Banc ABC wamekataa kulipwa, msaada wenu unahitajika

Banc ABC wamekataa kulipwa, msaada wenu unahitajika

Kwani unavyofanya marejesho hutunzi kumbukumbu? Ulipochukua mkopo hukupewa mchanganuo wa gharama za mkopo pamoja na riba utakazolipa?
Marejesho yanakatwa kwenye mshahara, Ila nimepata cash (taslimu) mkononi nataka waachane na mshahara wangu.
 
Nikaenda wanikope 1,200,000 na wakaingizia makato kwenye mshahara wangu na nilikubaliana nao niilipe hiyo kwa miezi 6. Kweli wakaingiza mzigo nikiwa nyumbani na ulinisaidia kwenye msiba hadi ukaisha fresh.

Baada ya mwezi 1 nikapata pesa yao nikasema niwarudidhie na wanitoe kama mteja wao. Ilikuwa ni mbinde, nikasema hawa nikiwachekea hawatanitoa. Niliwawashia moto pale Mwanza mpaka wakanitoa na HRO nae akawawashia moto kuwa hataingiza makato ya mtu mwingine toka kwenye taasisi yetu awe mteja wao hadi wanitoe.

Usiwaendekeze, kawawashie moto watakutoa wapuuzi hao.
Kwa maelezo yako, hapo ulitumia Uswahili na ulienda kinyume cha mkataba wa mwanzo. Una bahati uko banana republic ila ungekuwa duniani hapo ungewakoromoea hawaongei sana unaongea na mwanasheria uone utakavyouza hadi nywele baada ya hukumu.
 
Ni baada ya kuhangaika huku na huko bila kupata mkopo wa kuendeleza biashara yangu hatimae nikakutana na hii Banc ABC wakanipatia mkopo wa miaka miwili Ila kwa makubaliano kuwa nikipata pesa yao kabla ya huo muda naweza kulipa pesa yao tukaachana.

Kweli nilipambana kwa namna yangu na Hali yangu Hadi nikapata pesa yao baada ya miezi mitatu tu na biashara yangu inaendelea.

Tatizo limeanza pale niliporudi kwao Banc ABC kutaka balance yangu ili niwalipe tuachane.

Ni mwezi wa nne Sasa tangu niombe kulipa Deni kuanzia mwezi wa tano Hadi wa Tisa (mwezi huu) wananisumbua, hawataki kunipatia balance (kiasi kilichobakia).

Msaada tafadhari nifanyeje nilipe Deni?

Sitaki kudaiwa Ila wananilazimisha, Wazo langu ilikuwa niwapeleke mahakamani Ila nimewaza huenda Kuna sehemu naweza kuanzia kuepusha lawama zisizo na msingi.

Msaada wa hatua za kuanzia...
Soma mkataba wa huo mkopo bwana Mgaa gaa upwa ili kujua gharama za kuterminate contract.hayo makubaliano ya kufanya malipo yote kabla ya mida mliyafanya kwa njia ya story hayakuwekwa kwenye mkataba.Kimsingi wewe ni mteja mzuri kwa benki,kwamba hela yao ipo
 
Mtwara BOT wanaofisi pale,jitahidi uende Leo ndugu yangu,jengo lao lipo MIKINDANI mtwara mjini,makabala na Barabara ya makonde na uchumi,mbele kuna wizara ya ardhi na rahaleo primary school
Asante Sana ubarikiwe sana
 
Soma mkataba wa huo mkopo bwana Mgaa gaa upwa ili kujua gharama za kuterminate contract.hayo makubaliano ya kufanya malipo yote kabla ya mida mliyafanya kwa njia ya story hayakuwekwa kwenye mkataba.Kimsingi wewe ni mteja mzuri kwa benki,kwamba hela yao ipo
Ndiyo, napenda nilipe Deni lao atakama wakisema waongeze riba ya miaka yote miwili.
 
Inbox haifunguki.
Huna hata haja ya kwenda. Watumie e mail tu: complaints.desk@bot.go.tz
Jitambulishe, kisha elezea ishu yako in details, na kama una ushahidi attach pia (eg mkataba wa mkopo, etc).
Wanajibu haraka sana, na wanawasiliana na benki yako, na issue yako inakua resolved haraka sana. Benki wanawaogopa sana, maana wakizingua tu wanachapwa faini. Mimi siku hizi bank wakinizingua tu, napanda huko.... Benki yangu wameshanijua, nikiwa na issue wanai resolve haraka sana ili nisiende BoT. Kuna siku nilikua branch wananihudumia, nikasikia wanaambizana chini chini, 'huyu ndo yule mteja wa BoT'.
Mgaa gaa upwa
 
Hiyo ni benki ya kihuni,kuna kipindi niliwah kukopa kwao makato yalipoisha wao wakaendelea kukata,
Kusitisha makato unaambiwa uandike barua kusitisha makato na kurudisha pesa
Ni benk ya hovyo
 
Huna hata haja ya kwenda. Watumie e mail tu: complaints.desk@bot.go.tz
Jitambulishe, kisha elezea ishu yako in details, na kama una ushahidi attach pia (eg mkataba wa mkopo, etc).
Wanajibu haraka sana, na wanawasiliana na benki yako, na issue yako inakua resolved haraka sana. Benki wanawaogopa sana, maana wakizingua tu wanachapwa faini. Mimi siku hizi bank wakinizingua tu, napanda huko.... Benki yangu wameshanijua, nikiwa na issue wanai resolve haraka sana ili nisiende BoT. Kuna siku nilikua branch wananihudumia, nikasikia wanaambizana chini chini, 'huyu ndo yule mteja wa BoT'.
Mgaa gaa upwa
Asante sana
 
Back
Top Bottom