GeoMex
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 5,430
- 20,063
hii Reli ilitakiwa ifanyiwe replacement yote,kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,umri wake etc ni death trap kwa sasa.
Reli ina miaka mingapi?
Tuanzie hapo
Chanzo cha ajali sidhani kama itakuwa ni uchakavu wa miundo mbinu,ila itakuwa ni mvua kama inavyoonelana kwenye picha hapo juu tuta limeliwa na maji...
Imesharekebishwa na wachina tayari,wako katika kumalizia mpaka Isaka.
Ni kweli mkuu @ kuna mradi wa uboreshaji wa Reli ya kati(Metre Gauge) ulionza toka 2018 na anategemea kukamilika 2021 hii
Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ndio iliyopewa hiyo tenda ya Dola milion 300 na inatekelezwa katika vipande vinne ambayo ni Dar es Salaam- Ngerengere- Kilosa – Itigi hadi Isaka na mpaka mara ya mwisho nimefuatilia walikua wameshapita Dodoma wanaelekea Itigi huko kwahiyo nadhani eneo la Ajali lilishafanyiwa marekebisho(Upgrades)
Ukarabati wa reli hiyo unakwenda sambamba na Ujenzi wa madaraja, kuchomelea reli bila kuacha nafasi,uinuaji wa tuta la reli pia kujenga vituo vya kudumu vya kusimama trein pindi lifanyapo Safari zake.
Lengo la ukarabati huu haswa ilikua kuboresha reli iliyochakaa(ya zamani), kuiongezea uwezo wa kubeba mzigo mkubwa zaidi na pia kuifanya treni ihimili spidi kubwa zaidi
Heri ya Mwaka Mpya