Bado tupo utumwani? kwanini tunasita kubadili jina la jiji kubwa zaidi Afrika mashariki

Kuacha kuhakikisha vitu vya msingi kama maji kutoka 24/7/365 days na kuongeza barabara za ring road plus kupanga mji ili kulifungua jiji wewe unalilia vitu vya ajabu kama Jina.Sasa ukibadili jina unapata nini wakati mnashida kibao zinawazonga.Waafrika ni lini mtaweza kuadress critical issues na kuachana na INFERIORITY COMPLEX.
 
 
Hili jengo la sasa la Ikulu inasemwa lilijengwa na British architect John Sinclair baada ya ngome ya Mjerumani kuharibiwa.
Sasa mpaka hapo ushakubali kulikuwa na ngome ya Wajerumani.

Na Wajerumani nao walikuta jengo la Waarabu alilojenga Sultan Majjid. Hapo Ikuku Dar palikuwa na jengo la chuo cha kujifunza Uislamu hapo.
 
Hakuna uthibitisho wa hiyo ikulu kama ilivyo kuwepo hapo kabla ya Wakoloni wa Ujerumani au Uingereza. Hili suala nalichukulia kama ilivyokuwa Ikulu ya Dodoma kabla Magufuli hajajenga hii ya sasa jinsi ilivyo, Chamwino kulikuwa na Ikulu kabla ya Magufuli lakini anayechukuliwa kujenga Ikulu ya Dodoma ni Magufuli.
 
Bombay ilibadilishwa kuwa Mumbai,
Harare zamani ilikuwa Fort Saalisbury
Instanbul zamani ilikuwa Constantinople
Gold Coast ilibadilishwa kuwa Ghana
Toronto ilikuwa York zamani
Hii dhana ya kufanya mambo kisa flani alifanya ni namna mufilisi kabisa ya kutetea hoja.

Njooni na athari na faida za kiuchumi kwa nchi kubadili jina la mahali acheni blaaablaaaa.
 
kamuite mtoto wako "abeed" jina lililotumika kuwaita watumwa weusi,

Tuna matatizo ya muhimu kama maji, jina lolote linaweza kumfaa mwanao
 
Mawazo mfu, mnawaza kubadilisha majengo na vitu majina baadae mnasifia kuwa mnaleta maendeleo. Wenzenu waliwaza kujenga SGR, Kufufua Air Tanzania, kujenga uwanja wa msalato, kujenga Ikulu mpya Dodoma, kujenga mji wa Serikali Dodoma na JNHEPP. Jina hata wewe unaweza kubadilisha ila halifuti jina la awali kwa wale waliokufahamu tangu awali.
 
Sasa mpaka hapo ushakubali kulikuwa na ngome ya Wajerumani.

Na Wajerumani nao walikuta jengo la Waarabu alilojenga Sultan Majjid. Hapo Ikuku Dar palikuwa na jengo la chuo cha kujifunza Uislamu hapo.
Basi Wajerumani walijenga kwa ukubwa na ufahari zaidi kuliko vijengo walivyovikuta hapo ndio maana wanachukuliwa kama wajenzi wa hiyo Ikulu.
 
Hiyo Ikulu kama ilivyo leo hata huyo Mjerumani na Muingereza hawajaijenga hivyo.

Hata Nyerere, Mwinyi na Mkapa hawajaijenga hivyo.

So where do you draw the line and how?
 
Basi Wajerumani walijenga kwa ukubwa na ufahari zaidi kuliko vijengo walivyovikuta hapo ndio maana wanachukuliws kama wajenzi wa hiyo Ikulu.

Sawa.

Ukikubali point hii utakuwa umekubali pia kuwa Sultan Majjid alikuta kijiji cha Mzizima akajenga kwa ukubwa na ufahari zaidi mji wa Dar es salaam.

Checkmate.
 
Hiyo Ikulu kama ilivyo leo hata huyo Mjerumani na Muingereza hawajaijenga hivyo.

Hata Nyerere, Mwinyi na Mkapa hawajaijenga hivyo.

So where do you draw the line and how?
Rais gani amejenga Ikulu ya Dodoma?
 
Utumwa utakuwa kichwani kwako vile unajiona mtumwa na utatenda sawa na watumwa mbele ya waarabu hadi leo.

Jina linabaki kama utambulisho wa mtu au mahali ili watu wapatofautishe na mahali pengine. Nani aliipa jina hiyo sehemu inabaki kuwa historia. Tulikuwa na stendi ya mkoani inaitwa Mbezi Luis sasa hivi ni Magufuli na watu wamekubali jina hilo kuwa ni kituo cha kukutania kwa safari au mambo mengine.

Ukiwa na akili ya kitumwa utawaza kila kitu kwa mtizamo wa kitumwa. Au maskini kwa mtizamo wa kimaskini. Badili mtizamo.

Mfano.

Bwagamoyo........ Bagamoyo.
Watumwa walibwaga mioyo yao wakiingia kwenye boti kwenda utumwani.

Saa Dani...... Saa ndani.
Mwarabu akiishi eneo ilipo hifadhi ya Saadani kwa sasa alikuwa akiwajibu watu wanaomuuliza ni muda gani sasa, yeye anajibu saa dani yaani saa ipo ndani.

Msasani .......... Musa Hasani
Eneo hili akiishi ndugu mmoja akiitwa Musa Hasani. Ndipo pakawa maarufu Msasani.

Mnyamani....... Mwinyi Amani
Soko la Buguruni Mnyamani likipewa jina la mtu maarufu hapo Mwinyi Amani.

Nhobora .......... Tabora
Hinyanga.......... Shinyanga
Ng'wanza ........ Mwanza
Geta ............ Geita
Gahama ....... Kahama
Idodomya...... Dodoma

Ukiangalia yote hayo majina ya upande wa kushoto ya asili yana maana, lakini yalikuja kubadilishwa na wageni kwasababu ya kushindwa kutamka kwa Lugha za wenyeji. Lakini vile wao ndio walikuwa watawala enzi hizo ilibidi vitabu viandikwe kwa kufuata maelekezo yao. Ni sawa na leo flyover ya Ubungo tunaiita Kijazi kwa kuwa watawala waliamua iwe hivo.

Futa utumwa kichwani ufurahie maisha
 
Sawa.

Ukikubali point hii utakuwa umekubali pia kuwa Sultan Majjid alikuta kijiji cha Mzizima akajenga kwa ukubwa na ufahari zaidi mji wa Dar es salaam.

Checkmate.
Mkuu mimi nimeuliza legacy ya Sultan Majjid kuonyesha alifanya cha maana Dar Es Salaam kuweza kuchukuliwa kama mwanzilishi wa mji, hata Ikulu yenyewe haiwezi kuwa legacy yenye uzito ya maana. Wakoloni wazungu tunaona walianzisha mipango miji, administrative structures, ujenzi wa miondombinu(majengo, bandari na reli), shule n.k Sultan yeye legacy yake ilikuwa ni nini kusema ameanzisha mji wa Dar es Salaam??
 
Hayo majina mengi uliyoweka yana asili ya hapa kwetu nakuongezea na Mbeya ilikuwa inaitwa Ibheya, maana yake mji wenye chumvi, Nairobi hapo kenya neno la kimasai lenye maana Maji baridi,

Majina mengine ni Carrier Corps sisi tuliita kariakoo,

Shida ni hio Dar es salaam, mtu alipaita kwasababu palikuwa ni salama kwa biashara zake za kuumiza babu na bibi zetu, ni sawa na muuza viungo anaisifia bandari fulani ni salama kwasbabu hapati bugudha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…