Bajeti moja ya barabara ya Rais Samia inaweza kujenga mara mbili ya barabara zote za lami zilizojengwa kwa miaka mitano iliyopita

Wataona very soon
 
Tena bajeti ya mwaka ujao ndio mtashangaa zaidi maana Jumuia ya kimataifa inamuamini mama na confidence kwenye biashara kwa sasa ni kubwa ,pesa inamiminika kama yote..

Mama atafanya wonders Sana.

👇🏿👇🏿👇🏿

Miezi sita ya Rais Samia,

Nchi imetulia tuli,
Wawekezaji kama wote
Wahisani kama wote
Wananchi Shangwe kila kona

#KAZIIENDELEE
 
Hiyo bajeti unaweza shangaa inaishia kujenga km100 Tu zingine Hao Hao kina Samai Na kiwete wanapiga
 
Rais Samia ameongeza wanafunzi 29,000 kwenye mikopo ya elimu ya juu HESLB kwa miezi sita tu,

miaka mitano mfululizo iliyopita tulifanikiwa wanafunzi wapya 32,000

Unaisemaje kasi ya Rais Samia?
#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

Kutoka Mwaka 2015/16 hadi 2020/21 pesa iliyoongezwa bodi ya mikopo ilikuwa Tshs 101BL na wanafunzi wapya walikuwa elfu 32 ,

Awamu ya sita kwa miezi sita pesa iliyoongezwa kwenye bodi hiyohiyo ni Tsh 120b na wanafunzi wapya ni elfu 29

Budget ya HESLB kwa mwaka 2015/16 ilikuwa 348.7B kwa wanafunzi 98,300

Budget ya HESLB mwaka 2020/21 ilifikia 450B kwa wanafunzi 130,883

_________________________

Awamu ya sita kwa miezi sita imeongeza budget kutoka 450B za awali hadi 570B za sasa na idadi ya wanufaika imeongezeka na kufikia 160,000.

#Hoja hapa ni muda wa matokeo

#HAKUNA KAMA SAMIA
 
Hongera zaidi mama Samia Suluhu
 
Haya mambo ndio yanifanya nimpende sana Mama Samia,

Hongera Sana mama yetu
 

Hivi wewe, unalipwa kumsaidia Samia au kumuharibia.

Hauwezi kupongeza mambo anayofanya Samia bila kumponda Magufuli.

Propaganda zako/ zenu na wenzako tangu 17/3/21 (ID zenu nyie wote) ni za kitoto sana. Hazimsaidia Samia na serikali yake. You guys need to learn the art public relations, be more sophisticated, more polished, muwe kwenye uhalisia zaidi.

Samia atasimama, ataheshimiwa kwa kazi zake. Sio porojo.

Sio vigumu kupendwa na kukubalika, tengeneza ajira kwa vijana, fanya kilimo kiwe attractive, ondoa kodi za ajabu, vikwazo, urasimu, rushwa.

Waweke watu kwenye nafasi kujali vigezo, taaluma, maadili. Usijali dini, ukabila, wametokea eneo gani, itikadi yao.

Kazi yake itaonekana.

Mnataka Madaraka, ila mnapoteza ushawishi kwa kuwafungulia kesi wapinzani kama kesi ya mbowe, kukandia nakuponda kila wa kitu kilichofanywa na Magufuli, kuweka wakulima na Watanzania kodi zisizo rafiki, vijana kukosa ajira, kutumbua wachapa kazi.

Mnasema kazì iendelee, kazi gani?ni hiyo hiyo mnayoiponda kila siku?

Vizuri mje na slogan mpya kwa kusema kila kitu cha Magu kilikuwa cha kishenzi, sasa ni tunarekebisha nchi na kupindua vyote alivyofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…