Balozi wa Tanzania aliyevurunda nchi ya SADC ni nani? Rais Samia apangua mabalozi akiwepo mmoja kutoka SADC

Balozi wa Tanzania aliyevurunda nchi ya SADC ni nani? Rais Samia apangua mabalozi akiwepo mmoja kutoka SADC

Huyo atakuwa Kipilimba, akalee wajukuu sasa
Dr.Kipilimba Mchungaji tena Mchungaji mkubwa wa kanisa kubwa nchini la Tanzania Assemblies of God na uchungaji huwa hakuna kustaafu

Anarudi kwenye kazi yake ya uchungaji kanisani kulea waumini kiroho

Walimtoa kanisani kumpa majukumu ya kiserikali anarudi huko huko walikomtoa kwenye uchungaji .Nafasi yake kanisani ipo vile vile.Atapokelewa kwa vigelegele
 
Bado inahitajika katiba mpya na uweledi zaidi katika kuteua hawa mabalozi, Sababu kila balozi inakuwa na military attachee hakuna sababu ya kupeleka wajeda wanaostaafishwa huwa wengi wamesihi maisha ya kutoa na kupokea amri hata nyanya genge hawajawahi kufanya biashara.
Unapizungumzia Economic Diplomacy unahtaji mtu mwenye spirit ya entepreneur aka tap fursa zote za kiuchumi. Mfano hizi nchi za North africa algeria, morroco, egypt, Tunisia wako mbali sana ki viwanda vya kati lakini inabidi aende balozi mwenye akili ya kupeleka fursa ya kupata mashine na ujuzi ili wananchi wetu waige kufungua viwanda vidogo na vya kati.

Sasa sisi tunapeleka wazee waliokwisha choka na kidumu chama cha mapinduzi, au machawa, au wazee wa saluti kwanza wenyeji watamuogopa kama kila akitembea kakunja sura miwani meusi watakuwa wanamkwepa hata invitation za events hapewi. Inabidi balozi akajichomeke kwenye sekta binafsi zile akili za kina mzee mengi aina ile ya watu inafaa sana kuwa mabalozi.
 
Dr.Kipilimba Mchungaji tena Mchungaji mkubwa wa kanisa kubwa nchini la Tanzania Assemblies of God na uchungaji huwa hakuna kustaafu

Anarudi kwenye kazi yake ya uchungaji kanisani kulea waumini kiroho

Walimtoa kanisani kumpa majukumu ya kiserikali anarudi huko huko walikomtoa kwenye uchungaji .Nafasi yake kanisani ipo vile vile.Atapokelewa kwa vigelegele
Ndio huyu huyu mchungaji alikuwa anawatupa watu kwenye viroba alfajiri
 
Huyu Bibi! Alichukua hatua gani.
Anapenda uswahili sana na michambo..

Hajui kama utendaji kazi wa watumishi umeshuka sana katika sekta mabalimbali.
Ni vile tu Afrika na waafrika wakipata kazi huwa hawajali
Ndio maana anaongoza nchi kiswahilikiswahili sana siunaona ana machawa kibao

na hata
Wazir wake wa fedha ,hata yule wazir wake wa habari majibu yao yalivyokuwa yakiswahiliswhili sana
 
Nchi hii ina mambo mengi muda wa kuyaelezea mchache

Una hoja
Maana hilo ni swala la Mwambata pale Ubalozini, yeye anatakiwa atoe ripoti kwa Rais na sio Rais kuambiwa na Rais mwenzake kuwa umetuletea boya
 
Kipilimba yuko sahihi kwa sababu ubalozi wake ulikuwa kama adhabu.

Serikali ijifunze sasa kutokana na hilo suala nashauri kwa watu waliokuwa na nafasi kama Kipilimba si vyema kuwapa ubalozi ni bora hata kumuacha akiendelea na utumishi wake kama ilivyoada
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida rais Samia ameeleza kupokea ombi kutoka kwa mmoja wa marais wa nchi za SADC akimwomba rais Samia ambadilishe balozi wa Tanzania aliyeko nchini “kwake” kutokana na utendaji wake mbovu.

“Nilishakutana na Rais mwenzangu ndani ya nchi za kiafrika, ndani ya Sadc, akaniambia nimbadilishie balozi, akisema uliyeniletea hata kazini haendi, mikutano hashiriki, yupo yupo tu, hatuelewi, Tanzania hatujawazoea hivyo, sasa labda umbadilishe, nikamwambia nimekusikia,” amesema Rais Samia .

Rais aliyasena hayo jana tatehe 16 August alipokuwa akiwaapisha mabalozi wapya ikulu.

Taarifa zilizopatikana leo tarehe 17 August zinaeleza rais Samia amefanya mabadiliko katika balozi tatu moja kati ya hizo ni ubalozi uliopo nchi ya SADC.

Je ni balozi yupi huyo aliyeombwa kumtangua? Soma habari hiyo hapa chini.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi mabalozi watatu na kumbadilishia kituo cha kazi Balozi Mbelwa Kairuki aliyekuwa China ambaye sasa anakwenda Uingereza akichukua nafasi ya Dk Asha-rose Migiro aliyemaliza mkataba wake.

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu usiku wa kuamkia leo Alhamisi Agosti 17, 2023 ikiwa ni saa chache tangu Rais Samia awaapishe mabalozi wapya huku akizungumzia suala la utendaji usioridhisha wa baadhi ya wanadiplomasia hao.

Katika mabadiliko hayo, waliopangiwa vituo vya kazi ni pamoja na Balozi Khamis Mussa Omar anayekwenda China akichukua nafasi ya Kairuki ambaye amehamishiwa London, Uingereza.

Rais Samia amempangia kituo cha kazi Balozi Ceaser Waitara kwenda Namibia akichukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba ambaye amestaafu.

Mwingine ni Balozi Bernard Kibesse aliyepangiwa kuiwakilisha Tanzania nchini Kenya, akichukua nafasi ya Balozi John Simbachawene ambaye amehamishiwa Kampala, Uganda.
Alivurunda Ile siku ya kupokea vyakula vya msaada akaanza kutoa amri kama amiri jeshi mkuu
Walioenda Cuba sasa wako Cuba
Bay of pigs [emoji241]
 
Ina maana hakuna reporting officer hadi aambiwe na Rais wa nchi husika?

TISS imeshindwa kazi?
Wasingeweza kumripoti mtu ambae aliwahi kuwa boss wao na ukute waliside nae kuwa kaonewa kutumbuliwa na kutupwa kule wasingeweza kumsemelea kokote
 
Wasingeweza kumripoti mtu ambae aliwahi kuwa boss wao na ukute waliside nae kuwa kaonewa kutumbuliwa na kutupwa kule wasingeweza kumsemelea kokote
Hakuna watu wanafiki duniani kama Vikosi vinavyojihusisha na mambo ya Usalama ie Jeshi, TISS Magereza etc, kuchomeana ni kawaida, fitna kawaida
 
Hakuna watu wanafiki duniani kama Vikosi vinavyojihusisha na mambo ya Usalama ie Jeshi, TISS Magereza etc, kuchomeana ni kawaida, fitna kawaida
Ni kweli lakini inategemea wanamchomea nani,mbona huyo hawakumchomea😁
 
Ni kweli lakini inategemea wanamchomea nani,mbona huyo hawakumchomea[emoji16]
Ndo hapo uone kuna tatizo sehemu.
Ila mabalozi wetu wote hawafai kuwa mabalozi, waangalie mabalozi wa US, UK kazi wanazopiga
 
Ndo hapo uone kuna tatizo sehemu.
Ila mabalozi wetu wote hawafai kuwa mabalozi, waangalie mabalozi wa US, UK kazi wanazopiga
Tatizo ni sababu za uteuzi wa kuwa Balozi maana kuna wanaoteuliwa kirafiki tu wakale bata sasa usitegemee mtu wa hivyo aliepewa zawadi akawe mchapakazi never na kuna wale wengine wanapokea kama adhabu kuwaondoa tu nchini wasionekane hao pia usitegemee kuna utendaji kazi hapo kwa hiyo wajisahihishe katika uteuzi
 
Back
Top Bottom