Bandari ya Dar es Salaam ina changamoto za Mafanikio

ogopa sana kuongozwa na hisia , sio Tz tu imetoa bandari kuongozwa na watu wengine zipo nyingi tu na maisha yanaenda. zile kelele za wachumia tumbo kina Dr slaa na wenzake zinakuchanganya
 
Hu Uzi ukiusoma kwa umakini sidhani kama utasikiliza kelele za wapotoshaji kuhusu bandari Dar. Nyumbu kwenye huu Uzi watapita kama upepo
Sasa wewe unafikiri hayo mabadiliko yameletwa na DP World au tayari serikali ilikuwa imeshawekeza kwenye miundombinu muda mrefu uliopita?

Na kama ni hivyo huoni kwamba ni ujinga kwa serikali kumkabidhi mwekezaji chombo ambacho kipo tayari na kinafanya kazi vizuri aje mgawane mapato bila yeye kuweka uwekezaji wowote? Na tena awawekee masharti kibao?

Mengi ya haya yaliyoandikwa hapa ni siasa tupu! Bado meli nyingi zinazoleta mizigo ya Congo na Uganda na hata Zambia zinakimbilia Mombasa kwani Dar foleni ni kubwa mno. Akili ni kitu kizuri sana la sivyo ni kudanganywa kipumbavu.
 
PendoLyimo unaiona hii! Ni aibu tupu
 
PendoLyimo
 
Kaka umesoma kweli na kuelewa kilichomaanishwa au utakuwa umecompare na msongamano wa barabarani ndugu
 
Mbona swiss port walichukua uendeshaji pale airport ya Dar na watu mlikuwa kimya, hivi vitu vipo duniani kote na kwa faida yako tu nikwambie tu kuachiwa wazawa kujiendesha sio mbaya ila sisi vingi tulivyoachiwa kujiendesha vilikufa kifo kibaya sana

Tuendele kuvumilia tu maendeleo lazima yaje na mabadiliko
 
Hakika
 
..makala uliyoileta inajenga picha kwamba MSONGAMANO ktk bandari yetu ni jambo la kujivunia, na huduma nzuri kwa WATEJA.
Hakika na inatafsiri kwamba bandari yetu ni chaguo Bora kwa wateja
 
Tunaposemaga #MamaYukoKazini wananzengo mtuelewe
 
Iwe swiss port , kadco, loliondo,tics/Hutchinson ya Singapore ya Tz na sasa dp weldi, kinachogomba ni Sisi wenyewe kupendekeza upigaji kabla ya kazi, na pili ni madhara yake .tatu gharama za kutoka hapo tulipokwama au kuweka nkataba ya chifu mangungo na mwisho ni hasara tunayokuwa tumepata na hao werevu wajinga wachache waluofikiria kwamba wamepata kumbe wamepatikana kuwaachia wajinga fulani hiyo mali walioipata kwa njia za mkato Kwa watu ambao hawawezi kuziendeleza hivyo mwisho wa siku tunakuwa tumejiuza Sisi wenyewe Kwa wageni. Hivyo kujipa mzigo karne kutoka hapo.
 
..MSONGAMANO maana yake ni inefficiency.

..hivi unafikiri WATEJA wa bandari yetu wanafurahia msongamano?

.
MSONGAMANO sio sawa na wingi...Bandari ya DAR imepokea meli nyingi haina msongamano wa meli
 
Katika mgawanyo wa kibiashara ni lazima kwa baadhi ya meli kwenda bandari ya Mombasa, sijaona andiko lako kuhusu meli zilikuwa zinaenda bandari ya Mombasa na zikaamishia bandari yetu.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
hoja yako imejengwa na hofu na wasiwasi. makala yetu inahusu Changamoto za Bandari ya Dar zinazotokana na maendeleo na si vinginevyo. sisi kama Taifa lazima tukubali kuwa kila tunapopiga hatua katika ufanisi kwenye jambo fulani, na changamoto nazo hufuata. ndio msingi wa aliyeandaa makala hii kuwa watu wengi wamezoea kulalamika wakiona meli zimepaki zikisubiri kutia nanga DAR PORT sasa mwandishi anatuambia badala ya kulalamika basi tufurahie
 
Safi Sana kwa uchambuzi wa Dar Port hali ya awali na sasa. Uchambuzi umegusa sehemu moja tu General Overview ya Dar Port.

Tunaomba uweke na uchambuzi sehemu za Port Operations ugusie Port Facilities, Truck turnround time, Vessel turnround time na mifumo ya uondoaji mizigo. Wakati uliopita na wakati wa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…