Bakhresa ameshinda tuzo ya TRA ya mlipa kodi, basi MoDewji usitusumbue kuwa wewe ni namba 1 Afrika

Bakhresa ameshinda tuzo ya TRA ya mlipa kodi, basi MoDewji usitusumbue kuwa wewe ni namba 1 Afrika

Mtu anayelipa kodi bila kusumbuliwa kwanza na TRA ni sawa na mtu mwenye moyo wa kutoa sadaka, havihusiani na kuwa namba moja Africa. Yawezekana kutolipa Kodi ndo kumemplelekea kuwa namba moja. Ukitumia logic utaelewa. Tatizo mnaleta ushabiki wa Simba na Yanga, Alikiba na Diamond kwenye kila kitu.
Kwa ujumla ubaguzi ni kitu kibaya.
Kama Mo angekuwa mkristo wafia dini wangeleta udini na kusema kwakuwa mo ni mkristo ndiyo maana ulipa Kodi bora kapewa Bakhresa Musilam.
 
Kinachohuzunisha ukimuuliza ni lini na wapi Mo Dewji "alijitangaza" tajiri namba moja ataishia kuweweseka tu.
Siandiki kitu bila ushahidi, soma hii cover ya Forbes magazine ya March 2026:-
Screenshot_20260702_102636_Chrome.jpg
 
Umasikini mbaya sana, tutafute hela wakuu. Hapa wanaume na pumbu zao kama vibuyu wapo wanachamba umbeya kwenye hela za watu
Huna hela nenda katafute, kwa nini unekumbilia uzi huu. Kwanza kabisa ungekuwa na akiki ungegundua kuwa uzi wetu ni wa kizalendo na siyo majungu. Tunataka kodi zikusanywe equitably kadri ya mapato ya mtu. Tatizo watu wa Facebook mnakuja na akili ya pangu paku huku.

Huku ni kwa watu wenye akili tu
 
Alipopata mtaji Kwa kushona viatu unguja akapanda mashua na kuja Kariakoo kuuza viazi na uji.
Alifungua hoteli Nawaz pale kituo cha mabasi ya kwenda Gongo LaMboto pale Gerezani na Hotel ya Azam pale pembeni ya Soko la Kariakoo mtaa wa Mkunguni
 
Kiswahili kigumu, ushasikia mlipa kodi binafsi...
Nina uhakika hapa wanamaanisha kodi za kampuni ya Azam ndizo kodi za Bakhresa kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa. Huwezi kuchukua corporate tax halafu useme ni kodi za mtu binafsi. Labda kama ingekuwa ni kodi(personal income) kutoka kipato binafsi cha Bakhresa kutoka kwenye faida inayotengeneza Azam.
 
View attachment 3620353

Mwenyekiti wa kampuni za Said Salim Bakhresa (SSB), Said Salim Bakhresa amepewa Tuzo ya Mlipa Kodi Mwenye Hadhi ya Juu katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bakhresa ameshinda tuzo hiyo iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya TRA kumtunuku tuzo kama hiyo katika mwaka wa fedha uliopita wa 2024/2025.

Mytake:
Siku zote MoDewji anafai kuwa yeye ametangazwa na Forbes kuwa ni tajiri namba moja kijana Afrika, swali je analipa wapi kodi?

Kama analipa kodi sawasawa mbona hatujawahi kumukna akinyenyua mabega kubeba tuzo?

Hitimisho:
Huwezi kuwa Bilionea namba moja hata Dar es Salaam tu halafu unalialia kulipa Tsh 20 Bilion za 49% ya Simba Sports
Wazanzibar wanapeana
 
Nina uhakika hapa wanamaanisha kodi za kampuni ya Azam ndizo kodi za Bakhresa kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa. Huwezi kuchukua corporate tax halafu useme ni kodi za mtu binafsi. Labda kama ingekuwa ni kodi(personal income) kutoka kipato binafsi cha Bakhresa kutoka kwenye faida inayotengeneza Azam.
Nadhani ni uandishi tu kwa vile Bakhresa ni maarufu kuliko makampuni yake. But I think hii ni kodi SSB Group of companies
 
Back
Top Bottom