Bajeti yapendekeza Elimu ya kidato cha tano na sita kutolewa bure


Unataka Nini ndugu yangu mbona malalamiko?. Yani mtoto anasoma form 5 na 6 bure bado unalalamika. Shukuru hata kwa kidogo ulichopewa. Mambo ya chuo kikuu ipo siku mtasoma bure.
 
Tatizo kubwa liko vyuo vikuu aiseee,yani mtu ada millioni na laki 7 unapata asilimia 40 unaongeza mwenyewe 1millioni na laki 3 aiseee unaishi maisha magumu sana ,bora hata huku chini .mtu ajilipie ila chuo apewe mkopo asilimia zote .maana kuna wengine vyuo wanashindwa kabisa yaani.lakini pia ni maneno ya kisiasa.
 
Asante Raisi kujali maskini watoto wa viongozi wa bunge,mahakama na Serikali wakiwemo wa mawaziri Raisi, makamu nk hawasomi hizo shule za bure wanasoma private

Something is better than nothing
Kama Serikali iko serious ibadili mitaala yote ya shule za msingi kuwa English medium
Haina maana kukomaa kuwa kiswahili Lugha ya kufundishia wakati hadi advocates wa kudai kiswahili kiwe Lugha ya kufundishia watoto wao wanasomesha English medium kuanzia wabunge,viongozi wa mahakama na Serikali
 
"Napendekeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Kuanzisha utaratibu wa kutoza ada ya shilingi 1,000 hadi 3,000 kwenye ada ya matumizi ya king’amuzi kulingana na kiwango cha matumizi" -
@mwigulunchemba1 Waziri wa Fedha na Mipango.

Chanzo: Dar Mpya Blog

Mkimaliza Kushangilia la Kidato cha 5 na 6 kufutiwa Ada zao rudini sasa mshangilie ha hili kwani nalo ni zuri kabisa tu.
 
Yaani unashangilia Ada ya Kidato cha 5 na 6 Kutolewa wakati Kwingineko Umebanwa na Unakamuliwa vilivyo? Watanzania sijui ni nani ameturoga / amewarogeni hakyanani.
Hujanielewa ndugu.
Hapo nimelaani kuwekwa kwa tozo mpya kwenye ving'amuzi, huku nikiunga mkono kuondolewa ada kidato cha 5 & 6 .
 
Mwigulu alipuliza, then akang'ata halafu akakata sikio kabisa.

Futa ada za A level, weka tozo ya king'amuzi then malizia na kodi ya kichwa..
 
Huyu lameku ni daktari ama mganga?
PhD's ( Doctorates ) nilizokuwa nikiziheshimu kwa Watanzania ni zile za kutokea Uhuru wa Tanzania mpaka mwaka 2000 ila za kuanzia mwaka 2001 hadi leo wa 2022 si tu kuwa siziamini lakini pia huwa nawadharau mno wale Wote wenye nazo kwakuwa kama Mimi mwenye 'tudigrii' twangu tu hutu twa SAUT ( kwa mwaka 2009 ) nawazidi katika kuwa Logical kwa Masuala mbalimbali Faida ya wap kuwa nazo ni nini au ipi?
 
Jamaa wanachofanya ni kuhamisha Magoli tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…