Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
- Thread starter
- #21
Mpaka mbuzi alie meeehehe....!Mkuu unapigia mbuzi gitaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpaka mbuzi alie meeehehe....!Mkuu unapigia mbuzi gitaa
Bandari bado ni kaa la moto.
Wabunge na Bunge limeupitisha mkataba, lakini wenye nchi, Watanzania hawajui kilichopitishwa ni kitu gani.
Kwamba kuna habari kuwa Wabunge walioenda "kuona" shughuli za DP World katika bandari za huko nje walikuwa compromised, hili linaleta utata mkubwa.
Ushauri kwa Rais Samia: sitisha mkataba huu usio na uwazi ili watanzania waeleweshwe na waridhike nao.
Mwenda pole hajikwai.
Mimi mara nyingi nimesema aachane nayo kabisa,Nchi hii imejaa Wajamaa ni mbumbumbu waliozoea shida,Wacha waendee kuingia gharama kubwa hapo bandarini,bidhaa kupotea, urasimu na upuuzi kama huo huku Wateja wakikimbia , kwani ana hasara gani watu wamechagua shida?Bandari bado ni kaa la moto.
Wabunge na Bunge limeupitisha mkataba, lakini wenye nchi, Watanzania hawajui kilichopitishwa ni kitu gani.
Kwamba kuna habari kuwa Wabunge walioenda "kuona" shughuli za DP World katika bandari za huko nje walikuwa compromised, hili linaleta utata mkubwa.
Ushauri kwa Rais Samia: sitisha mkataba huu usio na uwazi ili watanzania waeleweshwe na waridhike nao.
Mwenda pole hajikwai.
Wengi hata kama wangeusoma wasingeulewa.Wabunge wenyewe hawajausoma isipokuwa wamepewa amri wapitishe, pale hakuna bunge kuna genge la wahuni
Huo mkataba uliojadiliwa bungeni ni mmoja tu na hauna ukomo, tofauti na ile mikataba itakayosainiwa kati ya wafanyabiashara na wawekezaji hapa tunaongelea ile mikataba itakayo kuwa kazini kibiashara.
Sio tu hiyo mikataba ya kibiashara itakuwa na ukomo, pia muwekezaji atalazimika kujisajili BRELA hivyo kuwa chini ya sheria zote za ndani.
Hao wanasheria wanaojifanya wazalendo sana wangekuwa na moyo wa kizalendo kweli iwapo wangewaelezea wananchi huu ukweli kuhusu tofauti ya mkataba uliokwenda bungeni na hii mikataba ya kibiashara tutakayoingia na DP World.
Wanasheria wetu kwa kujua au kutojua wameamua kufanya kazi ya usaliti kwa nchi yao wenyewe!.
Huyo dada Maria Sarungi ana bahati amezaliwa nchi mfano wa Tanzania, sidhani kama angekuwa hai mpaka dakika hii nchini Rwanda kwa Kagame au Uganda kwa Museveni.
Achukue tahadhari na ushauri.Ila akijikwaaa anaenda moja kwamoja kupiga pua chini hadi kuchubuka na kubimba
Mashambulio kwa huu mkataba ni makubwa.Mungu Ibariki Tanzania!
Eee Mungu eeh, Ibariki Tanzania! Njoo huku!
CCM must go!
Pamoja na kuwa mkataba unawapa nyenzo na mamlaka Kampuni ya watu binafsi kuilazimisha Serikali ya Tanzania kufanya maamuzi magumu kama ya 'kuwataarifu' kuhusu hatua zezote zile Serikali itakayochukua, yaani....
Tanzania itaijulisha DPW juu ya fursa zozote zilizopo, na zitakazokuwepo sasa na baadae.
Basi,sasa Wananchi nao kwa sauti moja, watoe na kuitaarifu CCM, kuwa nao, Wananchi watafanya maamuzi magumu na kuwapa taarifa kuwa CCM hawatachagilika hapo baadae.
Sasa, kwa muktadha huo, itakuwa sahihi kwa Wananchi wote waendelee kudumisha amani na utulivu, umoja na mshikamano, kwa kulinda Katiba.....na maadili na utamaduni zetu na rasilimali zetu kuwajulisha chama cha mapinduzi, kuwa fursa zezote zile walizobakiwa nazo na fursa zezote zile zitakazo kuwepo hapo baadae, kuwa, itawa taarifu Umma/Wananchi, kuwa ifikapo Tarehe itakayotangazwa na uwepo wa Uchaguzi, kuwa, kama Chama kilichopo madarakani, kuwa, kitatota taarifa kuwa Chama kipigiwe kura iwapo tu, kilisharudisha Mkataba bungeni ujadiliwe kwa mapana na marefu, kwamba, kimeondoa vipengele tajwa na tata katika mkataba unaojadiliwa na mijadala yote nchini, na kuwa pia,kitaondoa wingu, jinamizi, laana , shetani, tandabuli la na hofu, na kwa, manufaa ya Nchi na Wananchi wake, kuwa, limerudisha matumaini na matamanio ya wananchi kwa Serikali yake, kuwa, kinyume na hayo, kuwa, Mkataba wake utakoma kwa njia ya Kura.
Kwamba, Wananchi watapiga kura yao na kuwaondoa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuchagiza mkataba hovyo kutokea Nchini.
Chagua kwa Uangalifu na Umakini mkubwa 2025.
Amani ikutandae