Bado CCM hakujatulia. Naziona teuzi na tenguzi nyingine muda si mrefu

Bado CCM hakujatulia. Naziona teuzi na tenguzi nyingine muda si mrefu

Wananchi, wanachama na serikalini kwa asilimia kubwa hufuata mkumbo kama nyumbu. Hii ni changamoto kubwa na msingi wa umasikini.
Kushangilia, kusifu na kuabudu bila kuzingatia mantiki ni kawaida.
Wachache sana waliowahi kuonesha msimamo na wanastahili sifa (Nchimbi, Kimbisa, Sofia Simba na wenzao).
Hata hivyo, tunahitaji chama imara, chenye wanachama wanosimamia itikadi na sera bila kuyumba kwa ajili ya kumkomboa mtanzania, mwafrika ambaye uhuru umeendelea kuwa wa bendera zaidi na siyo kiuchumi.
Tatizo lipo hata kwa wanaoteuliwa na kutenguliwa. Kwanini wanakubali kila teuzi? Namsifu sana Diwani Athumani, yeye alipotenguliwa uDCI akagoma kuteuliwa kuwa mnikulu (mpanga mapazia na meza pale ikulu).
 
Njaa inawasumbua pia , Makonda kavuka ka mstari ka kujipendekeza naona kateuliwa kuwa RC lakini hajatoa shobo kama wenzake kama hayupo vile
 
Hawa watoto wa mjini walizidiwa 2015 hata 2025 watazidiwa maana nchi itakuwa hoi

Wao wanajua kuiba tu halafu wanachukiwa na watanzania wengi
Walitaka kucheza fair ndiyo maana wakampa member wa washamba kijiti. Safari hii ni wao na tume mtu mpk mtu wao arudi mjengoni. Hata akipata kura moja, atarudi tu.
 
Njaa inawasumbua pia , Makonda kavuka ka mstari ka kujipendekeza naona kateuliwa kuwa RC lakini hajatoa shobo kama wenzake kama hayupo vile
Hana jeuri ya kukata. Akirogwa kesi zake zote zitamhusu. Huyo Diwani hata sokoni haruhusiwi kwenda baada ya kukata uteuzi mpya.
 
Hana jeuri ya kukata. Akirogwa kesi zake zote zitamhusu. Huyo Diwani hata sokoni haruhusiwi kwenda baada ya kukata uteuzi mpya.
Ha ha muda utaamua lakini siwaoni hao born town kwenye siasa kwa miaka 2 mbele , watafutwa wote

Tujipe muda , nchi isharudi ilikotoka ambako tulikuwa tumesahau pia Watu wanaenda kuogopa kuvaa mashati ya CCM

Pia hao born town hawakubali kuliko washamba ukitaka kuamini ingia mtaani
 
Ha ha muda utaamua lakini siwaoni hao born town kwenye siasa kwa miaka 2 mbele , watafutwa wote
Kuhusu suala la kufuta watu, watoto wa mjini ndiyo wanaoongoza . Remote inaangalia nani kimbelembele toka Kanda hiyo, Kisha inampumzisha kwa amani. Mpk 2030 unakuta washamba wenye nguvu wote hakuna.
 
S
Ni katika kuwatumikia wananchi, kujiimarisha na kujizatiiti mamlakani, CCM bila mbambamba yoyote haitasita kuteu lakini pia kutengua yeyote kadiri inavyoonekana inafaa....

Ina hazina ya kutosha ya waandamizi waadilif
na hodari wa kazi..
Soon unaungana na Lucas
 
Ni katika kuwatumikia wananchi, kujiimarisha na kujizatiiti mamlakani, CCM bila mbambamba yoyote haitasita kuteu lakini pia kutengua yeyote kadiri inavyoonekana inafaa....

Ina hazina ya kutosha ya waandamizi waadilifu na hodari wa kazi...
Mwenykiti wenu ni zero brain. Yeye mwenyewe anajua hilo.
 
S

Soon unaungana na Lucas
sina haja ya kuungana au kuunganishwa mtazamo wa yeyote katika masuala yoyote yale 🐒

ni bayana,
ninajisimamia mwenyewe bila shuruti wala shinikizo kutoka upande wowote ule. Na ikiwa maoni na mtazamo wangu ni kikwazo yeyote, bas aweza pita kando kwa amani kutafuta faraja panapomfaa...🐒
 
Teuzi kila baada ya miezi mitano au sita, ni mda gani sasa huyo kiongozi atakuwa amefanya mambo ya maana 🤔🤔??. Saa100 na genge lake ni tatizo sana ☹️☹️.
Punda anakaribia kukata roho anarusharusha miguu
 
Nadhani CCM hawakai kama Kamati katika kupendekeza, kuchambua na kupitisha nani awe nani ndani ya chama. Yawezekana maamuzi mengi hutegemea mahaba na mapendekezo ya mtu au kikundi cha watu wachache. Sina hakika na hili ndiyo maana nimetumia maneno nadhani na yawezekana.

Ukiangalia kwa nje, wanaccm wengi walifurahia sana uteuzi wa Makonda kuwa mwenezi na wamepigwa na butwaa baada ya kutenguliwa. Sasa unajiuliza ikiwa demokrasia ilifanya kazi ya kumteua iweje isitumike kumtengua, mpk inaacha malalamiko?

Hii ni ishara kuwa kuna kikundi cha watu wachache ama mtu mmoja (mwenyekiti) ndiye huamua nani awe ni nani ndani ya chama.

Pili, Jokate Mwegelo aliyeteuliwa Oktoba mosi 2023 kuwa Katibu wa UWT taifa, leo ametenguliwa na kuteuliwa kuwa katibu mkuu UVCCM. Je, Jokate amepwaya ktk nafasi hii kwa muda mchache kiasi hiki? Hamkumchunguza kabla ya kumteua?

Pamoja na uteuzi na utenguzi wa leo, bado nafasi ya katibu mkuu UWT taifa haijajazwa. Hivyo muda si mrefu utasikia mtu anateunguliwa halafu anateuliwa kujaza nafasi ya UWT taifa.

CCM bado kunafukuta, tutaendelea kushuhudia teuzi na tenguzi ndani chama hiki kikongwe.
Hiyo UWT si wangempa Makonda sasa,
 
Kuteua na kutengua ni njia ya kujiimarisha.
Baadhi ya watu ukiwapa cheo furani wanahaha nchi nzima kusumbua watumishi ambao wapo chini ya mamlaka nyingine.
Mtu kama huyo lazima umuondoe, kama unadhani bado ana sifa utampeleka eneo lingine.
We ukiangalia hapo kuna kijiimarisha gani zaidi ya kupelekeshwa na mtu fulani,msoga ni mtu mbaya sana
 
We ukiangalia hapo kuna kijiimarisha gani zaidi ya kupelekeshwa na mtu fulani,msoga ni mtu mbaya sana
Msoga hana maamuzi, inchi ina viongozi.
Rais tunaye, Makamo tunaye , Waziri Mkuu tunayè na Katiba pia tunayo.
Kama kuna mapungufu tuwalaumu wao maana wameapa kuilinda Katiba na si kumlinda msoga
 
Tatizo la CCM Ni kwamba Ile kamati kuu ya halmashauri kuu Ina watu wengi Sana.
Wangekua Kama watano au hata sita wanaoaminiana Kama ndugu, Siri zao zisinge julikana kirahisi.
Sasa mle mle ndani Kuna ambao hawapendani, Kuna wanaogombea cheo Cha mwenzao, Kuna wasio waaminifu hata kwa wake waume zao. Unategemea watakichukulia chama Kama Nyerere na Kawawa walivyokichukulia?
 
Ni katika kuwatumikia wananchi, kujiimarisha na kujizatiiti mamlakani, CCM bila mbambamba yoyote haitasita kuteu lakini pia kutengua yeyote kadiri inavyoonekana inafaa....

Ina hazina ya kutosha ya waandamizi waadilifu na hodari wa kazi...
Ni matumizi mabaya ya fedha za Umma.
 
Wanaccm wenzangu, hivi naweza kuwa na kadi ya uwt na uvccm kwa pamoja??? Na uvccm haina umri? sisi vijana wa 40s tujimix
 
Back
Top Bottom