Balozi Mbelwa Kairuki: Mpaka sasa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyeambukizwa maradhi ya Corona

Balozi Mbelwa Kairuki: Mpaka sasa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyeambukizwa maradhi ya Corona

Akili zingine bhana! Kwa hiyo serikali inasubiri waugue wafe ndipo arudishe mizoga nyumbani au watawazika huko huko Wuhan?
Leo Februari 11, 2020 Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amezungumza kuhusu video inayowaonesha vijana wa Kitanzania wanaosoma China wakiomba msaada wa kurejeshwa makwao.

Balozi ameeleza kuwa mpaka sasa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyeambukizwa maradhi hayo kutokana na kufuata maelekezo wanayopata kutoka kwa mamlaka za China.

Amesema mara kwa mara huwasiliana na wanafunzi hao pamoja na serikali ya China ili kufahamu na kutatua changamoto ndogo zinazowakabili na ameishukuru serikali ya China kwa ushirikiano wanaotoa kwa vijana wa Kitanzania.

Balozi akasema dawa imegunduliwa na Idadi ya watu wanaopona imeongezeka huku Idadi ya maambukizi ikipungua kwa asilimia 50 nje ya mji wa Wuhan ambao ndio kitovu cha virusi hivyo hatari.

Balozi akasema kuwa kuishi kwa kufuata maelekezo ndilo jambo linalomfanya hata yeye kubaki hai. Amesema hawaruhusiwi hata kutoka nje na kwamba kitendo cha kukusanyika walichokifanya vijana hao ni hatari sana kwa afya zao.

Kuhusu ombi la vijana hao kurejeshwa Tanzania, Balozi Kairuki amesema hakuna usafiri wowote unaoruhusiwa kutoka ama kuingia kwenye mji wa Wuhan na kwamba Japan ilijaribu kuwaokoa vijana wake lakini kwa bahati mbaya wakaambukizwa na kuvibeba virusi hivyo mpaka nchini kwao.

Balozi akasema virusi hivyo ni hatari na kwamba serikali ya Tanzania haitafanya kitendo chochote kitakachokuja kuwadhuru Watanzania walio wengi.

Balozi huyo akasema kitendo walichokifanya vijana hao kimetokana na msongo wa mawazo unaotokana na kukaa ndani ya uzio wa makazi yao bila ruksa ya kutoka nje.

Balozi Kairuki akatoa wito kwa Watanzania kumuombea yeye na Watanzania wengine wanaoishi China ili Mwenyezi Mungu awavushe salama na kadhia hiyo. Pia amewaomba wazazi kuwapa faraja vijana wao waliopo China ili waondokane na msongo wa mawazo.

Nukta Muhimu: Tatizo lililopo China lisitumiwe kisiasa kwani serikali haiwezi kutumia nguvu kwenda kuwachukua vijana hao kwakua imejifunza kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa Serikali ya Japan ilipoamua kuwarudisha raia wake nchini mwao waliokuwa wanaishi China.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa jamaa wa CCM na serikali yao nadhani wanawaza kwa kutumia tundu la haja kubwa[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32]
Kwanini Serikali yetu hukibilia Mungu kwa jambo linalohitaji utekelezaji? Akili tuliyopewa na Mungu na kodi tunayotoa kama haiwezi kuwasaidia watu wetu tunalipa kodi ya nini.

Halafu unakimbilia eti tatizo hilo isitumike kisiasa wakati siasa ni maisha na ni kila kitu acheni kudanganya watu. Haya mambo yanakera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo badala ya watu waikimbie hatari unataka wafie huko kwa 'maslahi ya taifa'? Are you lunatic????
Tusilichukulie kisiasa jambo hili, kwa jinsi wabongo tulivyo hao wakirudi bahati mbayo gonjwa likaja nchin lazima tutaanza kuilam serekali kwa maamuzi iliyochukua ni bora tu kufuata huo ushauri, ingawa naajua wenye ndugu zao huko wanaumia Sana
Inabidi tu iwe hivyo kwa maslah ya taifa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawashangaa sana hawa matutusa wa serikali kuwazuia wanafunzi kurudi nyumbani wafie China[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32][emoji32]
Kuna statement inasema chuo walichopo ndipo wagonjwa wanapopelekwa, kama ni kweli hapo huwezi kuwa na matumaini hata kwa kusali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kurudishwa huku ni ngumu basi hata wasaidiwe kukaa vyema kisaikolojia huko waliko. Inaonekana wana msongo sana.
 
Serikali DHAIFU ndivyo zilivyo. Nchi za Ulaya kwa kuwa wao wanajitambua wameishawarudisha raia wao nyumbani. Kwa kuwa serikali ya CCM ni watoa kafara wakubwa, ngoja wakawatoe kafara watoto wa watu ili washinde uchaguzi 2020. Hicho ndio cha muhimu kwao.
Blah blah blah

Tumuamini Kairuki maana yeye ni mkweli?

Kuna mtu yeyote wa hii serikali ni wa kuamini akisemacho?

Tunaamini wale watoto, wao ndio wakweli zaidi ya yeyote!

Wanaomba kurudi nyumbani maana ni kwao

Wakifika wawahifadhi mahali maalumu mpaka wawe salama kutoka

Serikali bana, inakwepa majukumu kwa sababu za uongo mtupu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ndilo jambo la msingi. Tunasubiri wafe kwanza halafu tulete nyumbani maiti zenye virusi. Serikali yenu hii ni ya ajabu sana.
Tuwaombee wenzetu walioko huko Wuhan, China wasije wakaambukizwa hilo liugonjwa na jinsi ngozi nyeusi tunavyochukiwa, sidhani kama watapatiwa matibabu mazuri zaidi ya kuachwa wakufe.

Lakini najiuliza kwanini balozi anashindwa kuwatafutia makazi mbadala maana inaonekana makazi yao hayako salama kwa kuwa yamegeuzwa wodi ya kuwahudumia wagonjwa; labda pengine kwa sababu waliobaki hapo chuoni ni Waafrika tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu ombi la vijana hao kurejeshwa Tanzania, Balozi Kairuki amesema hakuna usafiri wowote unaoruhusiwa kutoka ama kuingia kwenye mji wa Wuhan na kwamba Japan ilijaribu kuwaokoa vijana wake lakini kwa bahati mbaya wakaambukizwa na kuvibeba virusi hivyo mpaka nchini kwao.

Katika sehemu zote, nilipopaelewa zaidi ni hapa tu...

Yaani ni bora mfe wachache, wengi wapone...
 
TUNAWAPENDA SANA TENA SANA ILA BORA WAKAE HUKO TU KWA SASA NAHAKIKA WATAANDIKWA KATIKA HISTORIA YA MASHUJAA WA TAIFA
Duuh!
Ulivyo andika ushawapigia hesabu kabisa watakufa mashujaa.
Hawafi, inaonekana huu ugonjwa unawashika jamii ya waasia wa mbali kama wachina, wajapan, wakorea, n.k.
 
Serikali DHAIFU ndivyo zilivyo. Nchi za Ulaya kwa kuwa wao wanajitambua wameishawarudisha raia wao nyumbani. Kwa kuwa serikali ya CCM ni watoa kafara wakubwa, ngoja wakawatoe kafara watoto wa watu ili washinde uchaguzi 2020. Hicho ndio cha muhimu kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu

Tupo na plitical class ipo radhi kuona raia wake wanakufa ugenini!

Haafu wanatoa sababu za kikvma sana aisee!

Wawalete hao watoto wawahifadhi wawahudumie mpaka wawe salama kuingia uraiani!

Ni haki yao kurudi kwao,sio hisani ni haki yao kurudi their country of origin no matter what!

Whether wanaumwa au hawaumwi,kuja ni haki yao kikatiba!
 
Hata sisi ni wazazi; tuna haki ya kuonyesha masikitiko yenu jinsi serikali inavyowazuia raia wake kurudi nchini ili wakafie China. Sijawahi kuona serikali ya kiuaji kama hii.
Sitegemei kuona serikali ikilikalia kimya ombi lao,sijui watajibiwa nini ila ningependa kujua serikali itaamua uamuzi upi wa busara na hekima!.
Sisi hata tukijadili huku mitandaoni kwamba waje au wasije bado mwenye mamlaka ya uamuzi na utendaji ni serikali.. itakuwa vyema jambo hili pia likijadiliwa bungeni ili tuone watetezi tuliowateua wanaamua nini juu ya watanzania wenzetu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
***** zako! Unataka wasitoke nje wafe au CCM mmewatoa kafara ili mshinde uchaguzi mkuu wa 2020. Are you maniac?
Hawa wanafunzi kitendo cha kutoka nje na kukusanyika ni hatari sana kwa afya zao. Walishaambiwa wasitoke nje ila wao wanaamua kukiuka masharti wanatoka na kukusanyika! wakiendelea kuwasikiliza hawa wanasiasa wetu uchwara wa upinzani wataangamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe walau umeongea fact. Lakini ujue kuwa mahali walipo wanafunzi wetu ndipo serikali imeweka base ya wagonjwa wao; so ni rahisi wao kuambukizwa ugonjwa. Bora tu warudi nyumbani halafu watakuwa isolated kwenye eneo salama. Tupo pamoja???
Hao watoto hata wakirudi Tanzania inatakiwa wawe isolated. Hakuna tofauti na wanachofanyiwa China sasa why risk their return.

Huo ugonjwa sio wa mzaha kabisa na unaweza kuwa nao kwa siku kadhaa bila ya kuhisi chochote.

Nilikuwa nasoma habari za super-spreader wa UK jamaa katoka Hong Kong (alipopatia ugonjwa), kapitia france holiday na kurudi kwao mpaka anafika yupo poa tu.

Kutokana na trail yake huko France case nne zilizobainika chanzo yeye, UK case zote 11 chanzo yeye.

Tena kwa bahati nzuri alipojihisi anaanza kuumwa alipiga simu hospitali wakamwambia ajifungie chumbani kwanza, wakampa utaratibu wa kwenda kwao na walipompokea tu straight kwenye isolated unit.

Hao wote wengine 11 waliobainika ni through back tracking ya alikutana na nani.

Kutokana na hao 11 waliopo wizara yao ya afya imetamka hali ya hatari kuwepo maana na wao aijulikani washawapa wangapi.

Wabaki huko huko China walipo hao watoto, tena washauriwe wasi interact kwa sana maana inaonekana una spread kirahisi na kama wanaishi mazingira ya hostel mmoja akiupata itakuwa balaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini waombe warudishwe? Ninavyojua ni kwamba China iko hapo karibu na Namibia . Nimeshaona mtu ametoka Naminia kwa basi. Wakiona vipi basi wakodi Costa
 
***** zako! Unataka wasitoke nje wafe au CCM mmewatoa kafara ili mshinde uchaguzi mkuu wa 2020. Are you maniac?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndiyo bure kabisa akili yako haina akili. Unaleta mambo ya siasa kwenye masuala ya msingi. Tatizo Chadema mnajifanya mnajua kila kitu. Serikali ya China imeshashauri walioko huko wasiondoke bali wakae tu ndani na wasitoke nje kwa usalama. Kitendo cha kwenda kuwachukua itakuwa kama ilivyotokea kwa wajapani baada ya kuwachukua wakiwa wazima walipofika Japani ikangundulika baadhi wameshaambukizwa tayari.
 
Back
Top Bottom