Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Nchi yenye chuki ya kiwango hiki haiwezi kudumu ni suala la muda tu we Chato yao watakuwa huru na sisi wa Mtemi Mkwawa tutakuwa na nchi yetu.
Kwanini hii chuki mnaiona nyie pekee?

Mbona sie watu wa iringa, mbeya, mara, mtwara na kwingineko hatuoni hii chuki?
 
Haiwezekani kila mtu akawa anajipangia Cha kufanya ndio maana Kuna vipaombele vya kitaifa vinavyoratibiwa na wataalamu wa uchumi baada ya kufanyia utafiti mahitaji ya msingi ya wananchi.Kujenga viwanja ni upuuzi Kama huu tu wa madaraja.

Serikali umejenga vituo vya afya Kama 500 hivi umesikia nani anapinga? Sera ya afya ni kituo cha afya kila kata lakini Kuna zaidi ya kata 2000 hazina vituo vya afya hapo bado zahanati kila Kijiji nk

Hiyo pesa ingetisha vituo vya afya 120 kwa Bei ya serikali ya mln 500,huoni tungeendelea kupunguza tatizo?
Nyie sifia sifia mnauzi sn. Vituo vya afya bila wahudumu bila madawa si ni km mabanda ya kufugia kuku tu?
Shule hazina waalimu hazina vifaa sasa si ni km mabanda ya ng'ombe tu?

Hayo ni maendeleo ya vitu tu.

Poor healthy services
bora elimu badala ya elimu boda
 
Hii ndio sababu inayosababisha chadema isijenge ofisi?

Nmeona humu mnashangaa mi v8 inayotumika kwenye kampeni za mgombea wa ccm nikawaambia hata chadema ingekuwa na matumizi mazuri ya ruzuku mngekuwa na kama yale angalau ma 3.

Lakini ona aibu inyowakumba! Wagombea wenu huku mitaani njaa kali hata kufanya kampeni wanashindwa hawana pa kuanzia.
Kwamba chadema hawana ofisi? Mbona viongozi wetu tunakutana nao ofisini? Umewahi kusikia mwananchi ameshindwa kuona na kiongozi wa Chadema eti kuna mahali hakuna ofisi. Hizo shida utazikuta CCM tu wanajifanya wana ofisi lkn hawawezi kuhudumia wananchi ndio maana watz hawataki kusikia hbr za CCM.

Kwanza CCM hayo majengo ni kwa ajiri ya kujadiri kupiga diri za kifisadi km ununuzi wa ndege, majenzi ya chato na uchafu mwingine wote sasa mnafaida gani kua na hizo ofisi ambazo ni mali ya umma.
 
Kwamba chadema hawana ofisi? Mbona viongozi wetu tunakutana nao ofisini? Umewahi kusikia mwananchi ameshindwa kuona na kiongozi wa Chadema eti kuna mahali hakuna ofisi. Hizo shida utazikuta ccm tu wanajifanya wana ofisi lkn hawawezi kuhudumia wananchi ndio maana watz hawataki kusikia hbr za CCM.

Kwanza ccm hayo majengo ni kwa ajiri ya kujadiri kupiga diri za kifisadi km ununuzi wa ndege, majenzi ya Chato na uchafu mwingine wote sasa mnafaida gani kua na hizo ofisi ambazo ni mali ya umma.
Hata ukiweka kiti chini ya mti hiyo ni ofisi,

Basi endeleeni kufarahia wana chadema.
 
Niliposoma hapo ulipoandika hili eneo lina watu wa kipato cha chini nikagundua uzi wako wote utakua hauna maana nikaacha kusoma.

Nadhani wewe utakuwa huna ufahamu wowote juu ta mikoa ya kanda ya ziwa na watu wake, hasa Mwanza na Geita na unaishi maisha ya kukariri kama sio kusikia.

Kwa taarifa yako hilo daraja likikamilika Mabasi yatatoka Mwanza hadi Kigali, Bujumbura na Kampala yatapita kwa urahisi sana na hii italifungua sana jii la Mwanza.
 
Hizo hela ni bora angejenga viwanja vya mpira kila kuboresha industry ya football ili kupunguza hii concepts za kukosa ajira yaani CCM hovyo tu.

Tukisema kuwa Magufuli ni mkurupukaji na alipaswa kuwa Mnyapara wa KUSIMAMIA BARABARA na si kumpa Ikulu wanabisha!!
Watu aina ya Magufuli wanatakiwa kusimamiwa yaani wawe chini ya mtu fulani awatume na kuwasimamia tu.

Haiwezekani 700 Bilioni uziteketeze kwenye Daraja la Busisi ambao halina Tija kabisa. Mbaya zaidi hakuna Bunge la Bajeti lililokaa kupitisha hiyo Fedha. Kweli huyu ni Rais wa ajabu ambaye Tanzania haijawahi kuwa naye!
 
G Sam,

Magufuli anastahili pongezi kubwa sana kwa ujenzi wa hilo Daraja la Kigongo-Busisi maana litakuwa ni mkombozi kwa wakaazi wa Mwanza, Sengerema na wa Mikoa mingine watakaopita njia hiyo.

Pia litapanua wigo wa biashara kati ya Mwanza na maeneo ya kuzunguka daraja hilo, kama hiyo haitoshthamani ya ardhi katika maeneo ya kuzunguka kivuko hicho imepanda na wananchi wengi wanaanza kuwekeza Mahoteli na biashara mbalimbali maeneo hayo kwani kufikika maeneo yote hayo itakuwa ni rahisi kuliko vikwazo vya awali vya kusubiri Vivuko.

Shime Watanzania MITANO TENA TUMPE JPM ili amalizie kazi alizokwishazipanga. Halafu kuhusu mikopo kwa hao watu unaowaita wa kipato cha chini, Mabenki yapo kwa kazi ya kutoa mikopo lakini pia kwa taarifa yako wale watu wa maeneo hayo si kwamba wana kipato cha chini bali wako vizuri sana, labda wewe unawalinganisha na watu wa wapi?
 
Mantiki hiyo utaipata tarehe 2 Nov tukisha mwapisha rais Magufuli.
 
Suala siyo DARAJA,

je, KIPAUMBELE KWA ENEO LA KANDA YA ZIWA NI DARAJA?
Labda kipaumbele cha Kanda ya Ziwa ni Ubwabwa na Vipapatio vya Kuku vya Ashim Rungwe maana kwa ujenzi wa Daraja hilo kutafungua njia nyingi za biashara na Mataifa jirani kama Uganda, Burundi, Rwanda, Kongo na kwingineko.
 
Kwenye hili siko nanyii kabisaaaaa, na tena for sure wewe utakuwa ni muchagga muuzza duka tuuu, kwa hiyo watu wa kanda ya ziwa hawatakiwi kujengewa daraja na SG reli? Piiga ua apo lazima tu tofautiane.
 
G Sam,

Katika hili naomba nitofautiane na wewe! Watu wanapoteza muda mwingi sana kusubiria ferry. Likikamilika litafupisha muda wa safari kati ya maeneo mengi na Mwanza. Kama ukishasafiri na bus kutoka Bukoba kuja Mwanza lazima ukubali mara nyingi watu wanajaa zaidi ya saa 1 kusubiria ferry! Wacha ukamilike!
 
Kwa hili nami natia hoja hapa;

Ujenzi wa daraja la Busisi-Kigongo sio kweli kwamba hauna umuhimu kama wachangiaji wengi wasemavyo ila tujaribu kuangalia kwa mapana sana huku tukihusianisha gharama, mahitaji na alternatives ya mahali husika.

1. Kwa sasa mradi huu wa Tshs.700b kwa ujenzi wa daraja tena sehemu moja tu mimi naona ni matumizi yasiyokuwa na tija. Hii ni pesa nyingi sana kwa eneo hili ikiishia kwenye mradi mmoja tu huku ikiacha changamoto zingine lukuki za eneo hilo.

Maeneo ya kanda ya ziwa bado kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi majumbani hasa kwenye maeneo hayo hayo ya Misungwi, Sengerema, Geita, Nyamagana n.k kwanini pesa hii isitatue changamoto hii kwanza?

Maeneo mengi ya kanda ya ziwa bado barabara ni changamoto, ni mbovu na hazina lami ambapo kama inshu ni kuwahisha wagonjwa Bugando bado wengi wanacheleweshwa na barabara mbovu huko watokako kwanini pesa hii isitatue changamoto hii kwanza?

Ni kweli kusubiri vivuko pale ni kero kubwa sana lakini hili linatatulika kwa kuongeza idadi ya vivuko kuendana na mahitaji, hakika pale vikiongezwa vivuko vingine kama viwili au vitatu vyenye ukubwa na speed ya kutosha hakutakuwa tena changamoto ya foleni mahali pale ambapo ujenzi wa vivuko hivyo hauzidi bilioni 5 kwa kila kimoja pesa ambayo ingeweza kutumika haizidi bilioni 15 na kuacha hela zingine zikaingia kwenye hiyo miradi ya maji na ujenzi wa barabara za lami kanda ya ziwa.

Shida ninayoiona mimi ni maamuzi ya nchi hii kuwa ni ya mtu mmoja mwenye madaraka na mamlaka makubwa sana, akiamua tena majukwaani tu bila kutumia vyombo vya ushauri hili linatugharimu kama taifa. Watendaji wengine wamekuwa ni waoga kushauri kitaalamu maana hawawezi kumkosoa boss wao( kushauri maamuzi ya mkuu ni kumkosoa).

Turudi kwenye uongozi unazingatia kanuni za kiuongozi laiti kama ungewasikiliza wanakanda ya ziwa mahitaji yao nadhani daraja hilo si kapaumbele kikubwa kwa sasa japo kwa baadae ni sawa kabisa.
Mkuu umesema vema kabisa! na hili ni jibu tosha kabisa kama tukiweka ushabiki pembeni, kama taifa bado tunazo changamoto nyingi kuizamisha pesa hii yote sehemu moja ni hatari sana na kama rais kama kweli alikuwa na maono mazuri basi pesa za ule uwanja wa chato ndiyo angezitumia kujengea hilo daraja.
 
G Sam,

Hoja yako ni njema lakini ingekuwa na nguvu zaidi ungejadili au kujibu hoja za “devils’ advocates”

1. Kivukoni kina chukua muda gani kuvuja abiria na mizigo, hufanya kazi saa ngapi kwa siku, magari mangapi na abiria wangapi kuvushwa kwa siku?
2. Magari ya abiria yatachukua muda gani kuvuka daraja, kuokoa muda kiasi gani kwa siku (saa 24) na magari, abiria na tani ngapi za mizigo kwa siku
3. Kokotoa faida au hasara kuvuka kwa kivuko vs kuvuka kwa daraja kwa siku, mwezi na nwaka. Je mradi unalipa au hasara?
 
Back
Top Bottom