Bado inatafakarisha: Ilikuwaje Nyerere arithi taifa kwa njia ya kidemokrasia na yeye akaleta udikteta?

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
2,375
Reaction score
4,784
Wale pro-Nyerere wote nawaita humu. Kichwa kinajieleza chenyewe. Ni kweli Nyerere alirithi Tanganyika kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi halafu baada ya yeye kuingia kwenye madaraka, akaamua kwa utashi wake yeye binafsi, kuleta udikteta kupitia chama chake cha TANU na baadae CCM.

Na huu udikteta wa CCM kwa namna moja hauwezi kuutenganisha na matukio yote ya ajabu ya kisiasa yaliyotokea ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa miaka yote sitini iliyopita.

Binafsi yangu moyoni na kwa dhati kabisa, bado naitafuta sababu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere pasipo kuona hata sababu moja ya kwanini nifanye hivo. Yaani naona kama mambo yote haya ya hovyo yalianzia kwa mwalimu.

Nikosooni kwa hoja, kwanini sio hivyo ninavyofikiria.

MC
 
Hata Magufu.. alichaguliwa kidemokrasia lakini akaleta udikteta
 
Tuonyeshe kwanza uditekta wa Nyerere, yapi aliyofanya mpaka umpe hicho cheo cha uditekta
 
Gentleman,
I think this is among very nonsense narratives ever in platform.

I'm sorry for saying that light truth 🐒
 
Toa sababu. Usijifiche kwenye kichaka cha kusema eti ni 'nonsense narrative!' Kwani ni uongo uhuru haukupatikana kwa demokrasia kupitia uchaguzi ambapo Nyerere alishinda? Kosoa kwa hoja
 
Tuonyeshe kwanza uditekta wa Nyerere, yapi aliyofanya mpaka umpe hicho cheo cha uditekta
Alishinda uchaguzi kidemokrasia, kwanini alisitisha mfumo wa demokrasia uliomuweka madarakani? Huo ndo udikteta wenyewe. Kubali ukatae
 
Kwanini unahangaika na watu waliokufa.
Lazima tuangazie historia ili tujue tunasongaje mbele. Ingekuwa hatutakiwi kuhangaika na watunwaliokufa basi yafaa nini kujifunza somo la historia? Na kama ni hivo mbona mpaka leo Afrika inaimba kuhusu ukoloni ambao ni jambo la kihistoria? Ni kwasababu madhara yanaonekana mpaka leo, kwahiyo haikwepeki lazima tuwazungumzie na kama walikosea tuwape ukweli wao.
 
Kuunda katiba inayompa Raisi mamlaka makubwa bila kushtakiwa.

Huu ni UDIKITETA kabisa.
Shida ni kwamba watu wanataka tumuone Nyerere kama alikuwa ni Mungu kwenye sura ya binadamu, hii sio sawa. Udikteta ulinzia kwa Nyerere. Kwahiyo tunapoongolea Tanzania iliyoharibika hatuwezi kukwepa kumtaja Nyerere
 
Toa sababu. Usijifiche kwenye kichaka cha kusema eti ni 'nonsense narrative!' Kwani ni uongo uhuru haukupatikana kwa demokrasia kupitia uchaguzi ambapo Nyerere alishinda? Kosoa kwa hoja
kwahiyo unanilisha maneno au?

hayo ndio maoni na mtazamo wangu huru dhidi ya hiyo porojo, full stop.

muda wa kujadili dhana potofu sinao:1Head:
 
Wale pro-Nyerere wote nawaita humu. Kichwa kinajieleza chenyewe. Ni kweli Nyerere alirithi Tanganyika kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi halafu baada ya yeye kuingia kwenye madaraka, akaamua kwa utashi wake yeye binafsi, kuleta udikteta kupitia chama chake cha TANU na baadae CCM.

Na huu udikteta wa CCM kwa namna moja hauwezi kuutenganisha na matukio yote ya ajabu ya kisiasa yaliyotokea ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa miaka yote sitini iliyopita.

Binafsi yangu moyoni na kwa dhati kabisa, bado naitafuta sababu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere pasipo kuona hata sababu moja ya kwanini nifanye hivo. Yaani naona kama mambo yote haya ya hovyo yalianzia kwa mwalimu.

Nikosooni kwa hoja, kwanini sio hivyo ninavyofikiria.

MC
Zama zile sio hizi,mapinduzi yalikua njenje..yeye mwenyewe alinusurika!serikali nyingi Africa zilipitia hekaheka ya mapinzuzi zama zile,so alikua sahihi kuongoza vile
 
kwahiyo unanilisha maneno au?

hayo ndio maoni na mtazamo wangu huru dhidi ya hiyo porojo, full stop.

muda wa kujadili dhana potofu sinao:1Head:
Huna hoja wewe. Toa hoja yako tuijue. Kwani ni uongo Nyerere hakuingia madarakani kwa demokrasia? Kwani ni uongo kwa utashi wake alinzisha mfumo wa kidiktata wa chama kimoja?
 
Zama zile sio hizi,mapinduzi yalikua njenje..yeye mwenyewe alinusurika!serikali nyingi Africa zilipitia hekaheka ya mapinzuzi zama zile,so alikua sahihi kuongoza vile
hiko ni kichaka cha kujifichia tu.
 
Lazima tuangazie historia ili tujue tunasongaje mbele. Ingekuwa hatutakiwi kuhangaika na watunwaliokufa basi yafaa nini kujifunza somo la historia? Na kama ni hivo mbona mpaka leo Afrika inaimba kuhusu ukoloni ambao ni jambo la kihistoria? Ni kwasababu madhara yanaonekana mpaka leo, kwahiyo haikwepeki lazima tuwazungumzie na kama walikosea tuwape ukweli wao.
KUna dhana kwa history cant predict the future but the present situation can predict the future...hii utumiwa na wenye akili kubwa duniani..Chao
 
Hiyo ni dhana tu mkuu, wala haina uhalisia. Ni school of thought tu! Wengine wanaamini history can predict the present and the future; pia wapo sahihi na wanaweza kuthibitisha hilo.
 
Wanaoamini history can predict the future ndo watu wajinga na wapumbavu duniani...Kuna Tacticals na Strategics
 
Kinachomtofautisha Nyerere na wengine

1. Hakukuwa na social media hivyo kucontrol narratives ilikuwa rahisi. Ukishaiminya RTD, umemaliza mchezo kwa hiyo hata evidence kwa yaliyotokea. Mengi yanabaki kwenye masimulizi maana hayakuwa documented..

2. Alikosea kwa nia nzuri, yani anafamya makosa sio kwa sababu anataka kunufaika yeye au familia yake. Ila anakosea kwa kuipeleka nchi kubaya akidhani anaipeleka katika njia sahihi

Mengine ukikaa na wazee wa zamani wakakusimulia. Hayana utofauti sana na yanayotokea
 
Back
Top Bottom