Bajeti 2021/22: Wadau tunakataa kodi ya Majengo kulipwa kwa LUKU

Mtakuwa mnakatana wakati wa kulipa kodi ya nyumba,ni rahisi sana yaani rahisi sana, kodi kwa mwezi 40,000 kwa miezi 6 = 240,000 toa kodi ya nyumba ya kipindi hicho 5000 unampa zake 235,000 mnaachana kiroho safi mnakwama wapi ndugu zangu?
Hayo yooote ya kazi gani ?
 
Huu Ni utaratibu mzuri wa kukusanya Kodi, watakuwa wamepanua wigo mpana zaidi,
Kwa wale ambao hawatumii umeme au wanatumia nishati mdadala watatafutiwa utaratibu wao wa kulipa hiyo kodi
 
Kwa hiyo kama wapangaji wana luku zao nao watakuwa wanakatwa kodi ya jengo? au pale mmiliki hakai kwenye jengo lake ina maana wapangaji ndo watakuwa wanamlipia kodi ya jengo kupitia malipo yao ya LUKU, ama?
 
Ndio uwezo wa MWIGULU ni wakufikilika
 
Nadhani Mwigulu anaamini kila Mtanzania anaishi kwenye nyumba yake kutokana na porojo za uchumi wa kati

Waziri ameamua wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma wanaoishi nyumba za serikali au mashirika ya umma WALIPE kodi ya majengo kwa kupitia LUKU!!!!!! na kama haitoshi wapangaji ni lazima(mandatory) kulipa kodi ya majengo kupitia LUKU!!! Is this normal or rather is it truly justifiable??? Wachumi katika wizara ya fedha wapo likizo au ndiyo njia fupi ya kufanya serikali ya awamu ya sita ilaumiwe au maandamano yaanze kwa wazee wastaafu au ambao umri ni zaidi ya miaka 60 na wako kwenye nyumba zao walipe kodi against sheria iliyopo?? wapo exempted from taxation!!!
 
Mbona kodi yenyewe ni ndogo sana...Buku tu kwa mwezi or elfu 12 kwa mwaka hii nayo tutoe mishipa kuijadili humu?
Km nyumba ina wapangaji wa 5 hio ni 200 kwa mpangaji, hii kweli nalo la kujadili kweli...mpangaji analipa kodi ya 50k-150k anashindwaje kuchangia 200 km kodi ya Jengo.
Kuna watu tunakatwa 30% PAYE na kuna watu wanakatwa 8% na kuna watu hawakatwi kabisa, hili ndo tuliongelee ila sio issue ndogo ndogo km hizi unless tumekosa kazi za kufanya.
Na km tuna taka ku protest kuhusu hii kodi then tuanze na ushuru wa magari ulioingizwa kwenye mafuta unaowafanya ht wasio na magari waulipie, mtu unanunua petrol ya jenereta unalipia na ushuru wa magari.

Watanzania tupende kulipa kodi...kuna mchangiaji hapo juu kazungumzia kushuka kwa gharama za kuunganishiwa umeme kutoka 300k mpaka 27k, haya ni mapato yamepungua ila hamlalamiki, ila buku tu kwa mwezi tunatoka mapovu...tunataka maendeleo ila hatutaki kuyachangia, then serikali ikikopa kufidia nakisi napo tunalalamika deni la taifa...kila kitu kwetu ni lawama, hatuna jema.
 
Wameshindwa kubuni vyanzo vipya waondoke kwani lazima waongoze wao?
 
Wameshindwa kubuni vyanzo vipya waondoke kwani lazima waongoze wao?
Hapo hawajabuni chazo kipya, kodi ni ile ile kilichobadilika ni namna ya ukusanyaji...sasa wewe unaepinga tupe alternatives, ni nyia ipi rahisi ya kukusanya kodi ya jenho in an efficiency and effective way...
Kwa wanatanzania mnavyopenda kulalamika ht wangebuni lazima mngelalamika tu....kifupi hamna jema
 
Kwani hao wapangaji si wanaishi kwenye nyumba walipe t tena wao ndo vipele sana kwenye kampeni kuliko wenye nyumba.lipeni Kodi ya jengo langu ninywe bia kwa bei nafuu.πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Hapo hawajabuni chazo kipya, kodi ni ile ile kilichobadilika ni namna ya ukusanyaji...sasa wewe unaepinga tupe alternatives, ni nyia ipi rahisi ya kukusanya kodi ya jenho in an efficiency and effective way...
Kuna tofauti kati ya kukata kodi juu kwa juu na kukukusanya

Kwakifu hawa watu sina imani nao
 
Wewe unapendekeza vipi!? Toa na solutions sio kukosoa tu
 
Kila mtu anayetumia umeme siyo mbaya akalipa kodi? Nchi hii itajengwa na walipa kodi, ukiusifia mradi wa umeme vijijini REA kisha ukapinga kodi kwenye luku basi utakuwa na shida kichwani kwani mrado ule ulitumia pesa nyingi za mkopo na bado unaendelea kufyonza bajeti
 
Una akili sana wewe, meko na task force ni ushetani na kukosekana ubunifu, kodi ilihitajika lakini siyo unyang'anyi
 
Mitazamo

1. Inaonekana utaratibu wa kulipa Kodi ya Majengo utamgharimu zaidi Mpangaji, na itakuwa nafuu kwa Mwenye Nyumba.

2. Hata hivyo inategemea na utaratibu wa nyumba husika:
- Kuna nyumba Mwenye Nyumba anakusanya kiasi chote cha umeme kutoka kwa wapangaji kila mwanzoni mwa mwezi.
... hapa wapangaji wakiwa wafuatiliaji (kweli kweli) watakubaliana na Mwenye Nyumba aongeze/achangie na kiasi cha Kodi ya Majengo pale anapokusanya pesa ya umeme ili kiasi cha umeme kisiathiriwe na Kodi ya Majengo.

3. Kuna nyumba wapangaji hulipia umeme kwa zamu (pale unapoisha).
... hapa inaonekana kutakuwa na changamoto kubwa.
... Itabidi tu kuwe na makubaliano na Mwenye Nyumba.

4. Mfumo wa kulipia Kodi ya Majengo kwa LUKU hautaweza kuwa "one-size-fits-all" kwa sababu uraiani mambo yanatofautiana.

...Kama ilivyo kwa mabadiliko yoyote, itachukua muda kidogo kuendana na huo mfumo mpya.

5. Ninaamini kutakuwa na 'mechanism' au mwongozo wa kutekeleza pendekezo hilo, tuwe na subira.

Ahsante
 
Kwani mpangaji akilipa kodi ya jengo iko mbaya gani? Hii ni njia efficient sana ya kukusanya kodi - you collect at source
Wapangaji ongeeni na landlords wenu wapunguze rent. Mwigulu komaa hapo hapo.
Kwamba imepitishwa sidhani , maana ni lazima ijadiliwe bungeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…