Balozi Seif: Zanzibar ndio inayonufaika zaidi na Muungano wa Tanzania

Ni kweli, jiulize tu swali kidogo kwa upande was ajira. Angalia wa Zanzibar walioajiriwa Tanzania bara na Wazanzibari wanaojishughulisha na shghuli za kiuchumi Tanzania bara, waliopo mpaka Katavi, mpakani mwa TZ na Malawi, Kigoma, Mwanza etc. Halafu ulizia Watanzania bara wanaofanya kazi Zanzibar ukizingatia udogo wa nchi yenyewe.....utakuja na hitimisho linalosemwa...hapo bado hujaangalia mambo mengine....
 
Kama anafaidika ni yy aliewekwa hapo kwa mtutu wa jeshi la kikoloni yy anaona faida pmj na Watanganyika wenzake waliojazana Nchini kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kukusaidia ndugu yangu ss watanganyika hatuna roho ya ubaguzi kama mlivyo nyinyi huku kwetu mkija mnakua huru sana kununua mashamba, kujenga , kufanya biashara na kamwe huwezi sikia mtanganyika analalamika juu ya uwepo wenu, huko kwenu sasa...
 
SI TUNAKUZA UCHUMI WENU, NA KODI TUNAWALIPA
faida ya muekezaji inakwenda pande zote mbili,
Mfano bakhresa katengeneza Ajira Nyingi mno Huko kwenu,na Pesa zake zote ziko kwenye Mabenki yenu huko.
Kimsingi nyinyi Munafaidika zaidi.
Na tukisema tumchukue bakhresa arudi Zenji Hamtokubali kwani ataleta mtingisiko mkubwa wa kiuchumi
Si ndo nyinyi munaofaidika zaid?
Au hujui calculations za Uchumi?
 
Kwa kukusaidia ndugu yangu ss watanganyika hatuna roho ya ubaguzi kama mlivyo nyinyi huku kwetu mkija mnakua huru sana kununua mashamba, kujenga , kufanya biashara na kamwe huwezi sikia mtanganyika analalamika juu ya uwepo wenu, huko kwenu sasa...
Hilo ni kweli
kwa sababu sisi hatukuwaleta Majambazi huko wala Walevi.

Tumeleta Wajasiriamali wanao uwezesha ushumi kukua kwa kasi.
Sisi watu wa Zanzibar hatubweteki huko Tanganyika,Tunachakarika kweli kweli.
Maana Elimu tumenyimwa wengi wetu kwa sababu ya ukoloni kutufelisha,
Mitaji hatuna kwa sababu ya Ukoloni wa Tanganyika kutubana,
Tumeishia Kufanya Biashara za mitaji midogo midogo,
Lakini Muungu si Athumani.
Tunapambana kama binadamu wengine.
Lakini Hata Muungano usingelikuwepo,kusingelizuia sisi kuishi huko.
Kama vile tunavyoishi Kenya, Msumbiji, Kongo.
Au Tunavyo ishi Uk na kwengineko.
 

Kwanini mpaka leo bado mumeshindwa kuifuta? Nahisi munachelewa kabisa
 
Wazambari wapo wengi huku bara wanafanya biashara mbalimbali huko mikoani mpo kibao, chakula mnaletewa Zenji kutoka bara, na mambo mengine hafu unasema hamfaidiki zaidi acha kukufuru

Hicho chakula hua kinapelekwa bure? au wananunua?
 
Kwa kukusaidia ndugu yangu ss watanganyika hatuna roho ya ubaguzi kama mlivyo nyinyi huku kwetu mkija mnakua huru sana kununua mashamba, kujenga , kufanya biashara na kamwe huwezi sikia mtanganyika analalamika juu ya uwepo wenu, huko kwenu sasa...

Mkuu umewahi kuenda Zanzibar? Na Kwani watanganyika hawako huru Zanzibar? mbona wapo hundred thousands wanaishi vizuri tu.
Tatizo sio watanganyika kuishi Zanzibar wala Wazanzibar kuishi Bara. Tatizo ni mamlaka ya kiutawala ndio wanayoyadai wazanzibar. Watanganyika wataendelea kuishi Zanzibar kwa kufuata taratibu husika na wazanzibari watatendelea kuishi Bara kwa kufuata taratibu husika.

Wamechoka kutawaliwa na Serekali ambayo wao wenyewe wameshindwa kujiletea maendelea ndani ya nchi yao. Wamechoka na CCM
 
Mkuu kwani hapa pana ushindani wa kuwa nani kamzidi mwenzake?
Umesema Zenji isingekuwa sehemu yetu ingelikuwa kama Rwanda au zaidi hapa ukidhihirisha Rwanda ni bora kuliko sisi, kwa sababu huwezi kulinganisha cha hovyo kwa cha hovyo!
.
Swali la msingi Rwanda inaizidi nini Tanganyika?
Kigali kuna daladala za baiskeli kama za Igunga, Shinyanga, Misungwi, Sengerema na Geita 😝😝😝 yaaaani sikuona hata uzuri wake
 
ameongea ukweli sasa hivi Zanzibar wameishiwa mchanga wa kujenga tumaini pekee ni bara
 
Mkuu Dodoma pale bungeni munawalipa hela zenu zipi ebu weka wazi. Ni serikali ya Tanganyika ndo inalipa au Tanzania? Ni rasimali ipi inayotumiwa kinyume na utaratibu, umepatia kabisa wakijitenga Wazanzibar ww hupungukiwi na kitu hilo ni kweli kabisa maana hata wewe huna faida yoyote kwao.
 
Kama kweli una faida sana iwe serikali moja, no baraza la wakilishi na rais, Zanzibar kuwa na wabuge nane tu na wakuu wa mikowa wawili
 
Wazambari wapo wengi huku bara wanafanya biashara mbalimbali huko mikoani mpo kibao, chakula mnaletewa Zenji kutoka bara, na mambo mengine hafu unasema hamfaidiki zaidi acha kukufuru
Msipeleke tena hicho chakula chenu cha bure huko Zanzibar, wapelekeeni mayatima na omba omba walioptapakaa kila kona hapa Tanganyika.
 
Sawa Msemajo wa Familia Ya Bakhresa tumekuelewa ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwani kuna utofauti kati ya Tanganyika na Tanzania! Kama ingekuwepo basi tusingesikia nchi inayoitwa "Zanzibar"

Wale wabunge kutoka Zanzibar wanalipwa na walipa kodi wa Tanganyika/Tanzania! na wakati huo huo wakiwa na bunge lao kule Zanzibar ambalo halina Wawakilishi kutoka Tanganyika!
 
Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Serikali ya Muungano ndio inayohudumia wizara zote zilizo chini ya Muungano kwa kutumia mapato yatokanayo na kodi, mikopo na ruzuku. Kodi hawalipi watanganyika tu hata Zanzibar TRA ipo na ina ofisi zake. Wanacholipwa wabunge na watumishi wengine wa Zanzibar huku bara ni haki yao wala si hisani ya Watanganyika kama vile ilivyo kwa majeshi, askari na watumishi wengine watanganyika wanaofanya kazi Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…