Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Ikulu gani ya Dodoma?Rais gani amejenga Ikulu ya Dodoma?
Dodoma kuna Ikulu tangu utawala wa Nyerere.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ikulu gani ya Dodoma?Rais gani amejenga Ikulu ya Dodoma?
Wewe unashida mahali ebu nenda kamuone daktari kwa ushauri zaidi😀kamuite mtoto wako "abeed" jina lililotumika kuwaita watumwa weusi,
Tuna matatizo ya muhimu kama maji, jina lolote linaweza kumfaa mwanao
Mkuu,Mkuu mimi nimeuliza legacy ya Sultan Majjid kuonyesha alifanya cha maana Dar Es Salaam kuweza kuchukuliwa kama mwanzilishi wa mji, hata Ikulu yenyewe haiwezi kuwa legacy ya maana. Wakoloni wazungu tunaona walianzisha mipango miji, administrative structures, ujenzi wa miondombinu(majengo, bandari na reli), shule n.k Sultan yeye legacy yake ilikuwa ni nini kusema ameanzisha mji wa Dar es Salaam??
hivi wewe jina lako la kwanza unaitwa nani?Tukiangalia majina karibia yote ya mikoa yana asili ya hapa kwetu iweje jiji kubwa nchini na Africa Mashariki tubaki kungangania jina la kikoloni lenye historia ya kitumwa ?
Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said
Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."
Sultani Majid alikuwa akifanya biashara ya kikatili ya utumwa iliyomtajirisha, Bandari aliyotumia aliisifia kwa kuiita Dar Es Salaam, kwa tafsiri ya kiswahili ni bandari salama, alisafirisha babu na bibi bila bugudha ndio maana akapaita Dar Es salaam, sehemu ambazo babu zetu walifikia wamechapwa sana mijeredi, wamelimishwa sana mashambani, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao, utaowakuta ni waafrika waliohamia kuanzia miaka ya 70s
View attachment 3250594
Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA
Naam mlifanyie kaziTukiangalia majina karibia yote ya mikoa yana asili ya hapa kwetu iweje jiji kubwa nchini na Africa Mashariki tubaki kungangania jina la kikoloni lenye historia ya kitumwa ?
Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said
Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."
Sultani Majid alikuwa akifanya biashara ya kikatili ya utumwa iliyomtajirisha, Bandari aliyotumia aliisifia kwa kuiita Dar Es Salaam, kwa tafsiri ya kiswahili ni bandari salama, alisafirisha babu na bibi bila bugudha ndio maana akapaita Dar Es salaam, sehemu ambazo babu zetu walifikia wamechapwa sana mijeredi, wamelimishwa sana mashambani, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao, utaowakuta ni waafrika waliohamia kuanzia miaka ya 70s
View attachment 3250594
Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA
Ongezea Tanganyika Sasa hivi inaitwa Tanzania! Maana kule Zanzibar wakija bara,huwa wanasema wanakuja Tanzania.Bombay ilibadilishwa kuwa Mumbai,
Harare zamani ilikuwa Fort Saalisbury
Instanbul zamani ilikuwa Constantinople
Gold Coast ilibadilishwa kuwa Ghana
Toronto ilikuwa York zamani
Mi ndio nimeshangaa mtoa mada alivyo lipamba mwanzoni nikahisi analizungumzia NEW YORK CITY ila nikashangaa anazungumzia Dar es salaam. Huyu jamaa amekosa exposure na usikute katokea mkoani hukoJiji la hovyo sana .mpangilio wa makazi ni hovyo.Tunazidiwa na jiji zuri la Kigali na Bunjumbula
Mbona Hinyanga kwa sasa Shinyanga napo walipaita hivo sababu ya kuwa walikuwa wanakutana hapo kwenye mnyaa mkubwa. Hinyanga maana yake kwenye mnyaa.Hayo majina mengi uliyoweka yana asili ya hapa kwetu nakuongezea na Mbeya ilikuwa inaitwa Ibheya, maana yake mji wenye chumvi, Nairobi hapo kenya neno la kimasai lenye maana Maji baridi,
Majina mengine ni Carrier Corps sisi tuliita kariakoo,
Shida ni hio Dar es salaam, mtu alipaita kwasababu palikuwa ni salama kwa biashara zake za kuumiza babu na bibi zetu, ni sawa na muuza viungo anaisifia bandari fulani ni salama kwasbabu hapati bugudha.
Ajabu kweliKatika uzi wake kuna maneno 11 ya kiarabu aliyoyatumia
Itabidi tuyaondoe nayo
Sultan Majjid alinunua kipande hicho cja kutoka Magogoni mpaka Aga Khan kutoka kwa famikia ya Tambaza tangu alivyoingia huko 1860s.
Sasa Mjerumani kajenga vipi Ikulu hapo wakati hilo jengo la Ikulu lilikuwapo kabla Mjerumani hajafika hapo?
Tunabadilisha kwa sababu zingine, siyo kuondoa memory ya utumwa au ukoloni...tunaweza kubadilisha.
..hata majina ya mitaa mbalimbali ya Dsm yalibadilishwa baada ya uhuru.
..barabara ya uhuru nadhani wakati wa Muingereza ilijulikana kama Accacia street/avenue.
Hii haimaanishi kwamba Wajerumani hawajajenga Ikulu kwenye kiwanja cha Sultani palipokuwa na majengo ya Sultani Majjid hapo Ikulu Dar.View attachment 3250910
View attachment 3250911
Germany Old Boma, Bagamoyo.
Makao makuu ya kwanza ya watawala wa Ujerumani hapa Tanganyika yaliyojengwa na Wajerumani. Iangalie hiyo design, same same na Magogoni.
Pia mimi sijabisha Wajerumani walijenga Ikulu yao katika ardhi ya Sultan Majjid/Mzee Tambaza/watu wa pwani ya Dar es Salaam(Wakoloni walichuka ardhi waliyoona inafaa popote Tanganyika kwa matumizi mbalimbali, hili haliwezi kuwa jambo la ajabu au la kipekee sana).Hii haimaanishi kwamba Wajerumani hawajajenga Ikulu kwenye kiwanja cha Sultani palipokuwa na majengo ya Sultani Majjid hapo Ikulu Dar.
Pia picha hizo hata hazithibitishi kwamba Wajerumani hawajaiga kujenga hivyo kitoka kwa Waarabu.
Hizo picha hazi prove lokote zaidi ya kusema Mjerumani alijenga majengo Bagamoyo.
Kitu ambacho hakijabishiwa hapa.
Na Beijing ambayo inawatu zaidi ya milioni 21 lakini imepangwa vizuri na inavutia sana.Au New York cityKule wapo wachache mji mzima hawazidi hata wakazi wa tandika utalinganisha na dar ambayo sawa na wananchi wote nchi nzima
Mkulu unaposema jina la dar..."tumelikubali" una maana ya Watanzania wote au ni kina nani hao ambao wamelikubali?Jina la Dar es salaam tulishalikubali, tulikichukua na kulifanya letu, si la Sultani tena.
Ukishikilia kuwa ni la Sultani, wewe ndiye unampa Sultani umuhimu asiokuwa nao.
Pia, kihistoria Dar es salaam kama mji ni mji ulioanzishwa na Sultani. Hiyo ni historia ambayo haifutiki hata ukibadili jina.
Hii ni sawa na kachumbari tu kwenye pilau, hakuna jambo kubwa sana hapa.
Sawa.Hii ni sawa na kachumbari tu kwenye pilau, hakuna jambo kubwa sana hapa.
Inawezekana Mjerumani alimpa tu tenda ya kutengeneza milango Mwarabu au Mswahili akajiongeza kuweka mambo yake na Mjerumani akaona ni urembo unaopendezea kwenye mlango.
Huu hapa mlango mmojawapo wa German Old Boma, Bagamoyo
View attachment 3250942
Hayo majengo yamejengwa kwenye ardhi aliyoinunua Sultan Majjid na yeye alikuwa kashajenga chuo cha kueneza Uislamu hapo.Pia mimi sijabisha Wajerumani walijenga Ikulu yao katika ardhi ya Sultan Majjid/Mzee Tambaza/watu wa pwani ya Dar es Salaam(Wakoloni walichuka ardhi waliyoona inafaa popote Tanganyika kwa matumizi mbalimbali, hili haliwezi kuwa jambo la ajabu au la kipekee sana).
Sijabisha pia labda kulikuwepo na majengo ya Sultan Majjid, sina uhakika na hilo, sijui yalikuwa ya aina gani kama yalikuwepi ila uhakika mkubwa ni kwamba majengo ya Ikulu ya sasa hayakuwa ya Sultan Majjid au Mzee Tambaza bali yalijengwa na Wajerumani.