BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa

Masheikhe waache ulafi!
 
Yaani mtu amesoma sheria mpaka kuwa mwanasheria mkuu wa Bakwata haoni aibu kuongea Upumbavu kama huu...?...anajua mtoto wa miaka 14 alivyo? Kweli ataweza kubeba majukumu ya kuwa mke achilia mbali kuwa mama? Na shule je?.

Aisee...inasikitisha sana.
Halafu huyo mwanasheria hawezi kukubali binti yake aolewe akiwa na umri huo
 
Khhha..
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe.
Kama ni binti yangu wa miaka 14 umlazimishe umuoe hata kwa kumsomea albadiri ujue kwangu bado ni ubakaji. Nikishindwa kukushughulikia kisheria nitatumia njia nyingine kukumaliza
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe...
Nakubali sisi Watanzania wengi huwa wavivu wa kufikiria hata jambo liwe dogo kiasi gani, na huo ni ujinga , hivi unasema asiolewe ili hali anafanya machafu na watu wazima wa kila rika?

Hivi kati ya penati na mpira wa kurushwa bora nini?, una sema asiolewe sasa akija kutiwa mimba ndio utaona kila mtu mbaya na kesi juu.

Natoa mfano wa mwisho true story, mume wa dada angu ana mtoto anayepaswa kuanza form1 mwaka huu 2023 , lakini ile desemba tu kakutwa ana mimba na hadi sasa mimba ni kubwa, baba yake ni mkulima tu, mama yake mzazi yupo mbali na hyo dada angu ni mama wa kufikia tu na aliyempa mimba ni mwanafunzi mtoto wa form 2, sasa hebu fikiria hii, mtoto ata mlea nani ?, si bora ange olewa tu
 
kama ni binti yangu wa miaka 14 umlazimishe umuoe hata kwa kumsomea albadiri ujue kwangu bado ni ubakaji. Nikishindwa kukushughulikia kisheria nitatumia njia nyingine kukumaliza
... hata hao maustaadhi wenye elimu zao sioni wa kuruhusu mwanae aolewe at 14! Wanacheza na akili za wajinga wasiojielewa! Eti binti wa SSB au wa mama aolewe at 14! Thubutu!
 
Sikubalian nao kabisa binti wa 14 ni ubakaji wa watoto tena wafungwe maisha.

Watoto wahimizwe kusoma ili kuondoa ujinga kichwan na sio kuwaza waolewe tu ndoa zenyewe
Ni kweli wote wanaomaliza la Saba(miaka 14) huendelea na masomo!?..wanaokwama kusoma wafanyeje!?..wapate uzoefu wa ngono mitaani mpaka watapofika miaka 18!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…