Balozi Mbelwa Kairuki: Mpaka sasa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyeambukizwa maradhi ya Corona

Balozi Mbelwa Kairuki: Mpaka sasa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyeambukizwa maradhi ya Corona

Leo Februari 11, 2020 Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amezungumza kuhusu video inayowaonesha vijana wa Kitanzania wanaosoma China wakiomba msaada wa kurejeshwa makwao.

Balozi ameeleza kuwa mpaka sasa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyeambukizwa maradhi hayo kutokana na kufuata maelekezo wanayopata kutoka kwa mamlaka za China.

Amesema mara kwa mara huwasiliana na wanafunzi hao pamoja na serikali ya China ili kufahamu na kutatua changamoto ndogo zinazowakabili na ameishukuru serikali ya China kwa ushirikiano wanaotoa kwa vijana wa Kitanzania.

Balozi akasema dawa imegunduliwa na Idadi ya watu wanaopona imeongezeka huku Idadi ya maambukizi ikipungua kwa asilimia 50 nje ya mji wa Wuhan ambao ndio kitovu cha virusi hivyo hatari.

Balozi akasema kuwa kuishi kwa kufuata maelekezo ndilo jambo linalomfanya hata yeye kubaki hai. Amesema hawaruhusiwi hata kutoka nje na kwamba kitendo cha kukusanyika walichokifanya vijana hao ni hatari sana kwa afya zao.

Kuhusu ombi la vijana hao kurejeshwa Tanzania, Balozi Kairuki amesema hakuna usafiri wowote unaoruhusiwa kutoka ama kuingia kwenye mji wa Wuhan na kwamba Japan ilijaribu kuwaokoa vijana wake lakini kwa bahati mbaya wakaambukizwa na kuvibeba virusi hivyo mpaka nchini kwao.

Balozi akasema virusi hivyo ni hatari na kwamba serikali ya Tanzania haitafanya kitendo chochote kitakachokuja kuwadhuru Watanzania walio wengi.

Balozi huyo akasema kitendo walichokifanya vijana hao kimetokana na msongo wa mawazo unaotokana na kukaa ndani ya uzio wa makazi yao bila ruksa ya kutoka nje.

Balozi Kairuki akatoa wito kwa Watanzania kumuombea yeye na Watanzania wengine wanaoishi China ili Mwenyezi Mungu awavushe salama na kadhia hiyo. Pia amewaomba wazazi kuwapa faraja vijana wao waliopo China ili waondokane na msongo wa mawazo.

Nukta Muhimu: Tatizo lililopo China lisitumiwe kisiasa kwani serikali haiwezi kutumia nguvu kwenda kuwachukua vijana hao kwakua imejifunza kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa Serikali ya Japan ilipoamua kuwarudisha raia wake nchini mwao waliokuwa wanaishi China.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mke wa balozi anaendeleaje na yule mdogo wake Jesi ?
 
Tunachotaka kujua lini watawarudisha Au mpaka waambukizwe😕


Everyday is Saturday...............😎
 
Naelewa na sijakurupuka una hofu na nini..? Mi nataka kujua maamuzi ya serikali yangu wala sijasema nipo kwenye mlengo upi.
Maamuzi ya serikali yameelezwa na balozi kairuki , Soma bandiko vizuri
 
Kule walipo wanafunzi wetu wa kitanzania ndipo serikali ya China imeweka kituo cha kuwahudumia wagonjwa. Kwa hiyo, uwezekano wa wao kuambukizwa na kuuawa na virusi ni mkubwa sana. Wakiletwa nyumbani na kuwa isolated eneo la mbali kama vile kule Mabwepande watakuwa salama zaidi. Sijui kwanini watu mnakuwa wagumu wa kuelewa.
Si kweli kwamba China imeweka Wuhan kama sehemu ya kuwahudumia wagonjwa, isipokuwa virus zilianzia hapo. Kwa sasa huo mji wote umekuwa isolated.

Wengi waliokufa ni wale waliopata maambukizi ya awali wakati ufahamu wa virus ulipokuwa mdogo na kwa sasa wengi wanaokufa ni wale wanaochelewa kuripoti.

Other wise huko Wuhan spread rate imeshuka na idadi ya wanaopona imeongezeka kama utawai kuripoti washajua namna ya kumdhibiti. Ata huyo super-spreader wa UK leo karuhusiwa kurudi nyumbani.

Usichukulie poa kuna meli hizi za cruise nadhani ilisimama Hong Kong au somewhere in China, wakati outbreak inaanza japokuwa hakuna mgonjwa ata mmoja humo ndani mpaka leo sasa hivi wiki ya tatu ipo majini hakuna nchi inataka ifanye docking kwao, sio abiria tu wakifika inabidi wawe quarantined bali na meli yenyewe yote.

Ndege ikitua hapo hujui nani ataigusa, wanafunzi usafiri wao wa kutoka huko walipo mpaka airport hujui kwenye hiyo coaster alikaa nani; waliofunga access ya kuingia na kutoka Wuhan sio kwa bahati mbaya bali kuzuia spread ambazo unaweza pata kwa namna nyingi.
 
HILI NI JAMBO AMBALO MAMLAKA WANAPASWA KULIAMUA KWA AKILI MNO, ILA MTOA UKUMBUKE KUWA SERIKALI YOYOTE ULINZI WA RAIA WAKE NI JAMBO LA KWANZA KABISA
 
Je hamna wageni wanaotoka huko? Kama wapo tutajuaje kama hawana vimelea
 
Mimi kwa maoni yangu naona wachukuliwe then wakifikishwa hapa Tanzania wawe isolated yaani watengewe sehem yao ya kukaaa halafu waletwe wataalam wa kuwapima ugonjwa Huo ili kama kuna aliepata maambukizi akae huko huko hadi apate matibabu na ambao hawana maambukizi waruhusiwe kujiunga na familia zao.


Wahenga walisema.".mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani"



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom