Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Baada ya tukio lile Joseph Sokoine alirejeshwa nyumbani haraka.
Acha kupotosha wewe, mheshimiwa Balozi Joseph Sokoine, aliteuliwa na Rais hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa naibu katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoka kuwa balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, hapo alifanya kazi na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, inawezekana ndipo alitambua uwezo wake
Kwa taarifa yako, katibu mkuu/ naibu katibu wa wizara yeyote mkuu ana hadhi kubwa kuliko balozi anayetuwakilisha kwenye taifa lolote
Kwa maana hiyo, hayati Rais Magufuli alimpa promotion kutoka kuwa balozi kwenda kuwa naibu katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais
Na hata alipoteuliwa kuwa naibu katibu mkuu, bado aliendelea kuwa na hadhi yake ya BALOZI
Acheni upotoshaji wa hovyo hovyo