Alirudishwa kwa sababu alienda kumtembelea lissu hospitali ubalgiji
Acha uongo wewe
Mheshimiwa balozi Joseph Sokoine, aliteuliwa na hayati Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa naibu katibu mkuu wa ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kutoka kuwa balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji
Kwa taarifa yako, katibu mkuu( Permanent Secretary) / Naibu katibu mkuu( Deputy Permanent Secretary) wa wizara yeyote, ni wakubwa kuliko balozi wa Tanzania anayetuwakulisha kwenye nchi yeyote hapa duniani
Hata kwa majukumu ya kazi, katibu mkuu/ naibu katibu mkuu wa wizara, wana majukuku makubwa zaidi na mazito kuliko balozi
Kwa taarifa yako, balozi ana ripoti kwa mkurugenzi wa idara( eneo husika ambalo nchi ya balozi ipo) kwenye wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
Kwa mfano, balozi wa Tanzania nchini China, ana ripoti kwa mkurugenzi wa idara ya Asia na Australia, kwenye wizara ya mambo ya nchi na ushirikiano wa kimataifa
Na wakurugenzi wa idara wizarani, wapo chini ya katibu mkuu na naibu katibu mkuu
Kwa hiyo balozi Joseph Sokoine kuteuliwa kuwa naibu katibu mkuu, ilikuwa ni promotion na sio demotion
Kws hiyo tuache propaganda za hovyo juu ya hayati Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli