Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Kila mtu na maisha yake..... Muhimu wapate mahitaji yao ya muhimu... Mengi alizaa mapacha akiwa na miaka karibia 70.. na hakuna aliyeshangaa... Ila akizaa mchovu kelele mji mzima..
 
Huku kwetu vijijini tuna uwezo huo, chakula tele mashamba na hata nguvu pendwa uhakika... huko mjini dhiki nyingi chumba kimoja cha kupanga unadhani wote tunaishi hivyo?
Maziwa unakamua tu kwa ng’ombe au mbuzi
Nyama ya kuku au bata bwelele
Nyumba unaamua ukate vyumba vingapi

Kijijini ni raha sana.
 
Jichunguze utagundua kuwa wewe ndio huna akili.
Umekariri life ya kizungu bila kuchuja hata moja.
Km uchumi wangu upo stable acha nipate hata watoto 50.
Kupanga uzazi kwangu ni big NO!

Uko sahihi, kama uwezo unaruhusu zaa sana tena sana ila pia jaribu kuweka mipangilio katika kuzaa kwako!

Anza mapema kisha maliza mapema ili kujipa muda wewe wa kutafuta na kujenga misingi imara ya familia ili hata kuanzia mwanao wa mwanzo apate muda wa kufundishwa na mwalimu wake wa kwanza maishani (baba & mama)!

Tusijisahau familia sio baba mama na watoto tu , maana kadri muda unavyosogea wajukuu na wakwe wa kike na kiume nao wataongezeka kuwa sehemu ya hiyo familia! So ulezi bado unaendelea!

Otherwise make your grand kids your kids, there is wisdom in that!
 
Haipendezi ,wazazi wa zamani walikuwa wanatwanga fasta fasta ,wanapishana mwaka mmoja hadi miwili anazaa watoto wa5 hadi 10. ukipiga gap hapo Mtoto wa kwanza hadi wa mwisho wanapishana miaka 10 hadi 15......Hadi Mtoto wa kwanza anaoelewa/oa lets say miaka 24 hapo mtoto wa mwisho anakuwa na miaka 9 ambapo Mama mtu alishafunga uzazi miaka 9 iliyopita.
 
Huwa ninajifunza mengi sana kupitia uandishi pamoja na ideas zako. Be blessed.
 
Tatizo wanawaletea shida wengine? unazaa ukiwa na miaka 60 wakati huna uwekezaji wowote kuweza kuwasaidia hao watoto, unaishia kutengeneza migogoro kwenye familia na jamii kiujumla.


Na huu ndio mzizi wa umaskini katika familia zetu nyingi!

Mtu tangu kabaleghe yeye anafanya kazi ya kuzalisha na kulisha kiasi kwamba hata muda wa kulea na kuwekeza zaidi hautoshi na rasilimali ni ndogo kuja kushtuka yuko na 50 years!
Bado atatoka kwenda kufuata mwari mpya nako ni kazi ya kuzalisha na kulisha kiasi inapungua nguvu sio kama zamani!
Watoto wakubwa wanapata majukumu ya familia ya pili ya baba then the circle continues!

Wachache sana wanaofanikiwa kujitoa katika huu mnyororo!

Tuzae hata watoto ishirini, ila kwa mpangilio na uwezo!!
 
USITUPANGIE,
 
changamoto tu za kimaisha; kuna magonjwa, kutengwa, uchumi n.k......

kwa sababu yoyote ile iliyokuwa, je azae huyu au asizae kisa mtoto wake nae anazaa?!!!


Binafsi mimi nisingezaa tena! Ningesubiri wajukuu!

Hao ningewafanya wanangu na pia kwa mzazi kupata Mjukuu ukiwa bado na nguvu basi ni kama baraka!

It’s like getting a second chance to create a whole human being again, kwa kutumia ujuzi na makosa ya zamani kufanya bora zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…