Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Brother hili swala hutakiwi kugeneralize, siyo kila mtu hana uwezo wa kulea watoto zaidi ya watatu hadi Saba. Kinachotakiwa ni mtu kufanya tathmini ya hali yake kiuchumi kabla hajachukua maamuzi ya kuongeza idadi ya watoto na pia kuzingatia ushauri wa Afya kuhusu child spacing.

Kuzaa watoto ni baraka Kama una wezo wa kuwalea na kuwapatia mahitaji yao jinsi inavyotakiwa. Kwa hiyo hakuna limit kwamba mtu anatakiwa aishie kuzaa watoto watatu ndo aonekane kuwa anafuata uzazi wa mpango.
 
Kwahiyo waache kubanduwana?
 
Wala sio kosa, kwani hapo maadili gani kavunja, kuzaa ni kukosa maadili, nani kakwambia na mara nyingi ukiona hivyo ujue huyo mama alizaa mapema sana ndio maana mwili wake umemruhusu kubeba kiumbe kengine. Sio kosa sio dhambi sio kukosa maadili
 
sasa ujinga gani, hujui familia kubwa ni faraja.
familia ikiwa ndogo sana misiba ikitokea huwa inachoma sana kwa maana mpo wachache, mkiwa wengi kuna amani na faraja fulani hivi

hivyo tatizo sio big family ni uwezo tu wa kulea, kama mtu ana uwezo azae tu, kama kina kardashian, ni wazungu ila familia ni kuubwa hadi inafurahisha ile ni faraja kubwa sana.
 
I hate that behavior. Sio tu baada ya kuolewa; mwanao wa kwanza akishapevuka ni kukosa maadili mama kuendelea kubeba mimba.
maoni yako hayakubaliani na watu wengi, hakuna tatizo lolote, wala su ukosefu wa maadili, kwani hiyo mimba kapachikwa tu ama imepatikana kwenye mahusiano rasmi yanayotambulika!!

lini kuzaa kumekuwa jambo la nje ya maadili!!!!?
 
true point
 

Usiseme maisha ya sasa, sema kwa maisha ya mjini... kule kwetu kijijini bado wanafytatua kama kawa tena kwa amani kabisa.
 
Usiseme maisha ya sasa, sema kwa maisha ya mjini... kule kwetu kijijini bado wanafytatua kama kawa tena kwa amani kabisa.
Mkuu, ni sahihi mtoto wa mwisho akalingana na mjukuu wa kwanza?
 
Nafikir hakuna tatizo kwani kuzaa ni natural process.SO hakuna tatizo
 
Jichunguze utagundua kuwa wewe ndio huna akili.
Umekariri life ya kizungu bila kuchuja hata moja.
Km uchumi wangu upo stable acha nipate hata watoto 50.
Kupanga uzazi kwangu ni big NO!
 
Very true, shemeji yangu (mtoto wa baba mkwe) amezidiana na mwanangu mwaka mmoja. Mmoja ana miaka 4, mwingine 3
Inasikitisha sana. Sasa huyo mzee anazo nguvu za kulea huyo mtoto au atalelewa na mume wako?
 
Hakuna tatizo hapo.

Ikitokea Mzee akaoa mke mdogo/akaongeza mke wakati mwanae mkubwa ndio ameoa hilo haliepukiki na hakuna tatizo kabisa.
Anao uwezo wa kuwahudumia hao watoto rika la wajukuu zake?
 
Jichunguze utagundua kuwa wewe ndio huna akili.
Umekariri life ya kizungu bila kuchuja hata moja.
Km uchumi wangu upo stable acha nipate hata watoto 50.
Kupanga uzazi kwangu ni big NO!
Mkuu, ninakuunga mkono katika hili. Suala la uzazi wa mpango ni lazima liendane na hali ya uchumi wa wazazi husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…