round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Tukiangalia majina karibia yote ya mikoa yana asili ya hapa kwetu iweje jiji kubwa nchini na Africa Mashariki tubaki kungangania jina la kikoloni lenye historia ya kitumwa ?
Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said
Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."
Sultani Majid alikuwa akifanya biashara ya kikatili ya utumwa iliyomtajirisha, Bandari aliyotumia aliisifia kwa kuiita Dar Es Salaam, kwa tafsiri ya kiswahili ni bandari salama, alisafirisha babu na bibi bila bugudha ndio maana akapaita Dar Es salaam,
Ni sehemu ambayo Sultan aliitumia kwa namna moja au nyingine kutumia bandari kujitajirisha na biashara yake ya kikatili iliyotumikisha babau zetu mashambani kwa mijeredi mashambani, babu zetu walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao ( utaowakuta ni waafrika waliohamia kuanzia miaka ya 70s)
Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA