Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.
Naawatakia Muungano mwema huku nikisisitiza
Nautakia huu muungano wetu adhimu udumu milele na hivyo kukitokea yoyote anayetaka kuuchokoa muungano, namshauri chokochoko amchokoe pweza, muungano hutauweza kwasababu tutaulinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia muungano mwema.
P
Mimi nauombe Muungano huu ukumbane na corona ,na kwa vile tayari unaumwa maradhi hatarishi na jua hauta pona Ng'o
Corona ni hatari sana kwa mwenye magonjwa kama ya Muungano.kasorozake zimekuwa nyingi mno na kiasi kila tume inayoundwa kuzimaliza inashindwa kwa jinsiulivyo DHAIFU.
Corona nakuomba tuondoshee kinu juani,Muungano una maradhi sugu,na hauwezi kamwe kuwa na afya kwa jinsi ulivyo na mapungufu yasiyowezekana kutibika kwa dawa.
MUUNGANO TUUTAKAO
1.wenye Dialoge baina ya washirika wake.
2.Usiolindwa kwa mtutu wa bunduki,bali kwa mapenzi na maelewano.
3.unaowatambua washirika wake Tanganyika na Zanzibar kuwa zilikuwa nchi Mbili huru na Raia wake walikuwa huru,
4.Kila upande uwe na right ya veto kwenye mambo ya msingi ya Muungano,sio kuburuzana.
5.UWE HURU KWA NCHI NYINGINE KUJIUNGA NA KUJITOWA KWA ANAYEONA KABANWA,AU KUJIUNGA KWA MASHARTI YASIYOFANANA KWA KILA NCHI IWE HURU KUWA NA ''MINIMUM CONDITION za kujiunga''.
6.
Muungano ulenge wazo zima la Umoja wa Afrika ,na sio uishie Zanzibar tuu.
Ewe Mungu wa Mbiguni,Mungu wa baba zetu waliotangulia kabla ya Uhuru wa Nchi zetu.
Mungu wa Mkwawa,Kinjikitile,Kimweri,Abushiri,Isike, Machemba,Mwana wa mwana,Mkamandume,Bikhole,Sultan Barghash, Sultani Hamud,,na wengi walio zipigania dola hizi za Azania dhidi ya wakoloni waovu .
Tunakuomba Uvunje muungano huu mbaya na utuletee Muungano ulio Mzuri zaidi na mwema kwa watu wa pande zote husika ,na Tunakuomba ewe Mungu
Uuimarishe muungano huo mpya uwe mkubwa zaidi wenye mataifa mengi zaidina ulio chini ya mapenzi yako ewe Mungu Mwenyezi.
Amin, Amin, Amin