Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unamkumbuka balozi Abdul Cisco Mtiro? Alikuwa na kihereni sikioni.......Kuna tofauti kubwa ya kuwa kiongozi na mwananchi wa kawaidaBro hata wewe una starehe au una vitu unapenda kufanya.
Ukiwa kiongozi haikuzuii mambo yako mengine usifanye.
For as long as havunji sheria ya mtu wacha aburudishe nafsi yake.
Mf Mkapa alikuwa rais wa nchi lakini starehe yake kubwa ilikuwa tungi na muziki
Na haikumzuia kuendelea kusakata rhumba na kupiga vyombo.
Kikwete anafahamika KWA kupenda vimwana . Mbona kapita na wengi Sana akiwa presidaaaa
Kuwa kiongozi haiondoi nature yako.
Dah. Tunaomba kuona kipengele ya Katiba mpya kuhusu hii issue?CCM OUT, KATIBA MPYA IN.....!
Mbona huu upuuzi wote utabakia kuwa historia!
Mshana anapogeuka mmawia!This is childish and too low. Ulitaka kila mtu achangie kile unachopenda?!
Kwanza amechanja!!!?Kuna hali mbili au tatu kwenye makuzi
Kukua kimwili
Kukua kiakili
Kukua kimwili na kiakili
Kuna kukua kiroho pia lakini huku huambata na akili, huwezi kukua kiroho huku akili ikiwa ni ya kitoto
Makuzi ya kawaida ni kuwa na uwiano sawa wa kukua kimwili na kiakili.. Hapa kimwili namaanisha kiumri. Unaposikia fulani ana mambo ya kitoto tambua huyo umri umeenda lakini matendo yake kiakili ni sawa na ya mtoto wa umri fulani.
Ama ukisikia ana mambo ya kikubwa yaani umrí ni mdogo lakini anayofanya yalipaswa kufanywa na mtu wa umri fulani kumzidi
Kuna shida kubwa huko kwenye vetting ya viongozi mbalimbali huko chama chawala, hasa viongozi hawa wa kisiasa. Wengi hawateuliwi kutokana na weledi maarifa, ujuzi na umahiri bali huteuliwa kama asante ama kwa sababu fulani isiyo na tija kwa taifa
Nafasi zinazolalamikiwa sana kwa sasa ni nafasi za uwakilishi wa nchi mbalimbali cheo cha balozi. Wateuliwa wengi hawajui ukubwa, umuhimu na weledi wa hii nafasi.. Wengi wao wanadhani balozi wa nchi ni sawa na balozi wa nyumba kumi
Balozi ni mwakilishi wa nchi pale alipo.. Ana mamlaka kamili na makubwa ya kusimama badala ya mkuu wa nchi..hivyo matendo yake, lugha yake, life style yake ni lazima iendane na nafasi anayoshikilia
Balozi mteule unaposhinda mitandaoni na kufanya vituko wanavyofanya wadogo zetu huko mitandaoni ni wazi kabisa huyo anakuwa hajitambui ama kakua kiumri na kimwili lakini sio kiakili.
Enzi za mwalimu kufanya vituko kama hivi ni automatically umejivua cheo husika hata kabla Mwalimu hajasema
Hebu ona hiki anachofanya huyu barozi wa walawi hapa!
View attachment 2231544
Wala hakuna ulazima wa kuweka kipengele cha kuzuia watu kijirekodi wakicheza.Dah. Tunaomba kuona kipengele ya Katiba mpya kuhusu hii issue?
Yes, majibu na ukweli lazima vipatikane!Ndani ya hii post majibu yatapatikana
Hizo 7b za Peter tungewekeza Safari Channel si ingekuwa mbali?Mimi sina utani huo...kwaheri..[emoji1550][emoji1550][emoji1550][emoji1550]
Good suggestion; kwani Katiba la sasa haina hivyo vipegele? na pengine kwa maoni yako, Katiba mpya kitahakiksha hayo mabadiliko??Wala hakuna ulazima wa kuweka kipengele cha kuzuia watu kijirekodi wakicheza.
Mimi naongelea Katiba Mpya itakayoweka misingi ya uteuzi wa watu sahihi na wenye sifa kushika nafasi nyeti katika mifumo ya kiserikali.
Siyo kila mtu ateuliwe tu kwa sababu ni mwanachama wa ccm, au ni rafiki/mtoto/hawala/mke/mume/mchepuko/kunguni, au chawa wa kiongozi fulani. Au kiongoziajisikie tu kumteua mtu, halafu hakuna mamlaka ya kumhoji.
Tate Mkuu, yote uliyosema ni kweli ila binafsi nafahamu kuwa Komredi Polepole ana sifa za kuwa kiongozi wa juu sana humu nchini, in fact ana uwezo, weledi, akili, maarifa na uzalendo kuliko viongozi wengi saaana kwenye Kabineti ya sasa na hata huko Bungeni.Wala hakuna ulazima wa kuweka kipengele cha kuzuia watu kijirekodi wakicheza.
Mimi naongelea Katiba Mpya itakayoweka misingi ya uteuzi wa watu sahihi na wenye sifa kushika nafasi nyeti katika mifumo ya kiserikali.
Siyo kila mtu awe na sifa ya kuwa kiongozi kwa sababu tu ni mwanachama wa ccm, au ni rafiki/mtoto/hawala/mke/mume/mchepuko/kunguni, au chawa wa kiongozi fulani.
Mkuu usidhani shida ni chama cha ccm....tatizo ni watu,ikiwa watu ni wale wale then tegemea matokeo Yale Yale. Hao walio ccm saizi wanaweza wakahamia chadema au chama kingine chenye nguvu na wakaunda serikali.Acha kunifokea. Wengi mnapewa mamlaka makubwa huku wengi wenu mkiwa ni vilaza. Kisa tu mko ccm. Siku ya kufa hiki chama chenu, hakika hii nchi itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo.
Kaka pembe, nadhani uko sahihi some where ila ukuyafafanua vizuri. Hao uliwataja na wengine wengi ndani ya CHAMA letu, CCM, niwachumia tumbo tu. Ngoja twende and come 2024 na 2025 utaona mambo na hii picha wazi wazi! Tuombe uhai tu kwa Mungu, Yehova.Mkuu usidhani shida ni chama cha ccm....tatizo ni watu,ikiwa watu ni wale wale then tegemea matokeo Yale Yale. Hao walio ccm saizi wanaweza wakahamia chadema au chama kingine chenye nguvu na wakaunda serikali.
Kitakachokuja kuisaidia hii nchi ni vitu vikuu vitatu:
1. Elimu
2. Uwajibikaji.
3. Siasa safi.
Coz ukijaribu kuangalia mambo kwa mapana yake 2015-2021 akina mwigulu,kigwangala na wengineo walikuwa kwenye bendi ya kumsifu Rais Magufuli....ila kuanzia march 2021 nafikiri unaona mambo yalivyo badilika.