Bandari: Ushauri wa bure kwa Rais Samia, achana kwanza na suala la kuikodisha kwa wakati huu

Bandari: Ushauri wa bure kwa Rais Samia, achana kwanza na suala la kuikodisha kwa wakati huu

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Bandari bado ni kaa la moto.

Wabunge na Bunge limeupitisha mkataba, lakini wenye nchi, Watanzania hawajui kilichopitishwa ni kitu gani.
Kwamba kuna habari kuwa Wabunge walioenda "kuona" shughuli za DP World katika bandari za huko nje walikuwa compromised, hili linaleta utata mkubwa.

Ushauri kwa Rais Samia: sitisha mkataba huu usio na uwazi ili watanzania waeleweshwe na waridhike nao.

Mwenda pole hajikwai.
 
Kwani inakodishwa?

Ache wapewe kwanza, kwani sisi tunaifanyia kazi gani?

Hii nchi ina wajaa laana sana hii. Nakumbuka vile ka nchi masikini mwenza ka Malawi kalivyotoa fidia ili wajenge Malawi Cargo pale bandarini.

Masikini wenzetu wale wakatoa fidia kwa wakaazi wa eneo lile, viwanja vikapimwa huko Yombo Vituka. Wakatoa hela ya narabara ya lami, hospital, masoko na kila aina ya miradi ya huduma za kijamii.

Matokeo yake viwanja vikapimwa lakini watu wakaambiwa wakanunue na waliopewa fidia ya nyumba wakawa wachache mno.

Barabara ya lami ikaunganishwa kuanzia pale Jet ikaishia kwa gude, pale unapoishia ukuta wa Airport. Kenge kabisa hawa.

Barabara ikachongwa ya udongo mwekundu ambayo ilielekezwa kwa Mwinyi sijui dada yake huko Yombo Dovya.

Maji vikachimbwa visima vifupi vya ku pump ambavyo hata havina maji.
 
Mimi sijausoma uo mkataba.....sijui kilichopo ndani

Ila umepotishwa haraka sana inatakiwa wananchi waelezwe vizur kilichopo kwenye
Huo mkatab ni Haki yao kujua

Mikwaruzano hii inatokea sabab tu...bunge na selikali imeshindwa kuwaelezea wananchi....

Moja ya mkangqnyiko ni mkataba wa mda Gani??? Hakuna aliwahi kujib hili swali...
 
Kipindi iko chini ya Tics kwa miaka 25 ulishawai waambia Mkapa au Kikwete au Magufuli waache kushirikiana na wawekezaji Tics?

Tunawajua mawakala wa Kenya. Mnapigana kila kikucha ili Bandari zetu zisifanyiwe maboresho yanayohitajika ili Bandari zenu ziendelee kuwa juu yetu.

Ila jueni tu sasa Tanzania tumeamka na lazima bandari zetu ziwe za kisasa zaidi kuliko za kwenu hapo Kenya
 
Ushauri wa kipumbavu kabisa hauwezi ukafanyiwa kazi hata kidogo!!
 
Hakuna upuuzi wa Bandari. Kuna propaganda za wakenya na wazandiki wachache wasiotaka Tanzania tupate maendeleo ya kweli
 
Mimi sijausoma uo mkataba.....sijui kilichopo ndani

Ila umepotishwa haraka sana inatakiwa wananchi waelezwe vizur kilichopo kwenye
Huo mkatab ni Haki yao kujua

Mikwaruzano hii inatokea sabab tu...bunge na selikali imeshindwa kuwaelezea wananchi....

Moja ya mkangqnyiko ni mkataba wa mda Gani??? Hakuna aliwahi kujib hili swali...
Huo mkataba uliojadiliwa bungeni ni mmoja tu na hauna ukomo, tofauti na ile mikataba itakayosainiwa kati ya wafanyabiashara na wawekezaji hapa tunaongelea ile mikataba itakayo kuwa kazini kibiashara.

Sio tu hiyo mikataba ya kibiashara itakuwa na ukomo, pia muwekezaji atalazimika kujisajili BRELA hivyo kuwa chini ya sheria zote za ndani.

Hao wanasheria wanaojifanya wazalendo sana wangekuwa na moyo wa kizalendo kweli iwapo wangewaelezea wananchi huu ukweli kuhusu tofauti ya mkataba uliokwenda bungeni na hii mikataba ya kibiashara tutakayoingia na DP World.

Wanasheria wetu kwa kujua au kutojua wameamua kufanya kazi ya usaliti kwa nchi yao wenyewe!.

Huyo dada Maria Sarungi ana bahati amezaliwa nchi mfano wa Tanzania, sidhani kama angekuwa hai mpaka dakika hii nchini Rwanda kwa Kagame au Uganda kwa Museveni.
 
Sasa itakuwaje?
Watu hawataki kunyolewa!
Minafikiri tofauti kidogo....
Ifike wakati sasa wananchi tuanze kujadili soka na minyanduano tu huku tukuomba Mungu na kila mmoja akijipambania, maana mamlaka zimepewa nguvu ya kikatiba za kufanya wanavyo taka. Na ikitokea umeipanga mamlaka basi kosa linabadilika na kuwa uvunjifu wa sheria.
 
Minafikiri tofauti kidogo....
Ifike wakati sasa wananchi tuanze kujadili soka na minyanduano tu huku tukuomba Mungu na kila mmoja akijipambania, maana mamlaka zimepewa nguvu ya kikatiba za kufanya wanavyo taka. Na ikitokea umeipanga mamlaka basi kosa linabadilika na kuwa uvunjifu wa sheria.
Watawala lazima wawajulishe kinagaubaga wenye nchi, watanzania juu ya mustakabsli wa hatma ya vitega uchumi wao.
Nia inaweza kuwa njema, lakini wananchi/wenyenchi wakieleweshwa na kuondoa duku duku zote, muafaka unakuwa rahisi.

Kwa mfano vifaa vyote vya ulinzi na usalama ni muhimu, sasa jeshi likiagiza vifaru, si chini ya nchi tatu zinapata habari hiyo.
Na siri zaweza kuuzwa na nchi ya tatu.
Hilo halikubaliki.
 
Back
Top Bottom