Bado nazidi kuona makosa makubwa kwenye usajili wa Simba. Kwa mwendo huu mashabiki jiandaeni maumivu tena na tena 2023-24

Bado nazidi kuona makosa makubwa kwenye usajili wa Simba. Kwa mwendo huu mashabiki jiandaeni maumivu tena na tena 2023-24

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2020
Posts
8,542
Reaction score
18,340
Habari ndugu ZANGU.
Mimi ni mdau WA soka.
Na mpenzi na mdau wa Simba.

Nimekuwa nikifuatilia usajili HASA WA wachezaji wa KIGENI ndani ya simba.

NIMEWEZA KUYAONA MAKOSA YAFUATAYO KIUFUNDI.

1. KOSA kubwa la Kwanza ni KUMUACHA Golikipa Beno kakolanya., Hivyo wanalazimika KUSAJILI Golikipa wa kigeni. Baada ya Manura KUUMIA. (Santos)
Hivyo kujinyima WiGo WA wachezaji wa ndani.

2. KOSA la pili Kukosa beki MBADALA WA KIGENI WA Che Malone na Inonga Incase Wana Kadi au WAKIUMIA.

Na hapohapo wamekosea MBADALA WA Mohamed Hussen.
YAHAYA mbegu ameng'ang'ania SINGIDA akiwa na GADIEL Michael ALIYE ondoka.

3 . KOSA KUBWA KABISA KABISA NI KUKOSA BACKBONE YA TIMU/ UTI WA MGONGO WA TIMU KIUNGO MKABAJI CDM 6
Tangu AMEONDOKA LWANGA , mkude, Nyoni na sawadogo hakuna MBADALA wao.

Japo Kunatetesi na Unafuu nasikia NGOMA amesaini Simba hii itakuwa nafuu Ila NGOMA ni 8.

4. KOSA LINGINE ni kujaza idadi kubwa ya Mawinga
I. Saido.
Ii. Onana.
Iii. kibu Denis
Iv. Sakho, Banda
V. Chama.
Vi Aubin Kramo.

5. KOSA LINGINE usajili WA mshambuliaji mmoja tu no 9. Jean Baleke.
Boko AMEISHA.
Ile Simba ya Makombe ilikuwa Kagere, Boko na mugalu saizi ni Baleke pekee

6 . Kidogo wamenifurahisha kwenye no 10.
Phili, Saido, chama.

MAKOSA NI MENGI MNO MUDA NI MCHACHE.
SIMBA NA ROBERTINHO REKEBISHENI HAPA.
USHAURI WA BURE. MSIJE MKAANZA LAWAMA.

NAFASI ,ZA KIGENI NI 12 TU.
NA ZIMEISHA.

Naomba Uzi Huu ujadiliwe na wanaojua mpira tu sio mashabiki Maandazi
 
Umekuwa na haraka utafikiri umeshaambiwa kuwa ndio mwisho wa kusajili. Kuwa mvumilivu hadi ifikie uongozi umetamatisha usajili.
Sio mpaka uwe na elimu kubwa ya mpira ndio ung'amue mambo, Simba anasajili wachezaji 5, na wachezaji hao keshasajili 3 tiyali ambao wamekamilisha idadi ya wachezaji 12, kwa maana iyo inabidi wawakate wachezaji wengine 2 ili kumuingiza kipa na kiungo, kipa atachukua nafasi ya sakho anayeuzwa na kiungo pia itawabidi wamkate banda ili aingie, baada ya hapo akuna mchezaji mwingine wanayeweza kumkata
 
Usajili haujaisha ....
Ligi haijaanza.....
 
Nafasi za Banda na Sakho watachukua Ngoma na Santos. Back up ya Baleke atakua Phiri and the vice versa. Pia unajua kua Ngoma ni kama Bangala pale Yanga? Ana uwezo wa kucheza kiungo na beki wa kati. Hivyo badala ya kusajili beki mwingine wa kati, Ngoma atatumika kama back up ya Inonga na Malone huku akiongeza ushindani wa namba eneo la kiungo ya chini.

Ikumbukwe Simba itasajili wachezaji wazawa ikiwemo beki wa kati mwingine.
 
Msiwe mnaanzisha nyuzi halafu mnatisha kuchangia watu wenye mawazo tofauti. Anyway, nakubaliana na wewe kwenye upande wa kipa na beki 3.
 
Mimi nalia na no 6 jaman kipind cha Lwanga tuliruhusu magolo machache
Tunahitaj 6 anayelinda mabeki
Ngoma/Mzamiru na Kanoute wote no 8

Hakika mkuu Tena kwa Bahati Mbaya nafasi zimejaa.

Kunauwezekano WA KUMUACHA Banda na KUMSAJILI Golikipa.

Kumuuza SAKCHO na KUMSAJILI Fabrice NGOMA no 8.

MAKOSA MAKUBWA Sana nayaona.
 
Niliomba Uzi Huu ujadiliwe na wanaojua mpira na si shabiki Maandazi.

TAFADHALI weka USHABIKI pembeni tujadiri fact.

Ukijiona HUWEZI kaa pembeni
Wewe unalugha ya kwenye kahawa. Lini uliujua huo mpira?
 
Back
Top Bottom