Bakhresa ameshinda tuzo ya TRA ya mlipa kodi, basi MoDewji usitusumbue kuwa wewe ni namba 1 Afrika

Narudia tena mo ana mbinu na mtaalamu wa biashara, anabiashara ambazo ndio UTI wake wa mgongo na zinampatia pesa nyingi na ziro tax payment rate mfano pitia hapa

https://www.businessresearchinsights.com/market-reports/sisal-fiber-market-120531

Angalia contribution yake kwenye sisal duniani alafu Rudi kwenye Sera zetu zinasemaje kwenye exportation ya zao Hilo.

Ndio maana utaona anafanya marketing kwenye food, beverage and soap na bizaa nyingine ambazo zina high competition pia mapato yake ni madogo Ku kwepa tax.

Lakini huwezi msikia akiongelea mazao, na resources nyingine zinazompatia utajiri kama chuma. Huwezi kuwa tajiri bila ku
Unatumia nguvu nyingi kutetea uwongo. Kama MoDewji ni bilionea aweke hizo Tsh 20 B za Simba tuelewe
 
duh, siamini hiyo orodha kama dola bilionea namba 1 east afrika rostam na makampuni yake siyo namba 1 kwenye kulipa kodi tanzagiza, najua Balesa analipa kodi lkn sikutegemea kama ni namba 1 kwa wafanyabishara binafsi ukichukulia biashara zake ndiyo ni nyingi lkn bado huwezi kuliganisha na oil companies ...
Nakunukuu..."Oil Companies",,,,,, Bakhresa ni mnyenyekevu sana na hana makuu,hajitapi wala hajionyeshi....
Anamiliki kampuni ya mafuta..... inanunua mafuta ya jumla na ana visima vya kuhifadhi mafuta Zanzibar....

Ni kati ya waTanzania wachache sana wanaomiliki Meli kubwa za mizigo.
 
View attachment 3620353

Mwenyekiti wa kampuni za Said Salim Bakhresa (SSB), Said Salim Bakhresa amepewa Tuzo ya Mlipa Kodi Mwenye Hadhi ya Juu katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bakhresa ameshinda tuzo hiyo iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya TRA kumtunuku tuzo kama hiyo katika mwaka wa fedha uliopita wa 2024/2025.

Mytake:
Siku zote MoDewji anafai kuwa yeye ametangazwa na Forbes kuwa ni tajiri namba moja kijana Afrika, swali je analipa wapi kodi?

Kama analipa kodi sawasawa mbona hatujawahi kumukna akinyenyua mabega kubeba tuzo?

Hitimisho:
Huwezi kuwa Bilionea namba moja hata Dar es Salaam tu halafu unalialia kulipa Tsh 20 Bilion za 49% ya Simba Sports
Shida yako unakariri, si lazima tajiri namba moja awe mlipa kodi bora; Ishu ni simple tu ni kwamba;
Utajiri hupimwa kwa thamani ya mali alizonazo mtu (kampuni, hisa, majengo, ardhi, uwekezaji n.k.).
Kodi inayolipwa hupimwa kwa kiasi cha mapato yanayotozwa kodi na shughuli za biashara katika kipindi fulani.
Mfano:
Mtu anaweza kuwa tajiri sana kwa sababu ana hisa nyingi kwenye kampuni, lakini mwaka huo akawa hajauza hisa au hajapata mapato makubwa yanayotozwa kodi.
Kampuni kubwa yenye mauzo makubwa inaweza kulipa kodi nyingi kuliko mtu tajiri binafsi.
Haya je wajua kodi ambazo Bakhresa zimetokana na nini, unajua utajiri wa Mo mfumo wake ni wa namna gani, mauzo ya bidhaa vs hisa n.k
Utajiri siyo noti za 10k
 
Acha kuandika hisia. Yaani uwe na mali chache halafu ulipe kodi kubwa?

Hivi mbona mnmu underrate sana Bakhresa?? Ni Mtanzania gani ambaye hatumii bidhaa angalao moja ya Bakhresa?
 
Acha ukilaza wewe, so kama nimeandika kihisia ina maana umepata hisia baada ya kusoma nilichoandika siyo? Wapi nimesema ukiwa na mali chache utalipa kodi kubwa? Rudia kusoma nilichoandika vizuri, tena usome horizontally na si vertically...
Halafu lazima utambue kuna tofauti kati ya mlipa kodi bora vs kodi kubwa.
Kuwa mlipa kodi bora haimaanishi ni malipo makubwa ya kodi, hakuna mahali TRA walisema Azam walilipa kodi kubwa kuliko makampuni mengine.
Pia fahamu kwamba kampuni inaweza kuwa kubwa lakini kwa mwaka husika ikawa na faida kidogo, hivyo malipo ya kodi yakawa si makubwa and viceversa.
Lakini pia kampuni inaweza kuwa ndogo lakini ikawa na ulipaji bora wa kodi, mfano kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati,na kwa kufuata sheria za kodi.
Nakupa mfano kidogo hapa ili ukilaza ukutoke; Timu ya mpira, inaweza kuwa na bajeti kubwa zaidi, lakini timu nyingine ikawa bingwa kwa sababu ilifanya vizuri zaidi msimu huo.
 
Huwezi kuficha upungufu wa uelewa kwa kuandika insha ndefu. Unachanganya hoja rahisi kisha unajisifu kana kwamba umeeleza jambo la kipekee. Hakuna aliyeshindwa kutofautisha mlipa kodi bora na kodi kubwa; tatizo ni ulivyowasilisha hoja yako kwa mkanganyiko. Ukijifunza kuandika kwa mantiki badala ya majivuno, hutahitaji kuwaita watu vilaza ili kuficha udhaifu wa hoja zako
 
Kwa ufupi wewe ni KILAZA.
 
duh, siamini hiyo orodha kama dola bilionea namba 1 east afrika rostam na makampuni yake siyo namba 1 kwenye kulipa kodi tanzagiza, najua Balesa analipa kodi lkn sikutegemea kama ni namba 1 kwa wafanyabishara binafsi ukichukulia biashara zake ndiyo ni nyingi lkn bado huwezi kuliganisha na oil companies ...
Hapa umetumia figure na data zilizopo au mawazo yako?
 
Yogesh manek amewahi kuwa mlipaji Bora wa Kodi binafsi mwaka 2017 na 2018 na top ten ya matajiri alikuwa hayumo
Kwanini alikuwa hayumo? Ni nani anayeorodhesha utajiri wa wafanyabiashara wa Tanzania? Je unafahamu uwekezaji wote wa Yogesh Manek?
 
Ni kituko kusema Azam wanalipa kodi kubwa zaidi kuliko Vodacom, TBL, SBL au CRDB
Azam ni sehemu ya Bhakresa Group of Companies Azam hailipi kodi peke yake, BGC inakusanya mapato na faida kutoka kampuni zake zote ikiwemo Azam ndio inalipa kodi hapo ndo utajua kwamba BGC ni kubwa kuliko hizo kampuni zote ulizotaja hapo juu.
 
Yogesh manek amewahi kuwa mlipaji Bora wa Kodi binafsi mwaka 2017 na 2018 na top ten ya matajiri alikuwa hayumo
Kwani kulipa kodi nyingi ndo kwamba automatically unakuwa tajiri? Unaweza kulipa kodi kubwa kwa mwaka husika na usiwe kwenye list ya hata top 20 ya matajiri kwa sababu utajiri tunaoongelea hapa (kifedha na mali) unakusanywa kwa miaka mingi sio miaka miwili au mmoja!
 
Acha kuandika hisia. Yaani uwe na mali chache halafu ulipe kodi kubwa?

Hivi mbona mnmu underrate sana Bakhresa?? Ni Mtanzania gani ambaye hatumii bidhaa angalao moja ya Bakhresa?
Jamaa kakupa facts kwenye uzi wake wewe ndo umeleta hisia
 
Ndiyo alisema kupitia Forbes. Ila nina waswasi utaniuliza tena kuwa Forbes ni nini?
Yeye hakusema, Forbes wenyewe ndo walisema, na walisema baada ya kuangalia na kutathimini mali anazomiliki (Ardhi, hisa, viwanda, nyumba, magari, biashara) na fedha taslimu benki.
 
Back
Top Bottom