Bajeti 2021/22: Wadau tunakataa kodi ya Majengo kulipwa kwa LUKU

Bajeti 2021/22: Wadau tunakataa kodi ya Majengo kulipwa kwa LUKU

Tuondoe posho zote tunazowalipia viongozi wanunue umeme chakula vinywaji nguo zao na usafiri wajitegemee wawaondolee wananchi mzigo wa kuwatunza na kuwajengea mahekalu. Waishi maisha ya mfanyakazi ambaye anategemea mshahara wake, wanapoomba wanasema wanataka kututumikia wakipata sisi ndio tunawatumikia!!!!
Posho haziwwzi ondolewa kamwe labda kupunguzwa.

Pia wakome kununua magari ya kifahari na bei kubwa kwa ajili ya oparesheni za serikali

Hii tabia iliyozuka ya viongozi kushindana na wafanyabiashara na wasanii ni upumbavu at our expenses
 
Vipi kuhusu wale wanaoishi nyumba za serikali kama polisi, wanajeshi, Marc, Ras, mawaziri na makatibu wakuu wa wizara watakuwa wanalipia Kodi ya nyumba za serikali kupitia luku? Au Sheria hiyo imewabaguaje? Je, mashule, hospitali na ofisi za umma zinazonunua umeme wa luku nao watachangia Kodi za majengo ya umma wanunuapo luku?
Aliyelielewa hili anifafanulie tafadhali kwani sijabahatika kuisikia hotuba!
Mkuu,Hio ni kodi ya kichwa.Relax uendelee kuilipa
 
... siku zote mlipa kodi ni mlaji wa mwisho! Mwenye nyumba mzigo wa kodi mwisho wa siku ataushusha kwa wapangaji tu! Kwangu, hili la kulipia kodi ya pango kupitia Luku angalau lina ubunifu badala ya kuweka "task force" zikimbizane na wenye nyumba vichochoroni angalau automatically watu watalipa kodi za majengo.
Amiin
 
Kitendo cha Waziri wa Fedha kupendekeza kodi ya majengo ikatwe kwenye manunuzi ya umeme kinapaswa kufafanuliwa vizuri ili wananchi waelewe vizuri.

Hii ni kwa sababu nyumba nyingi zina wapangaji na ambao ndio walipaji wa bili ya umeme kwa vile wao ndio wanaoutumia, ziko nyumba ambazo wenye nyumba hawamo kabisa, wanaokaa humo ni wapangaji tu, wanawezaje kulipishwa kodi ya jengo kupitia ununuzi wa umeme huku wakiwa si wenye nyumba?

Hata kama hela hiyo itakatwa kidogo kwa mtindo wa kudunduliza, lakini haipaswi kulipwa na wapangaji .

Hili lifafanuliwe au lifutwe tuweke utaratibu mwingine utakaowalipisha kodi ya majengo wahusika tu.
Naafikiana naye sana and amefanya akili hapa. Itabidi mwenye nyumba apunguze kodi kufidia hilo
 
Kwa minajili ya Serikali kukusanya mapato basi utaratibu mpya utakua bora zaidi kuliko Sasa. Kama swala ni nani alipe kodi kati ya mpangaji na mwenye nyumba basi urahisi ni kua tu siku mpangaji akilipa kodi ya pango kwa mwenyenyumba akate hela yake ya Luku.

Alternatively Mwenye Nyumba anaweza kununua luku ya hiyo 12,000/- ikawa ndio kodi yake ya ardhi/kiwwnja amelipa hapo Kisha kipindi kinachofuata watalipia wapangaji wenyewe.

Ilivyo sasa nyumba nyingi hazilipi hii kodi, hivyo kupitia luku basi nyingi zitalipa
Hivi kwa akili yako ukijenga nyumba na kupanga nyumba nani mmiliki hapo?

Unalipa huduma unayopata iwe umepata kwa kujenga,kukodi au kupanga.

Yaani mwenye nyumba aje kukulipia wewe kodi ya jengo eti Kisa mpangaji? Yeye ndio anaishi kwenye jengo?

Kila mtu alipe kodi na Serikali pia itambue vipande vyote vya ardhi Ili wamiliki walipe kodi ya ardhi
 
nina nyumba 5 , 2 Kyela , 3 Dsm , kati ya hizo 1 ya Kyela na 1 ya Tandika naishi mwenyewe , sasa hizi 3 kwanini wapangaji wangu wakatwe kodi ya jengo ?
Kama umeliona hilo, c uweke utaratibu wako Wa kuwarushia hiyo pesa watakayokua wanalipa kwenye jengo lako,
Tena ni rahisi tu , kila mwaka unakua unawanunulia wapangaji wako umeme Wa elfu kumi tu unakua umemaliza ,
Tusipende kulalamika kila kitu, Nchi ni yetu sote na tutakaoijeanga ni sisi wenyewe hakuna mwingine
 
Tuondoe posho zote tunazowalipia viongozi wanunue umeme chakula vinywaji nguo zao na usafiri wajitegemee wawaondolee wananchi mzigo wa kuwatunza na kuwajengea mahekalu. Waishi maisha ya mfanyakazi ambaye anategemea mshahara wake, wanapoomba wanasema wanataka kututumikia wakipata sisi ndio tunawatumikia!!!!
Hawa jamaa ni wezi hata ufanyeje mtu kama anaweza kuiba kura mchana kweupe atashindwa kuiba kodi?
 
Hiyo siyo kodi ya majengo bali ni kodi ya mita za umeme kwa jina la kodi ya majengo.
 
Kama umeliona hilo, c uweke utaratibu wako Wa kuwarushia hiyo pesa watakayokua wanalipa kwenye jengo lako,
Tena ni rahisi tu , kila mwaka unakua unawanunulia wapangaji wako umeme Wa elfu kumi tu unakua umemaliza ,
Tusipende kulalamika kila kitu, Nchi ni yetu sote na tutakaoijeanga ni sisi wenyewe hakuna mwingine
Nani kakwambia analalamika. acha watu wawe wazi kutoa mawazo yao tofauti ili kufanyike maboresho mazuri zaidi.na ndo maana hata baheti yenyewe inajadiliwaga bungeni ili kama kuna maboresho yafanyike.
 
Hiyo siyo kodi ya majengo bali ni kodi ya mita za umeme kwa jina la kodi ya majengo.
Hayo ni maelezo yako , mbona road license ilihamishiwa kwenye mafuta na maisha yanaenda tena hakuna usumbufu wowote hakuna mambo ya kusumbuana tena, hata hii imekaa poa hakuna tena mambo ya kusumbuana na wenye Nyumba Kama ilivyokua zamani
 
Hivi kwa akili yako ukijenga nyumba na kupanga nyumba nani mmiliki hapo?

Unalipa huduma unayopata iwe umepata kwa kujenga,kukodi au kupanga.

Yaani mwenye nyumba aje kukulipia wewe kodi ya jengo eti Kisa mpangaji? Yeye ndio anaishi kwenye jengo?

Kila mtu alipe kodi na Serikali pia itambue vipande vyote vya ardhi Ili wamiliki walipe kodi ya ardhi
Acha ujinga wewe.kodi ya majengo anatakiwa kulipa mmiliki wa jengo nasio vinginevyo.Kama ambavyo wamiliki wa magari ya abiria walivyokua wanalipa kodi ya magari yao nasio abiria ndivyo hivyo hivyo kwenye majengo inavyotakiwa kua.Ata mshahara wewe mmiliki wa mshahara ndiye unayelipa kodi nasio watumiaji wa mshahara wako.Ata kwenye biashara wewe mfanya biashara ndiye unayetakiwa utoe sehemu ya mapato yako kulipa kodi nasio wateja wako.Kwa hicho ulichokiandika hapo kama kodi ya jengo anatakiwa kulipa mpangaji je huyu mmiliki wa jengo yeye atakua kalipa kodi wapi?.Hii kodi imewekwa kisanii kwanza kwa serikali kurahisisha ukusanyaji wa fedha toka kwa watu lakini pia serikali kuongeza uwanja mpana wakukusanya sent ndogo ndogo toka kwa kila mita ya umeme au kwa kila mtu katika vitu ambavyo watu wanamatumizi navyo kila siku lakini hii ya luku kamwe haiwezi kua ni kodi ya majengo bali kodi ya mita za umeme kwajina jingine fichiki.
 
Mjinga ni wewe,usilete mfano irrelevant na usiwe mpuuzi,,hata hizo kodi za biashara unadhani anaelipa ni mwenye biashara au yeye ni daraja?

Hujui hata dhana ya tax unaropoka tuu,kwa akili yako mbovu unadhani kodi ya mafuta analipa mwenye gari tuu au mtumiaji kwa njia ya nauli?

Ndo nakueleza leo huyo unaemwita mwenye nyumba eti atalipa nini kwani anaishi mbingini? Hatumii umeme?

Nasema hivi na ujue kuanzia leo hiyo ni kodi kwa kila mkaaji awe mmiliki au mpangaji,unalipia huduma ya jengo unaloishi whether umepanga au umejenga.

Na ndio maana ukipanga unakuwa sehemu ya mmiliki wa hiyo nyumba kwa muda na kulingana na pesa uliyolipa.Lipa kodi hakuna kichaka cha kupanga utakwepa hakipo.

Narudia tena kushauri serikali kupitia wenyeviti wa mitaa wabainishe kila kipande cha ardhi Ili kilipiwe kodi ya ardhi na kudhibiti kuhodhi ardhi na kutoiendeleza,huko kuna pesa nyingi Sana.
 
Hivi kwa akili yako ukijenga nyumba na kupanga nyumba nani mmiliki hapo?

Unalipa huduma unayopata iwe umepata kwa kujenga,kukodi au kupanga.

Yaani mwenye nyumba aje kukulipia wewe kodi ya jengo eti Kisa mpangaji? Yeye ndio anaishi kwenye jengo?

Kila mtu alipe kodi na Serikali pia itambue vipande vyote vya ardhi Ili wamiliki walipe kodi ya ardhi
Whatever utakavyowaza, kodi ya jengo inalipwa na Mmiliki wa Jengo, sio anaeishi. Taarifa za nani anaitumia hiyo nyumba kwa wakati husika sio kipaumbele cha Serikali, bali nani ni miliki.

Na usipolipa kama kuna any penalty hasara itakua kwa mmiliki. Swala sio nani anaishi kwenye Nyumba. Ilivyo ni kua hata Hiyoi Nyumba ukiamua uweke Mifugo iishi humo still mwenye nyumba unatakiwa uilipie. Njia pekee ya wewe kutoilipa hiyo kodi ni kuiuza hiyo nyumba ili isiwe ya kwako.
 
Back
Top Bottom