Ee baba tuumbie moyo safi. Tuondolee mioyo ya tamaa na kupenda mali. Tulikuja uchi tuondoke uchi. Tutazikwa katika vipande vidogo sana vya ardhi. Tupe kupenda wengine zaidi. Tusaidie katika maisha yetu..kudumu katika kuutafuta uso wako. Kudumu katika sala na dua kila wakti. Mali zetu tamu ziwe Imani thabiti katika neno na mausia yako. Tuchape viboko pale roho zetu zinapoingiwa na tamaa ya mali, fedha etc.
Ni kheri tufike kwako tukiwa hatuna miguu, macho, mikono kuliko kuukosa ufalme wako. Tusaidie mali tutakazozichuma na wenza wetu zisiwe sababu ya kuondoa utu wetu. Tupe kudumu katika kusaidia yatima, wajane, wagonjwa na hata kwenda makaburini kusafisha kila mara. Hii itukumbushe duniani tunapita tu. Itukumbushe tunatakiwa tuache legacy ya wema tuliofanyia watu. Tukatajwe vizuri midomoni mwa watu. Maisha yetu yakaandikwe katika vibao vya mioyo ya watu kwa utu wema na fadhili tutakazokuwa tumefanya.
Zaidi tupe kukujua wewe na kuliishi neno lako. Milioni, Bilioni hazitatusaidia kitu kama hatuna uwepo wako na Neema yako. Ni kheri watoto wetu wale mihogo huku wakiwa watu wema na wauone wema na upole kwa mfano ndani yetu kama wazazi wao. Kila pepo la tamaa, chuki, ulafi wa mali, roho mbaya, fitna, kisasi, uchawi na ulozi..shindwa kwa jina la Yesu. Tunaomba na tunaamini...Amen.
NB: Kama utakwazika na hii comment naomba nisamehe. Niignore kabisa ikikubidi. Ubarikiwe