Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Kwahiyo unataka tusizae,halafu tufanyeje sasa wakati bado nguvu ipo na pesa zipo.Usizungumzie kirahisi tu kuzaa,inapaswa ujue ili uzae kuna kitu kinafanyika ndio mnazaa,kwahiyo unataka tuache...?
 
Nenda Simiyu uone hayo maajabu lakini so maajabu ni maboresho.
 
Kwanini usizae ukamaliza kabla binti hajapevuka?
maisha yana mambo mengi kunatime mimba zinazngua kutokea kutokana na mambo mbalimbali ya kimaisha, kuna kujipa pause ili kutafuta maisha, kuna vifo so tunaziba pengo la waliotangulia mambo ni mengi aseeh so kama uwezo upo tunafyatua tu kwanza elimu bure.
 
Mkuu, kwa hiyo mwanaume aliyeoa binti yako anakuja kumpa hongera mkeo (mama mkwe wake) kwa kujifungua mtoto mchanga (shemeji yake)?
 
Hasara ya kuchelewa kuoa halafu mtu anataka watoto 8.
 
Sasa na wale wanao owa mke mdogo umri chini ya mtoto wake wa kwanza wa kumzaa kwa miaka 10?
 
Mkuu acha Wivu
 
wazae tu hakuna shida ila wahakikishe wanawalea ipasavyo hao watoto maswala ya kufa mtoto akiwa Bado hajajitegemea wayaache.
 
Hizi kauli za kikoloni ziacheni huko, mnatawaliwa mpaka mnashindwa kufanya maamuzi yenu binafsi, kwani mke wangu kubeba ujauzito hata kama binti yake yake naye ana ujauzito shida nini? Mazingira ya vijijini msichana anaolewa akiwa na miaka 18, akipata mtoto akiwa na miaka 19 manake binti yake anaweza kubeba ujauzito yeye akiwa na miaka 39, kuna tatizo gani endapo ana afya njema kubeba mimba na miaka 39,41,42 ...., huyo binti yangu ana maisha yake nami nina maisha yangu.
Wengi wenu mnapiga kelele sababu kubwa mmefanya wazazi wenu ndo wa kulea watoto wenu, hivo ukiona naye ana mtoto wake roho inakuumeni, mnakuja na sababu zisizo kuwa na mashiko hata kidogo.
Mimi na mke wangu tutazaa mpaka tuamue hatuwezi kupangiwa na watoto, mbona kufanya ngono hamuachi mkasubiri ndoa?
 
Inategemea na mazingira na familia yako ikoje.
Ndugu Marehemu Mengi alipoona hana wajukuu akaaamua kutafuta wajukuu yeye mwenyewe. They are now 6/ 7 years old.

Was it at all worth it or even at least fair? hasa kwa hao watoto? Imagine wanaenda kuishi maisha yao yote bila baba (japo his legacy will console them) lakini nani asiyejua thamani ya baba katika malezi hasa dunia ya sasa?

Kama wanaadam wakati mwingine ni lazima tujilazimishe (force our selves) kuifikira kesho hata kama inauma kiasi gani! Tujipe muda wa kuwafikira hao watoto as binaadam wa baadae na aina ya binaadam tunaotaka wawe!

Matatizo mengi sana ya kisaikolojia yanayotukuta ukubwani , hasa kwa familia zetu masikini, yameletwa na tullivyokuja duniani na tulivyoandaliwa kuiface dunia!

Kama unahitaji watoto wengi basi anza mapema ili ujipe muda wa kuwatafutia na kuwawekea misingi imara ili waanzapo kujitambua wasikwame na kurudia mzunguko ule ule wa enzi na enzi!
 

Naunga mkono!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…