Bajeti 2020/21 Watumishi wa Umma mwaka wa 5 hakuna nyongeza ya mishahara wala punguzo la kodi

Bajeti 2020/21 Watumishi wa Umma mwaka wa 5 hakuna nyongeza ya mishahara wala punguzo la kodi

Inafikia hatua mtu unachoka na haya malalamiko mitandaoni. Mnashindwa nini kuwaiga USA?
Wewe umewaiga ?

Umewaigia wapi ?

Uwepo hapa hapa bongo ndo uwaige tujue kweli wewe umewaiga [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unaoneka wewe si mfatiliaji mzuri wa mambo.

Hujasikia juzi Wakufunzi wa Chuo kimoja wamekamatwa kwa kuhujumu uchumi, wakati kosa ni kufanya kazi chuo zaidi ya kimoja ili kukuza vipato vyao.

Yani Madaktari wasiwe na dispensaries zao, fundi umeme usifanye part time, na IT usiguse kazi ya mtu..

Alafu unaleta story za kipato cha ziada .

Nyie ndo wale Leo niko masikini huulizi nimepataje umasikini, lakini kesho nikiamka tajiri unakuja kunikamata na kuhoji nimetoa pesa wapi.
Mkuu unaelewa lakini maana ya kufanya kazi za ziada na mkataba wako wa ajira?

Sasa iko hivi Kuna masaa ambayo inabidi ufanye kazi kwa mwajiri wako (hapa nazungumzia serikali ) baada ya masaa hayo ya kazi yako uliyoajiriwa na serikali kuisha unaruhusiwa kwenda kufanya kazi sehumu nyingine au Kama una kibiashara chako nenda kafanye.

Sasa tatizo kwa hao unaosema wanafanya part time huko rucu ni kwamba walikua wakiiba muda wa mwajiri wao wa permanent (gorvenment ) hapo ndipo kosa lao linapo patikana.

hata Kama wanafanya kazi masaa kadhaa tu then wanaenda kwenye kazi zingine bila kumaliza masaa ya siku (masaa 9:30 Hadi 12:00 kulingana na nature ya kazi ) Bado wanakua wameiba muda
 
Mkapa hakuongeza mshahara lakini maisha ya wafanyakazi yalikuwaje, dawa si kuongeza mshahara bali ni kudhibiti mfumko wa bei leo hii mshahara ukiongezwa kila kitu kitapanda bei kuanzia daladala, kodi ya nyumba , chakula na vinginevyo inachotakiwa kufanya serikali ni kupunguza mfumko wa bei
Yes........sisi tunataka kila mwaka iongezwe 100,000 wakati mtaani nako vitu vinapanda kwa wastan wa 100000 tena.....faida iko wapi?
 
Hilo punguzo la kodi kwa wafanyakazi, toka mshahara wa shilingi 170,000 hadi 270,00 hujalisikia?
Hongera. Mnaolipwa laki 2 mmenufaika sana. Mazombie hata yakijambiwa yanaomba yaharishiwe....

Hiyo punguzo nadhani itapunguza usumbufu kwa shemeji yako. Maana kumhudumia mke na mdogo wake sio jambo dogo
 
Mtu hataishi kwa mkate tuu, hivyo pamoja na kutoongezwa mishahara, lakini msiwe na hasira bali hapo tarehe 25 October,
unachukua...,
unaweka ...
Waaah...
P
Blaza... ushaambiwa AtakeAsitake....

Sentensi pana sana hiyo...

Twenzetu Bujumbura msibani...
 
Na wanaweka vifungu vya kikatiba vya kuwalinda wasishitakiwe hata kama wameikanyaga hiyo Katiba,pathetic
 
Mkapa hakuongeza mshahara lakini maisha ya wafanyakazi yalikuwaje, dawa si kuongeza mshahara bali ni kudhibiti mfumko wa bei leo hii mshahara ukiongezwa kila kitu kitapanda bei kuanzia daladala, kodi ya nyumba , chakula na vinginevyo inachotakiwa kufanya serikali ni kupunguza mfumko wa bei
Natumai una akili nzuri tu,Ila hautaki kuzitumia...
Mfumuko wa bei ulishashindikana kuudhibiti,tazama sukari,ilitoka 1800/kg kwa sasa inaogelea 3000-3500

Mafuta ya kula yamepanda pia,mazao ya chakula tumeambiwa tuuziwe kwa bei ya juu sanaaa!

Kubwa kuliko yote,ni kwamba kwa kuacha mishahara ya watumishi kwenye mkwamo namna hii ina maana hata mafao ya kustaafu yanaathirika,hawa watumishi watakuja kujikuta wanachukua pesa kiduchu sana kwa sababu ya mkwamo wa nyongeza za mishahara!

Wakati huo huo,jaribio la kipuuzi la "kumtunzia" mfanyakazi pesa zake baada ya kustaafu ni kikwazo kingine kilicho hapo mbele!

Yaani mtumishi wa umma anafanya kazi kwa miaka 30+ anapaswa kupata milioni 100,then anapewa 25 kwanza,(wakati huo huo hicho kiasi kipo "stagnant" kutokana na kutopandishiwa mishahara yao!

Kwa hali hii,watumishi wa umma wanaendelea kuandaliwa kuwa masikini watakaoshindwa kumudu maisha yao wakati ambao hata nguvu za kutafuta hawatakuwa nazo!
 
TEETH na PEACE THIBI wanaongezewa Mishahara kila Mwaka , Watumishi wengine MABUMUNDA wataendelea Kupiga Miayo!!
 
Fanyeni kazi mbadala muache kulilia nyongeza,Mimi kamshahara kangu ni kadogo sana,nikikata kila mtu atacheka but sitakaa niililie government yetu iti kwanini hakuna nyongeza

Mishahara hata kwa wafanyakazi wa nchi za ulimwengu wa kwanza haijawahi kutoshereza ije kuwa Tanzania?

Piga kazi mbadala na hiyo uliyoajiliwa nayo.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Buku 7 kwa siku ndiyo kazi mbadala inayokufanya usitake nyongeza ya mshahara?
 
Umeshukaje? Sukari tunanunua 3300, maharage 2400, sembe elfu moja na pointi....unasema Nini?
Mishahara ya nini kama mfumuko wa bei imeshuka na umekua stable? Nyongeza ya mshahara ina faida gani kwenye mazingira ya mfumuko wa bei?
 
Watumishi mnalialia sana kama mishahara haiwatoshi acheni kazi mfanye issues zingine . Kutwa kucha kulialia mishahara lakini bado mpo tu kazin
 
Kwa akili yako ni punguzo la kodi ipi?
Sasa ni matako yako hayo? Yaani nyie ndio mnatufanya wapinzani tuonekane manyumbu! Maanake mtu aliyekuwa anapata 2.24m hatakatwa kodi, kodi inaanza kwa mtu anayepata 3.24m kwa mwaka.

Sasa mimi kwa mshahara wangu nimepiga hesabu nikakuta kuna punguzo la elfu 50 kwa mwezi, utasemaje hakuna punguzo hapo? Mnyonge mnyongeni......! Sema Magu amezingua kutowaongezea mshahara tu hao watu wake, ila yote hiyo ni kiburi cha huyo mzee!
 
Mtu hataishi kwa mkate tuu, hivyo pamoja na kutoongezwa mishahara, lakini msiwe na hasira bali hapo tarehe 25 October,
unachukua...,
unaweka ...
Waaah...
P
Tangu unyimwe ulaji na Serikali umekuwa na stress sana... Umekuwa na maisha magumu na kiofisi chako Cha chumba kimoja hapo kwenye la Africasana Kama mama ntilie.

Kama ulishindwa kuendelea kipindi Kile unapata matender ya milion 100+ usidhan utazipata Tena Sasa hivi kwa kujipendekeza.
 
Unaoneka wewe si mfatiliaji mzuri wa mambo.

Hujasikia juzi Wakufunzi wa Chuo kimoja wamekamatwa kwa kuhujumu uchumi, wakati kosa ni kufanya kazi chuo zaidi ya kimoja ili kukuza vipato vyao.

Yani Madaktari wasiwe na dispensaries zao, fundi umeme usifanye part time, na IT usiguse kazi ya mtu..

Alafu unaleta story za kipato cha ziada .

Nyie ndo wale Leo niko masikini huulizi nimepataje umasikini, lakini kesho nikiamka tajiri unakuja kunikamata na kuhoji nimetoa pesa wapi.
kweli
 
Kumbe mfumuko wa bei huwa unasababishwa na nyongeza ya mishahara ?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo ni nini haswa!!
Mkapa hakuongeza mshahara lakini maisha ya wafanyakazi yalikuwaje, dawa si kuongeza mshahara bali ni kudhibiti mfumko wa bei leo hii mshahara ukiongezwa kila kitu kitapanda bei kuanzia daladala, kodi ya nyumba , chakula na vinginevyo inachotakiwa kufanya serikali ni kupunguza mfumko wa bei
 
October 25 ndiyo jibu, kama wafanyakazi waendelee kukosa nyongeza ya mshahara kwa miaka mingine 5, kama watumishi wa umma waendelee kutukanwa kwenye majukwaa!
 
Huo ndio ukweli kabisa, hii awamu wanachomuandalia mtumishi ni hahaha magumu tu hakuna kingine na iko wazi, kusimama kwa nyongeza mshahara madhara yake watayaona wakati as kustafu
 
Back
Top Bottom