Sababu ya kifo cha Scandinavian ni baada ya mmiliki kujiingiza kwenye siasa za kijinga huku akijua analo deni beki ya ADB, ADB walikuwa wanamdai yeye akachukua mabasi kuwapeleka bure wanaccm Rufiji kuzindua daraja la Mkapa, mabasi yaliporudi ADB ikakamata mabasi yote ya Scandinavian na kuyafungia kwenye yadi ya serikali Temeke kusubiri mnada, huo ndio ulikuwa mwisho wake.
Kilichomponza ni kudhani kuwa CCM itaiambia benki mwacheni huyu ni mwenzetu, lakini ADB haiko Tanzania hivyo haiwezi kujua kama ni mwenzao.