Uchaguzi 2020 Balozi wa Japan ashangazwa na ubadhilifu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Balozi wa Japan ashangazwa na ubadhilifu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Ambassador's Message on the General Elections 2020 / Ujumbe kutoka Balozi kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020

2020/11/4
I am troubled by the information of widespread irregularities and wrongdoings during the recent election process in this country.

I am convinced that sound democracy based upon multiparty system works best to contribute to further development and prosperity of Tanzania.

GOTO Shinichi, Ambassador of Japan to Tanzania

===
Ninashangazwa na habari za hitilafu na ubadhilifu zilizoshuhudiwa kwa wingi nchini humu katika mchakato wa uchaguzi wa hivi karibuni.

Nina uhakika demokrasia ya kweli chini ya mfumo wa vyama vingi itachangia zaidi maendeleo na ustawi wa Tanzania.

GOTO Shinichi, Balozi wa Japani nchini Tanzania
 

Attachments

  • VID-20201103-WA0000.mp4
    919.5 KB
Akimaliza kushangaa atuambie!

Mwambieni hata hiyo Multiparty system yenyewe nchi hii ni matokeo ya kubakwa kwa demokrasia ya kweli.

Watanzania waliukataa huo mfumo since day one kupitia tume yaJaji Nyalali.
 
Hawajaanza Michakato Ya Kumfukuza Nchini?

Maana Anatumiwa Na Mabeberu, Anatoa Tamko Gani Hilo
 
ni kweli demokrasia ina gurantee maendeleo..kijiji X wamegoma kushiriki kichimba mtaro kwa hiari kisa mwenyekiti hawakumchgua wao katka uchaguzi mdogo..hivyo anachimba yeye na mtendaji..usipuuze hio kauli
Huo ni mfano mmoja

Kuna mifano mingi sana inayoonyesha demokrasia ikitumika vibaya inavyoweza kuwa chanzo cha maisha duni haswa Kwa nchi changa kama nchi zetu za Africa.

Hivyo tusipoiangalia hiyo tunayoiita demokrasia kwa umakini tunaweza kujikuta tunapiga vita mfumo sahihi ya kutuletea maendeleo ya uchumi na jamii na kubakia tukiimba demokrasia ndani ya umaskini.

Tena tutaishia kuwalaumu watawala kwa kutokutuletea maendeleo, tutabadilisha vyama katika kushika dola bila mafanikio yoyote kiuchumi wala kijamii sababu tumeshaikataa mifumo ya ukuaji wa uchumi endelevu na kuiona kama kizingiti cha demokrasia.

Ni muhimu kuwa demokrasia na muhimu zaidi kuwa na demokrasia kwa maendeleo nchi na watu wake.

Cc Papy ndombe NosradamusEstrademe Bams NAWATAFUNA
 
Hawa mabalozi wote wanafiki na waoga tu. Kila mtu anajificha nyuma ya kivuli cha “nimesikia taarifa za so and so”.

Hawa hata wakiitwa kufafanua kauli zao wataishia kudai kwamba “wao kama wao hawasemi kama uchaguzi ulivurugwa ila tu wamesikia kutoka kwa third party”
Labda useme hujui nini maana ya diplomacy.
 
UCHAGUZI UMEKWISHA SASA TUNAJENGA NCHI YETU HEBU BALOZI SASA ZUNGUMZIE WA USA HUU WETU ACHANA NAO UMEKWISHA NA RAIS KAAPA TAYARI

Balozi ana haki ya kuongelea uchaguzi wowote wa kijeshi. Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Hiki kinanukika wanaotuelewa mbona wa kumwaga.

Kukinukisha lazima tujue:

"kufa imo, kukamatwa imo, kupigwa imo, kujeruhiwa imo, kufanywa kilema imo, na maswaibu kibao yamo."

Ila ushindi ni dhahiri!
 
Wewe leta misaada tu haya ya uchaguzi ni maamuzi ya wanaccm watanzania wazalendo. CCM haiwezi ikatoa hela za Uchaguzi na kuwaachia wapinzani washinde, haiwezekani.
 
En
Mmoja mmoja na hatimaye watatoa jibu kwa umoja.

NOTE:
Ukilalamikiwa na jirani zako ipo siku watakusanyika pasi kujua na kujadili ili wakufunze.
Endeleeni kusubili, hayo kwenu tushayazoea, mnadandia dandia kila neno mkiliona huko manadhani litawaokoa, mwaka huu mmezama kabisa,
 
Labda useme hujui nini maana ya diplomacy
Whether I know or I dont, it doesnt matter. Nachosema ni kwamba hawa mabeberu hawana cha kufanya in most cases zaidi ya matamko tu. Tena wengine wengi tu leo wameenda kushuhudia tukio la kuapishwa.

Diplomacy!
 
Whether I know or I dont, it doesnt matter. Nachosema ni kwamba hawa mabeberu hawana cha kufanya in most cases zaidi ya matamko tu. Tena wengine wengi tu leo wameenda kushuhudia tukio la kuapishwa.

Diplomacy!
Kwa taarifa yako tu matamko yao ni soft cash, kunauwezekano mkubwa wa kukosa hard cash mbele ya safari.
 
Kwa taarifa yako tu matamko yao ni soft cash, kunauwezekano mkubwa wa kukosa hard cash mbele ya safari.
Kwa kuwa Wananchi tumenywea (hakuna maandamano wala kelele) na wapinzani wachache wameanza kuunga juhudi ili labda wapewe ulaji, hakutakuwa na any follow up action.

Hawa ‘development parners” wataiomba tu Serikali ifanye investigations kwenye irregularities ili zifanyiwe kazi. Mchezo ndio umeisha hivyo.
 
Haturudi nyuma, hatuna muda wa kuchezea.
Balozi afanye kazi yake, mambo yetu ya ndani hayamhusu, na kama amekwazika afunge virago.
Kuvunja misingi ya demokrasia na kuwanyima watu haki ya kuishi kwa kuwaua, siyo mambo ya ndani bali yapo kwenye declaration ya UN.

Utakuwa mwendawazimu kama utamuua mwanao halafu ukiulizwa na majirani, ukajibu kuwa huyu ni mwanangu na mauaji nimefanyia nyumbani mwangu, majirani hamhusiki.

Utakuwa kichaa hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom