BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa

BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa

.
FB_IMG_1679815790645.jpg
 
Nimewataja kwa maana hii ifuatayo, yeye kasema mtaani kwao kuna mmoja binti mmoja mapepe sana, hivyo ni bora tu aolewe akiwa na umri huo mdogo. Sababu yake kuu ni huo umapepe wa huyo binti. Sasa binafsi nikawaza, kama kuna mashoga mtaani kwake, tuwaache tu waendelee na tuukubali ushoga wao kisa wao wanapenda?
Sasa utawaua ufungwe na serikali?

Wakanyeni watoto wenu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Vijana wanatakiwa wakaulize mama zao waliolewa wakina na umri gani
Hawana haja ya kuuluiza mama zao. Kwa dunianilivyi sasa na kwabtunayiyaona Tanzania, wajiulize wao wenyewe, wameanza ngono wakiwa na umri gani?
 
Kwan Mtume Muhammad SAW Alioa binti wa miaka mingapi??

tusitoke njee ya utaratibu wa role model wetu
 
Kwan Mtume Muhammad SAW Alioa binti wa miaka mingapi??

tusitoke njee ya utaratibu wa role model wetu
Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam alioa wake 11 wa umri tofauti tofauti.

Kwani sheria za Tanzania zinafata maisha ya Mtume Muhammad Salla Allahu alayhi wasalaam?
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe.
Hawana akili kama marehemu aliyeoa binti wa miaka 6
 
Ulikuwa mtoto ila Fredy alikuwa anakupelekea moto kama kawa 🤣
Sijui umetoka kwenye malezi gani lakini mimi malezi niliyolelewa wakati huo wala nilkua sitambui habari za mahusiano katika umri huo,nilikua nasoma

Sikulaumu sana, kila mtu kuna namna amelelewa na kuna mazingira aliyokulia, bado nasisitizi msichana wa miaka 12-17 bado ni mtoto na hapaswi kuingizwa kwenye swala la ndoa, anahitaji elimu na muongozo

Sema kila mzazi ana namna anavyotaka kulea, kama unahisi binti yako ya miaka 12 amekomaa wewe ozesha hasara sio kwangu

Mimi binti yangu wa miaka 13 bado namchukulia kama mtoto na ninakazana kuhakikisha anatimiza ndoto zake kwa gharama yoyote
 
Nilijua una exposure kumbe we kibibi bado mshamba hivo Lucky ni kifupi cha jina Luckson, au huko kwenu kina "son" ni wanawake?
Kuna Lucky hapo, siyo "luck".
. Vipi kijana unabadili jina mpaka linakuwa la kike?

Usijali, tunawafahamu vijana wa sasa, mnapenda mambo ya kike. Ni chaguo lako.

Atakae oa au kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kama havunji sheria za nchi pia ni chaguo lake. Kama anavunja sheria za nchi, si sawa.
 
Sikubalian nao kabisa binti wa 14 ni ubakaji wa watoto tena wafungwe maisha.

Watoto wahimizwe kusoma ili kuondoa ujinga kichwan na sio kuwaza waolewe tu ndoa zenyewe ngumu na mateso mtoto atawezaje kuhimili visa vya mama mkwe na wifi kama mimba tatizo tutawekea njiti
Ina maana hukubaliani na marehemu Nyerere? Maana Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) "limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe".

Ina maana hiyo sheria ipo toka mwaka 1971.

Au hujaisoma vizuri post namba 1?
 
Ina maana hukubaliani na marehemu Nyerere? Maana Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) "limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe".

Ina maana hiyo sheria ipo toka mwaka 1971.

Au hujaisoma vizuri post namba 1?
Sikubalian na yeyote kwa hilo
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe.
Mm nitoe maoni yangu sasa baada ya kusoma badiko hili jana nikapitia paper mbalimbali za maswala ya sheria za ndoa katika nchi mbalimbali duniani.

Swala la umri kwanza alichokisema huyo mwanasheria ni maoni yake akirefer Quran ila pia quran hiyohiyo haikuweka umri sahihi wa binti aolewe akiwa na umri gani, bali anaweza kuolewa ata akiwa mimba tumboni ila kuingiliwa ni lazima awe amepevuka yani amevunja ungo.

Sasa kwa upande wa ulaya pia na wao wamepitia vipindi tofauti tofauti mfano mwaka 1800 sheria ya wingereza ziliruhusu binti wa kike aolewe akifika miaka 12 tu.

Kwetu sisi sheria ya 1971 inaruhusu binti kuolewa na miaka 14.
kwa maoni yangu sheria hizi za ndoa zina mkanganyiko mkubwa kwani kuna swala la tamaduni, imani na mazingira vinaingiliana humo.

Kwa maoni yangu kwa sasa na mazingira tuliyonayo binti wa kike angalau aolewe akifika miaka 18 kwa hiyo naunga mkono sheria yetu ya sasa.

Tunapaswa kumpa binti muda aweze kujifunza elimu mbalimbali za afya, mazingira na jamii hasa kwa wakati huu ni hatari sana kuruhusu binti wa miaka 14 au chini ya hapo kuolewa, maana binti hatakuwa na utambuzi wa mambo mengi na hasa mazingira ya sasa ni tofauti sana na mazingira ya huko nyuma dunia ya sasa ili usurvive lazima uwe na maarifa ya msingi angalau. hayo maarifa huwezi kuyapata yakakamilika ndani ya umri wa miaka 14.. angalau miaka 18.
 
Muarabu amejua kuvuruga wa afrika kupitia dini,sasa wewe unaoa mtoto wa miaka 14 ili iweje? ndoa sio kufanya tendo tu
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema Serikali kuzuia mtoto wa umri wa miaka 14 kuolewa ni kuzuia kumuabudu Mungu na kumruhusu shetani aingie kati.

Akizungumza na Swahili Times, Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikhe Hassan Chizenga amepinga kubadilishwa kwa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, hasa kipengele kinachoruhusu binti wa miaka 14 kuolewa kwa idhini ya mahakama katika mazingira maalum.

“Ndoa ina maana mtoto wa kike na wa kiume waruhusiwe kufanya tendo la ndoa, wawe wapenzi. Ikifanywa akatajwa Mungu na usimamizi wa wazazi kosa, lakini ikifanywa kiholela bila usimamizi wa wazazi ni sawa, mimi naona hiki ni.. [akitaja neno kali].

Kama Serikali inagawa kondumu ili kuwakinga na maambukizi, hivyo basi imekubali ndoa ya shetani iwepo lakini ya Mungu isiwepo. Sera ya nchi yetu inakubaliana kwamba haja ya kufanya hivyo [kujamiiana] ipo,” amesema.

Aidha, amesema dini haijataka kila mtoto aozeshwe akiwa na umri wa miaka 14, ila pale dharura itakapolazimu basi asizuiwe na kulazimishwa kuzini kwa sababu sheria inamlazimu.

“Sisi tunahamasisha watoto wasome. Wale ambao wako katika uwezo wa kuweza kusoma na wazazi wanawaendeleza wasome, ile elimu yenyewe automatically [moja kwa moja] itamfanya mtu asiwe na kiu ya lile jambo. Lakini kuna huyu mtoto ambaye masikini darasani haelewi akifundishwa hafahamu, ana miaka kumi na, na pengine kapewa umbo zuri lapendeza. [..] Sheria ya ndoa 1971 haijamzuru yeyote,” ameeleza.

Hata hivyo Chizenga ameongeza kuwa ndoa zinazofungwa hufanyika chini ya usimamizi wa wazazi hivyo wanaweza kuwaangalia na kuwaelekeza majukumu mbalimbali.

Chanzo: Swahili Times
 
Lakini kuna huyu mtoto ambaye masikini darasani haelewi akifundishwa hafahamu, ana miaka kumi na, na pengine kapewa umbo zuri lapendeza. [..] Sheria ya ndoa 1971 haijamzuru yeyote,”
 
Back
Top Bottom