FaizaFoxy hongera kwa jitihada zako kuweka mambo sawa kuhusu uwekezaji bandarini kupitia DPW, kampuni ya Emirate ya Dubai. Pamoja na juhudi zako za utetezi, ikabidi utuwekee mfano huo pasipo kueleza tofauti ya maudhui na utekelezaji, kisheria, wa "MoU" na "IGA".
Nitaendelea kuonesha shaka yangu kuhusu mkataba wa IGA. Ni
ukweli tu utaniweka huru na wenye mashaka kama mimi.
Serikali bado inaongelea faida za IGA zaidi kuliko madhara yaliyomo kwenye baadhi ya vifungu vya IGA ambavyo kama mikataba ya utekekezaji (HGAs) itaandaliwa katika misingi hiyo. Na kwa kuwa hiyo mikataba ya utekelezaji inabaki siri, kwa nini tusiwe na mashaka?
Kwa vyovyote vile, wenye mawazo kama mimi, tumetia shaka, pamoja na dhamira nzuri ya Serikali, ikitokea kuna sababu za kusitisha mkataba
Kifungu cha 23: Muda na Utaratibu wa Kusitisha Mkataba, kina ukakasi. Ukinieleza ukweli wa hicho kifungu, kwa maslahi mapana ya kitaifa, utakuwa umeniweka huru.
Kifungu kidogo cha
4. Nchi Wanachama hazitakuwa na haki ya kushutumu, kujiondoa, kusimamisha au kusitisha Mkataba huu katika hali yoyote, hata ikitokea ukiukwaji wa mkataba (material breach), mabadiliko ya kimsingi ya hali, kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia au kibalozi, au sababu zingine zozote zinazotambuliwa chini ya sheria ya kimataifa. Bila kujali yaliyotajwa hapo juu, mgogoro wowote kati ya Nchi Wanachama kuhusiana na hali kama hizo utashughulikiwa kulingana na mahitaji ya Ibara ya 20 ya Mkataba huu.
Ni nini maana ya
material breach?
Kifungu cha 20 kinahusu Utatuzi wa Migogoro, Kifungu kidogo cha
3. Migogoro chini ya Mikataba ya Mradi na HGAs pia itatatuliwa kupitia usuluhishi wa kimataifa katika ukumbi na kiti kisichoegemea upande wowote..
Kifungu kidogo hicho ni kinyume na Kifungu cha 21:
Sheria itakayo ongoza Mkataba huu itakuwa Sheria ya Uingereza ambapo sheria ya uongozi wa kila HGA na Mikataba ya Mradi husika itakuwa ni kwa sheria za Tanzania
NASUBIRI UFAFANUZI WAKO
Kazi iendelee.