Wale pro-Nyerere wote nawaita humu. Kichwa kinajieleza chenyewe. Ni kweli Nyerere alirithi Tanganyika kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi halafu baada ya yeye kuingia kwenye madaraka, akaamua kwa utashi wake yeye binafsi, kuleta udikteta kupitia chama chake cha TANU na baadae CCM.
Na huu udikteta wa CCM kwa namna moja hauwezi kuutenganisha na matukio yote ya ajabu ya kisiasa yaliyotokea ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa miaka yote sitini iliyopita.
Binafsi yangu moyoni na kwa dhati kabisa, bado naitafuta sababu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere pasipo kuona hata sababu moja ya kwanini nifanye hivo. Yaani naona kama mambo yote haya ya hovyo yalianzia kwa mwalimu.
Nikosooni kwa hoja, kwanini sio hivyo ninavyofikiria.
MC