmoja mpaka miwili ya matumizi tu hamna mtu atalinunua hilo gari zaidi ya dolla elfu hamsini ($50,000) na wateja wenyewe wa kutafta na tochi.

Ila njoo kwa Toyota sasa, gari ilionunuliwa dola elfu arobaini ($40,000) ndani ya miaka miwili huwezi kukuta inauzwa chini ya dola elfu ($30,000) na wateja wapo kibao.
 
Umemaliza mkuu.
 
Tatizo ni TRA kwenye ushuru wa magari ya ulaya bei zake zipo juu hatari 2009 VW Jetta $3500 CIF ushuru 18.5milion mpaka unashangaa hawajaa vipi
 
Aaaaah wajerumani wazee wa kufanya complications. Wajanja hawa jamaa.... mi nawakubali kwenye luxury features zao tu. Lakini Engine tumuachie Mjapan.
 
Ila BMW sizipendi coz kuna cku nilipanda ya mdada mmoja akawa ananiringishia[emoji23][emoji23]kuanzia hapo nikaichukia..saivi ipo juu ya mawe kaipaki[emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…