BAKWATA yampa Cheti cha Pongezi Rais Uhuru Kenyatta kwa kusitisha hotuba ili kupisha adhana!

BAKWATA naona wameachwa yatima sasa akili zimeanza kurudi mwanzo walikuwa kama tawi kuu la CCM
 

Hawa mabeberu wa kiimani wa Mashariki ya Kati na Ulaya wanatugawa sana waafrika kwa kutumia dini.

Naungana nawe lazima tustuke na kuzinduka kuhusu hizi imani za kigeni zisizo na mizizi yake Afrika kupitia matambiko, ngoma, madogoli, mahoka na miti mikubwa.

Na mara nyingi imani zetu za kiAfrika tulizifanyia mwituni mbali na miji au vijiji ili kupata ukimya na kutuwezesha roho, akili na kupandisha mizuka ndani ya bongo zetu kuwafikia miungu wetu wa asili wa kiafrika.

Hizi dini za kuja wao badala ya kujenga nyumba zao za ibada sehemu za utulivu wameamua kujenga maeneo yenye "vurugu" kibao na kuingilia maisha ya kila siku iwe usingizi, fiesta n.k Yaani dini hizi hazifuati kutafua sehemu na mazingira tulivu yasiyoingiliana na shughuli zingine za kila siku za wanajamii.

Ibada za imani zote zirudishwe "mwituni" kama mababu na mabibi zetu walivyokuwa wanafanya. Hata tendo la jando na unyango likifanywa mbali na makazi ya watu. Sasa angalia jando na unyago wa siku hizi linafanyika mtaani kwenye mazingira tofauti na jadi na desturi zetu za kiafrika.
 

Muafaka ni masuala haya ya dini hizi za kuja yafanyike "mwituni" au "vichakani" mbali na makazi ya watu. Hata vitabu hivyo vya dini ya kuja utaona makafara, kumkaribia Mungu au kuongea na Muumba wao vikifanyika mbali mlimani kwenye utulivu sawasawa kabisa na jadi zetu za imani za asili vile mababu zetu walitoka na kwenda mbali na makazi ya watu ili waongee na Miungu wao.

Mipango miji warudishe utaratibu nyumba za ibada ziwe nje ya miji yetu.
 
Hawa Bakwata wameshakosa kibali cha Waislam wa Tanzania ndiyo maana wanajisogeza sogeza kwa wanasiasa. Watatumikishwa sana na CCM
 
Hicho cheti kiko wapi? Baraza la waislamu la Kenya ndio wamentunukia Uhuru cheti na kimeoneshwa. Sasa sijui wewe ni msemaji wa Bakwata? Angalau ungeliweka ushahisi sio maneno matupu tu
Kuna wakati najiuliza watu Kama wewe sijui mna mtindio wa ubongo au tatizo Nini?
 
Uhuru anatakiwa apewe na cheti kingine cha kuwa 'Baba wa Demokrasia Africa'
 
Mwenyezi Mungu Mwenye Kuneemesha Ridhiki Kubwa Kubwa Na Ridhiki Ndogo Ndogo!!!
 
Uliona wapi mshirika na mashoga akawa na Soni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…