Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Haya mambo kama wewe huwezi, Basi nyamaza waachie wanaoona wanaweza....


Tusipangiane namna ya kuzaliana....
Tatizo wanawaletea shida wengine. Unazaa ukiwa na miaka 60 wakati huna uwekezaji wowote kuweza kuwasaidia hao watoto, unaishia kutengeneza migogoro kwenye familia na jamii kiujumla.
 
Sawa mzee baba. Sasa baada ya kuzaa na miaka hiyo 17 alikuwa anafanya nini hapa kati mpaka aje kuzaa mtoto wa pili na umri wa miaka 35?
changamoto tu za kimaisha; kuna magonjwa, kutengwa, uchumi n.k......

kwa sababu yoyote ile iliyokuwa, je azae huyu au asizae kisa mtoto wake nae anazaa?!!!
 
changamoto tu za kimaisha; kuna magonjwa, kutengwa, uchumi n.k......

kwa sababu yoyote ile iliyokuwa, je azae huyu au asizae kisa mtoto wake nae anazaa?!!!
Kama anajali maadili asizae tena kwa maana aliweza kukaa miaka 18 bila kuzaa mtoto wa pili sasa kwanini asivumilie miaka mingine 18 mbele? Kama anataka watoto alee yatima au watoto wa ndugu.
 
Kama anajali maadili asizae tena kwa maana aliweza kukaa miaka 18 bila kuzaa mtoto wa pili sasa kwanini asivumilie miaka mingine 18 mbele?
miaka 18 mingine mbele?!!!!! utakuwa unatania kiongozi.

yaani asizae kisa tu kuna wachache wenye mawazo yao hasi?!!!........isitoshe hizi desturi zinatofautinana kati ya sehemu moja na nyingine, kisicho sahihi kwako ni sahihi kwa mwingine.
 
Tuseme alizaa mtoto akiwa na miaka 18.

Sasa akiwa na miaka 40 binti ana miaka 22, sawa wote wanazaa sioni ubaya hapo.

Mmh hesabu yenyewe sijui nimepata.
Ni aibu kwa mama wa miaka arobain kuendelea kuzaa , Huu ni umri wa kula maisha , umri wa kuzaa ni miaka 15 mpaka 38, ndani ya iyo miaka unaweza kuwa na watoto Saba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
miaka 18 mingine mbele?!!!!! utakuwa unatania kiongozi.

yaani asizae kisa tu kuna wachache wenye mawazo yao hasi?!!!........isitoshe hizi desturi zinatofautinana kati ya sehemu moja na nyingine, kisicho sahihi kwako ni sahihi kwa mwingine.
Kama anataka watoto alee wa ndugu au yatima atapata thawabu kwa Mungu
 
Aisee ebu nieleze yangu,
Mimi ninao watoto 5 nina 42yrs sasa.First borne ana 14yrs yupo form 2,lastborn ana 4yrs yupo middleclass.
Nilimwomba Mungu sana nipate watoto 6 sasa nina watano.
Nilijitahidi sana kwa uwezo wake mola kujijenga kimaisha kabla sijaoa,so familia yangu imenikuta tayari nina kibanda na angalau kiusafiri cha kwendea kazini,kanisani nk.Nimeongeza familia pia nikaongeza miradi ya kudumu kwa ajili ya familia km vinyumba nyumba vya kupanga na kumfungulia mke kiduka ili apate pesa ya mboga na mahitaji yake madogomadogo.
Kilichobaki nimemwaahidi Mungu kuwajali watoto wangu na mke kwa namna yoyote ile wasome shule nzuri,chakula,malazi,mavazi na mahitaji yote ya msingi.
So mimi naamini watoto ni majaariwa na hakuna haja ya kuwabeza walio na watoto wengi km wamebarikiwa nao.
Mimi nina furaha na wanangu na nina wajibika nao 100%.Nipo kwenye utumishi mpk sasa na ninayafurahia Maisha haya na wanangu.
Note:Mungu umbariki kila mtu na uhitaji wake km una mtoto mmoja utepewa kwa kadri yako,km unao wengi Mungu anakujazia kwa kadri yako pia.

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Brother hili swala hutakiwi kugeneralize, siyo kila mtu hana uwezo wa kulea watoto zaidi ya watatu hadi Saba. Kinachotakiwa ni mtu kufanya tathmini ya hali yake kiuchumi kabla hajachukua maamuzi ya kuongeza idadi ya watoto na pia kuzingatia ushauri wa Afya kuhusu child spacing.

Kuzaa watoto ni baraka Kama una wezo wa kuwalea na kuwapatia mahitaji yao jinsi inavyotakiwa. Kwa hiyo hakuna limit kwamba mtu anatakiwa aishie kuzaa watoto watatu ndo aonekane kuwa anafuata uzazi wa mpango.
Imani za kizamani eti kuzaa watoto ni baraka
Halafu unaposema uwezo ni kitu relative mwingine uwezo kwake ni kuwapeleka watoto international school ndio anajiona ana uwezo, mwingine akiweza kuwalisha ugali maharage usiku naye anajiona Ana uwezo
Whatever the case 3 children should be a maximum for everybody
 
sasa ujinga gani, hujui familia kubwa ni faraja.
familia ikiwa ndogo sana misiba ikitokea huwa inachoma sana kwa maana mpo wachache, mkiwa wengi kuna amani na faraja fulani hivi

hivyo tatizo sio big family ni uwezo tu wa kulea, kama mtu ana uwezo azae tu, kama kina kardashian, ni wazungu ila familia ni kuubwa hadi inafurahisha ile ni faraja kubwa sana.
Kwan mkiwa wachache ama wengi wote si watakufa tu mnaweza mkawa wengi mkafariki wote kwa moto mara moja
 
Jichunguze utagundua kuwa wewe ndio huna akili.
Umekariri life ya kizungu bila kuchuja hata moja.
Km uchumi wangu upo stable acha nipate hata watoto 50.
Kupanga uzazi kwangu ni big NO!
Kwani wazungu ndio wanazaa watoto wachache peke yao? Nenda Korea, nenda Japan, nenda Qatar huko kote sio wazungu na wana familia ndogo, stable na zenye mafanikio, na future za watoto wao zipo guaranteed
Wewe umeweza tu kuwalisha ugali maharage unajiona una uweeeezoooo, eti uchumi wangu upo stable...
 
Aisee ebu nieleze yangu,
Mimi ninao watoto 5 nina 42yrs sasa.First borne ana 14yrs yupo form 2,lastborn ana 4yrs yupo middleclass.
Nilimwomba Mungu sana nipate watoto 6 sasa nina watano.
Nilijitahidi sana kwa uwezo wake mola kujijenga kimaisha kabla sijaoa,so familia yangu imenikuta tayari nina kibanda na angalau kiusafiri cha kwendea kazini,kanisani nk.Nimeongeza familia pia nikaongeza miradi ya kudumu kwa ajili ya familia km vinyumba nyumba vya kupanga na kumfungulia mke kiduka ili apate pesa ya mboga na mahitaji yake madogomadogo.
Kilichobaki nimemwaahidi Mungu kuwajali watoto wangu na mke kwa namna yoyote ile wasome shule nzuri,chakula,malazi,mavazi na mahitaji yote ya msingi.
Kaka mkubwa, sidhani kama umeisoma vema mada hii na ukaielewa...
 
Kama anataka watoto alee wa ndugu au yatima atapata thawabu kwa Mungu
akizaa wake na kuwalea kwa kuwa nafasi bado ipo, basi si thawabu tu atakazopata bali na furaha isiyo na kifani pamoja na uhakika wa usaidizi wa siku za mwisho za maisha yake
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu Watanzania;

Bado kuna watu wazima wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili.

View attachment 1667340

Siku ya sherehe ya mwaka mpya nilikuwatana na dada mmoja anaitwa Veronica (hili sio jina lake halisi) ambaye nilimaliza naye shule ya msingi mwaka 1999.

Huyu dada nilikwisha kutana naye mwezi kama wa August maeneo ya Banana Ukonga huku Dar. Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana miaka takribani 15 tulipiga story nyingi sana za zamani.

Sasa nilipokutana naye tena Ijumaa ya tarehe 01 January 2020 huku Kivule ninapokaa (kwa maana aliniambia anakaa Kata moja na mimi) nilimuona anaongozana na binti mdogo wa miaka kama 9 hivi.

Tena huyo binti wamefanana kweli kweli. Basi tulipoonana tulisalimiana tena kwa furaha sana. Baada ya story kadhaa nikamuuliza, huyu ndio mtoto wako wa kwanza? Akakataa. Akasema hapana, huyu sio mtoto wangu.

View attachment 1667350

Huyu ni mdogo wangu wa mwisho. Mtoto wangu ameenda kwa baba yake kusalimia atarudi shule zikifunguliwa. Sema ndio rafiki yake mkubwa sana huyu (mdogo wake wa mwisho) kwa maana wamepishana mwaka mmoja tu.

Mimi sikuwa na jambo lingine la kumwambia zaidi tu ya kumpa hongera lakini nikawa ninajisemea tu kimoyomoyo "ina maana haya masuala ya mtoto na mama kuzaa kwa pamoja bado yanaendelea katika karne hii ya 21?"

Hii issue nilikuwa ninaiona tu kwa wazee wa zamani ambapo unakuta mtu unakutambulisha "huyu ndio baba yangu mdogo/shangazi yangu tumbo moja na baba" au "huyu ndio mama yangu mdogo tumbo moja na mama" lakini ukijaribu kuwatazama actually wanalingana umri au wamepishana mwaka mmoja tu.

View attachment 1667352

Mimi ni moja kati ya watu wanaokerwa sana na lugha za hawa dada/mama zetu manesi lakini linapokuja suala la kukemea wamama/wababa wanaoendeleza utamaduni huu wa hovyo mimi ninawaunga mkono sana.

Kuna mtoto wa shangazi yangu mmoja yeye ni nurse huko Geita anakwambia mama mtu mzima wa design hii akija kujifungua (wanawafahamu sana kwa maana vijijini watu ni wachache) huwa wanawachamba kwa maneno na lugha chafu mbele ya waume zao.

Kuna mama mmoja aliwahi kufariki mwaka 2006 alipokuwa anajifungua wakati bado tunakaa kule Keko. Sasa wakati wa mazishi watu wamekusanyika na wageni wanataka kujua chanzo cha kifo chake ikawa sasa ni aibu kusema kuwa amelufa kwa sababu ya "complications" za uzazi ilhali binti yake mkubwa ana mtoto wa miaka 2 tayari.

View attachment 1667341

Mimi binafsi ninaona sio jambo la hekima wala busara kwa mama/baba kuendelea kuzaa watoto wengine wadogo ilhali wale "first born" wamekwisha kuwa wababa/wamama wanaokaribia ku-reproduce.

Sio vizuri mama kuonekana ana tumbo kubwa la ujauzito pindi wale "first borns" wanapokuwa wamepevuka akili.

Kwa maoni yako, ni sahihi mama na binti/mtoto kuendelea kuzaa kwa pamoja? Mtoto wa mwisho kulingana na mjukuu wa kwanza?

"HAPPY NEW YEAR 2021"

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Nosense., Haya mambo si ya kujadili na yaonekana wazi ata dini huna, na unafkiri kila kitu ulimwenguni kinaendeshwa ni mawazo binafsi ya mwanadamu, na ndio mana sasa ukijisikia unakuja hapa jf na kuandika tu chochote.
 
mimi mtu anayezaa zaidi ya watoto 3 katika dunia ya sasa naona kama amekosa akili. zamani watu walikuwa wakizaa mitoto mingi kwa sababu elimu na njia za uzazi wa mpango kulikuwa hakuna, sasa hivi zipo tele, mtoto pia alikuwa akitumika kama rasilimali ya kulima shamba na kuchunga mifugo, saa hivi mtoto anatakiwa alishwe, avalishwe na asomeshwe na utengeneze future nzuri kwa kuwekeza sio waje kutembea juani wakisaka ajira

Mwenzangu kama wewe huna uwezo wa kulea watoto zaidi ya watatu usiwaseme wenzio walio na uwezo hawana akili, eboo!!
 
Haya mambo si ya kujadili na yaonekana wazi ata dini huna, na unafkiri kila kitu ulimwenguni kinaendeshwa ni mawazo binafsi ya mwanadamu, na ndio mana sasa ukijisikia unakuja hapa jf na kuandika tu chochote.
Kuna uwezekano mkubwa sana hii mada ikakuhusu na inaonekana imekuchoma kweli kweli
 
Infantry,nimekuelewa mwenye mada vizuri ila nilikuwa najaribu kufanya quote ya jamaa mwingine anaeponda mzazi mwenye watoto zaidi ya 3 so mimi nimesahau kuunganisha ujumbe wake na wangu.Ujumbe wangu umekuja km wa mpinga mada.
Sawa mkuu, nimekuelewa ulikuwa unam-quote mtu ila kwa bahati mbaya ukakosea...
 
Back
Top Bottom