Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Hakuna tatizo hapo.

Ikitokea Mzee akaoa mke mdogo/akaongeza mke wakati mwanae mkubwa ndio ameoa hilo haliepukiki na hakuna tatizo kabisa.
Mkuu, mimi sizungumzii suala la mke mdogo kwa maana mke mdogo hana mjukuu mpaka watoto wake watakapozaa.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
I hate that behavior. Sio tu baada ya kuolewa; mwanao wa kwanza akishapevuka ni kukosa maadili mama kuendelea kubeba mimba.
Naam [emoji419][emoji419]
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu Watanzania;

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili.

View attachment 1667340

Siku ya sherehe ya mwaka mpya nilikuwatana na dada mmoja anaitwa Veronica (hili sio jina lake halisi) ambaye nilimaliza naye shule ya msingi mwaka 1999.

Huyu dada nilikwisha kutana naye mwezi kama wa August maeneo ya Banana Ukonga huku Dar. Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana miaka takribani 15 tulipiga story nyingi sana za zamani.

Sasa nilipokutana naye tena Ijumaa ya tarehe 01 January 2020 huku Kivule ninapokaa (kwa maana aliniambia anakaa Kata moja na mimi) nilimuona anaongozana na binti mdogo wa miaka kama 9 hivi.

Tena huyo binti wamefanana kweli kweli. Basi tulipoonana tulisalimiana tena kwa furaha sana. Baada ya story kadhaa nikamuuliza, huyu ndio mtoto wako wa kwanza? Akakataa. Akasema hapana, huyu sio mtoto wangu.

View attachment 1667350

Huyu ni mdogo wangu wa mwisho. Mtoto wangu ameenda kwa baba yake kusalimia atarudi shule zikifunguliwa. Sema ndio rafiki yake mkubwa sana huyu (mdogo wake wa mwisho) kwa maana wamepishana mwaka mmoja tu.

Mimi sikuwa na jambo lingine la kumwambia zaidi tu ya kumpa hongera lakini nikawa ninajisemea tu kimoyomoyo "ina maana haya masuala ya mtoto na mama kuzaa kwa pamoja bado yanaendelea katika karne hii ya 21?"

Hii issue nilikuwa ninaiona tu kwa wazee wa zamani ambapo unakuta mtu unakutambulisha "huyu ndio baba yangu mdogo/shangazi yangu tumbo moja na baba" au "huyu ndio mama yangu mdogo tumbo moja na mama" lakini ukijaribu kuwatazama actually wanalingana umri au wamepishana mwaka mmoja tu.

View attachment 1667352

Mimi ni moja kati ya watu wanaokerwa sana na lugha za hawa dada/mama zetu manesi lakini linapokuja suala la kukemea wamama/wababa wanaoendeleza utamaduni huu wa hovyo mimi ninawaunga mkono sana.

Kuna mtoto wa shangazi yangu mmoja yeye ni nurse huko Geita anakwambia mama mtu mzima wa design hii akija kujifungua (wanawafahamu sana kwa maana vijijini watu ni wachache) huwa wanawachamba kwa maneno na lugha chafu mbele ya waume zao.

Kuna mama mmoja aliwahi kufariki mwaka 2006 alipokuwa anajifungua wakati bado tunakaa kule Keko. Sasa wakati wa mazishi watu wamekusanyika na wageni wanataka kujua chanzo cha kifo chake ikawa sasa ni aibu kusema kuwa amelufa kwa sababu ya "complications" za uzazi ilhali binti yake mkubwa ana mtoto wa miaka 2 tayari.

View attachment 1667341

Mimi binafsi ninaona sio jambo la hekima wala busara kwa mama/baba kuendelea kuzaa watoto wengine wadogo ilhali wale "first born" wamekwisha kuwa wababa/wamama wanaokaribia ku-reproduce.

Sio vizuri mama kuonekana ana tumbo kubwa la ujauzito pindi wale "first borns" wanapokuwa wamepevuka akili.

"HAPPY NEW YEAR 2021"

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Sasa shida ipo wapi mkuu?
Shida ni mwanamke kuzaa au shida ni binti yako kuolewa?

Kwani unachokifanya wewe kwa mkeo na anachofanya mume wa mkeo kwa binti yenu,,, kina tofauti tofauti gani?..

Kwahyo unamaanisha binti yako akiolewa na wewe umwache mama yake,,?
 
mwafrika mimi hata usiniletee habari hizo:

kama mama bado anayo mayai na yupo katika umri salama wa kuzaa na ninahitaji mtoto; anazalishwa mara moja.

kama mama ana miaka 35 na binti yake wa kwanza na pekee mwenye miaka 18 aliyempata akiwa na miaka 17 naye ni mjamzito.....wala sisiti kumpachika mimba kwa sababu hiyo. utakuwa ni ujinga kuacha kuijaza dunia kwa vijisababu ambavyo ni maoni 'opinion' tu za watu na sio 'fact'.

kwangu kipaumbele ni; je, tunahitaji mtoto? je, ni salama kwa mama kujifungua sasa? basi!

mkuu Jurjana, tujuze suala hili katika msimamo wa kidini tafadhali!!!
 
mwafrika mimi hata usiniletee habari hizo:

kama mama bado anayo mayai na yupo katika umri salama wa kuzaa na ninahitaji mtoto; anazalishwa mara moja.

kama mama ana miaka 35 na binti yake wa kwanza na pekee mwenye miaka 18 aliyempata akiwa na miaka 17 naye ni mjamzito.....wala sisiti kumpachika mimba kwa sababu hiyo. utakuwa ni ujinga kuacha kuijaza dunia kwa vijisababu ambavyo ni maoni 'opinion' tu za watu na sio 'fact'.
Sawa mzee baba. Sasa baada ya kuzaa na miaka hiyo 17 alikuwa anafanya nini hapa kati mpaka aje kuzaa mtoto wa pili na umri wa miaka 35?
 
mimi mtu anayezaa zaidi ya watoto 3 katika dunia ya sasa naona kama amekosa akili. zamani watu walikuwa wakizaa mitoto mingi kwa sababu elimu na njia za uzazi wa mpango kulikuwa hakuna, sasa hivi zipo tele, mtoto pia alikuwa akitumika kama rasilimali ya kulima shamba na kuchunga mifugo, saa hivi mtoto anatakiwa alishwe, avalishwe na asomeshwe vizuri sio kumtumikisha kuchunga ng'ombe
Aisee kila mtu nana Mungu .9((?.((.(,mimi nina watoto 5 wa 14yrs yupo form 2.. mwisho

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom