Bajaji biashara kichaa Kuna jamaa kanunua juzi bajaji mpya Leo imepata ajali haitamaniki milion 10 zimeenda

Bajaji biashara kichaa Kuna jamaa kanunua juzi bajaji mpya Leo imepata ajali haitamaniki milion 10 zimeenda

A

Anawehuka tu akikumbuka hiyo bajaji alitegemea ingemtoa. Sasa hana bajaji hana 10m hana matumaini. Na hajui ataanzia wapi wakati ana familia
Mshaurini afanye ibada,pia ajichanganye na watu tofauti tofauti,atapata wazo jipya,nakutulia,,mi mwenyewe kuna rafiki yangu wa karibu sana nilimkopesha ten million,akaweka kwenye biashara ya duka,ikayeyuka yote,ye akashindwa kunielezea imekuwaje!!,akabaki tu kushangaa,haelewi ati hasara imetokeaje,nikaishia tu kusamehe japo moyoni kuna uma.
Lkn nilipoenda kijiwe kimoja DSM,rafiki yangu mmoja akawa anasimulia duka lake la vipodozi lenye thamani ya mil 60,,wezi waliingia wakakomba kila kitu, anasema alikonda kama miezi miwili kwa mawazo,lkn baadae alipata ushauri akawa fiti,mi niivomsikia nikajisikia nafuu sana na mawazo kwangu yalikata haraka sana.,sikuamini.
 
Kila biashara ina risk zake.
Hata mwanamke anabeba mimba miezi 9 anaenda leba na mtoto anakufa.
Ndio maisha yalivyo.
 
Sasa ye ye analilia bajaji wakati uhai wa mtu umeenda kipi kina thamani apo
 
Yaani huwa naona ni over price. Sioni sababu ya bajaji kuuzwa hio bei.
IMG-20250504-WA0064.jpg
 
Yaani bajaji inamuuma kuliko dereva aliyetajwa kufariki huyo dish limeyum a
 
Aisee, huku mtaani kuna jamaa alinunua bajaji juzi, akampa dereva ili ampelekee hesabu kila siku. Leo asubuhi bajaji imepata ajali mbaya sana—haitamaniki kabisa.

Imeharibika vibaya kiasi kwamba sasa ni ya kuuza kama chuma chakavu tu. Milioni kumi zimepotea kizembe sana.

Yule jamaa amechanganyikiwa kweli. Tangu asubuhi anaongea peke yake, hatulii hata tukijaribu kumbembeleza.

Na cha kusikitisha zaidi, taarifa ya hivi punde imesema yule dereva amefariki dunia hospitalini. Jamaa haamini kilichotokea—kabisa kama kapagawa.

Kweli kuna biashara nyingine si za kuingia tu kiholela. Hii ni funzo la maisha.
Bima zipo hamtaki kukata
Majanga yakitokea shida huanza apo.
 
Bima zipo hamtaki kukata
Majanga yakitokea shida huanza apo.
Bima wenyewe hawaziamini boda na bajaj.

Ukizipa bima kubwa uwezekano wa kupata majanga kwa vyombo hivyo ni mkubwa.
 
Uvivu wenu huo, unanua chombo unampa mtu na wewe huna kazi ya maana unasubiri uletewe mrejesho

Halafu 10m imeenda Bajaj haina Insurance au zote ndio hivyo huwa hazikatiwi?

Sasa jamaa kakosa Bajaj na mtu kafa daa

Hii sio biashara sasa
 
Aisee, huku mtaani kuna jamaa alinunua bajaji juzi, akampa dereva ili ampelekee hesabu kila siku. Leo asubuhi bajaji imepata ajali mbaya sana—haitamaniki kabisa.

Imeharibika vibaya kiasi kwamba sasa ni ya kuuza kama chuma chakavu tu. Milioni kumi zimepotea kizembe sana.

Yule jamaa amechanganyikiwa kweli. Tangu asubuhi anaongea peke yake, hatulii hata tukijaribu kumbembeleza.

Na cha kusikitisha zaidi, taarifa ya hivi punde imesema yule dereva amefariki dunia hospitalini. Jamaa haamini kilichotokea—kabisa kama kapagawa.

Kweli kuna biashara nyingine si za kuingia tu kiholela. Hii ni funzo la maisha.
Kwa mtazamo huu, kila biashara ni kichaa..!!
 
Elimu elimu
Screenshot_20250506_201703_WPS Office.jpg


Whatsapp: 0687746471

Hiki kitabu akinunue aanze kusoma taratibu. Biashara sio Millioni kumi biashara ni wazo.
 
Hizo milioni kumi angenunua viwanja na kujenga fremu za kupangisha zisingepotea kizembe hivyo
Huwa nashangaa sana.... Kuna maeneo kila kona ni mafremu.... Hakuna mzunguko wa watu kihivyoooo.... Mnawazaga nini kuwa fremu hizo zitakulipa kwa mzunguko upi wa biashara kwa watakaopangisha?? Au hayo huwa hayakuhusu mwenye fremu??
 
Back
Top Bottom