Bajaji biashara kichaa Kuna jamaa kanunua juzi bajaji mpya Leo imepata ajali haitamaniki milion 10 zimeenda

Arsenal Gunner

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
10,891
Reaction score
17,718
Aisee, huku mtaani kuna jamaa alinunua bajaji juzi, akampa dereva ili ampelekee hesabu kila siku. Leo asubuhi bajaji imepata ajali mbaya sana—haitamaniki kabisa.

Imeharibika vibaya kiasi kwamba sasa ni ya kuuza kama chuma chakavu tu. Milioni kumi zimepotea kizembe sana.

Yule jamaa amechanganyikiwa kweli. Tangu asubuhi anaongea peke yake, hatulii hata tukijaribu kumbembeleza.

Na cha kusikitisha zaidi, taarifa ya hivi punde imesema yule dereva amefariki dunia hospitalini. Jamaa haamini kilichotokea—kabisa kama kapagawa.

Kweli kuna biashara nyingine si za kuingia tu kiholela. Hii ni funzo la maisha.
 
Mtulizeni akitulia mwambie ndio maisha ila ki uhalisia biashara ya vyombo vya moto kama huna msuli wa Imani usifanye maana matukio yake kama hayo huwa yanachoma moyo sana
Anyway sio biashara naweza kumshauri mtu heri Car wash kuliko bajaji
 
risk yake kubwa --- na waendesha vyombo barabarani kufata sheria ni mtihani sana achilia mbali kupata mafunzo yenyewe.

hivi bima za bajaji au pikipiki zipo vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…