Balozi wa Kenya nchini Tanzania: Hatuiangalii Tanzania kama jirani bali kama Ndugu. Sisi sio maadui, adui yetu ni Corona

Balozi wa Kenya nchini Tanzania: Hatuiangalii Tanzania kama jirani bali kama Ndugu. Sisi sio maadui, adui yetu ni Corona

Sisi tunawaona wote katika SADC na EAC ni ndugu zetu. Ndiyo maana tumekuwa wa mwisho kufunga milango yetu.
 
Majibu yatarudi mapema, mabeberu sio watu wazuri siku zote, watu wanatumika bila kufahamu kwamba wanatumika...
 
Mbna uganda na rwanda wanafanya tu hivi?? Tofauti ipo wapi kati ya inachokifanya kenya na uganda,rwanda?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kenya ni wahuni na washenzi....wamefanya swab kwa dereva Mtanzania mpaka amepata kizunguzungu ...shenzi kabisa...hakuna hata diplomatic language katika kuchukua vipimo..
Nguvu tu mwanzo mwisho...Nadhani wanafikiri ni utawala wa JK...
 
“Rais Kenyatta amenituma hapa, anasema Kenya haiiangalii Tanzania kama jirani bali kama Ndugu, sisi sio maadui, adui yetu ni corona, ndio maana alikuwa Rais wa kwanza kuingia Chato kumsalimia JPM, akachukua dhahabu akasema mpelekeeni Magufuli” -Dany Kazungu, Balozi wa Kenya nchini Tanzania

“Bila hii corona April 26 mwaka huu Kenyatta alipanga aje asherehekee na Watanzania Muungano, alipanga awe na ziara ya muda mrefu hapa TZ kuliko Rais yeyote, uamuzi ambao Kenya imechukua kuhusu safari za mipakani sio kwasababu ya Tanzania bali adui yetu ni kirusi”-Balozi Kazungu

“Hakuna Mkenya anayemuombea mabaya Mtanzania, Wakenya tunawaombea Watanzania mpigane na janga hili, na sisi pia mtuombee, tusianze kukorogwa na kirusi hiki, tusianze kugongana kisa corona, Watu watulie, Viongozi wetu watakutana na tutalimaliza” -Balozi Kazungu
 
Back
Top Bottom