Nadhani CCM hawakai kama Kamati katika kupendekeza, kuchambua na kupitisha nani awe nani ndani ya chama. Yawezekana maamuzi mengi hutegemea mahaba na mapendekezo ya mtu au kikundi cha watu wachache. Sina hakika na hili ndiyo maana nimetumia maneno nadhani na yawezekana.
Ukiangalia kwa nje, wanaccm wengi walifurahia sana uteuzi wa Makonda kuwa mwenezi na wamepigwa na butwaa baada ya kutenguliwa. Sasa unajiuliza ikiwa demokrasia ilifanya kazi ya kumteua iweje isitumike kumtengua, mpk inaacha malalamiko?
Hii ni ishara kuwa kuna kikundi cha watu wachache ama mtu mmoja (mwenyekiti) ndiye huamua nani awe ni nani ndani ya chama.
Pili, Jokate Mwegelo aliyeteuliwa Oktoba mosi 2023 kuwa Katibu wa UWT taifa, leo ametenguliwa na kuteuliwa kuwa katibu mkuu UVCCM. Je, Jokate amepwaya ktk nafasi hii kwa muda mchache kiasi hiki? Hamkumchunguza kabla ya kumteua?
Pamoja na uteuzi na utenguzi wa leo, bado nafasi ya katibu mkuu UWT taifa haijajazwa. Hivyo muda si mrefu utasikia mtu anateunguliwa halafu anateuliwa kujaza nafasi ya UWT taifa.
CCM bado kunafukuta, tutaendelea kushuhudia teuzi na tenguzi ndani chama hiki kikongwe.