Bandari ya Zanzibar imeshapita IGA na Oman kwa sasa ni mikataba ya HGA

Am out for what u think bout, wat i need to know... Port contract is taking for how long? That's all!
Now they are working on HGA,.after HGA you'll see many contracts.

But one for variety of port impvements has been rushed on an MoU style, done deal 👇🏾
 
Hivi zanzibar watu million moja kwanini mnataka kubebwa bebwa na bara? Hivi kweli nyie ni wakushindwa kulipa umeme?
 
Hivi zanzibar watu million moja kwanini mnataka kubebwa bebwa na bara? Hivi kweli nyie ni wakushindwa kulipa umeme?

Si unauzima tu. Ulilazimishwa kuuwasha?
 
Memorandum of understanding sio mkataba. Hata kwenye IGA yetu inatajwa MoU iliyoingiwa kati ya TPA na DPW. Usipotekeleza MoU haupelekwi mahakamani na wala hakuna arbitration. IGA ni mkataba na tusipoutekeleza tunapelekwa Johannesburg.

Lakini unastahili sifa kwa jitihada zako za kutetea msimamo wako. Bahati mbaya ni kuwa hazina logic.

Amandla...
 
Hii ni habari ya MoU iliyosainiwa Aprili mwaka jana wakati wa ziara ya Mhe. Rais Dubai. Na imetajwa kwenye IGA. Sisi hatubishi kuwa kuna uwezekano wa kuingiwa HGA nyingi za thamani kubwa kubwa. Tatizo letu ni masharti yaliyomo katika IGA ambayo ndio yanaongoza HGA. Hata HGA ziwe nzuri vipi, IGA itabakia kuwa na dosari kubwa.

Amandla...
 
Sasa tatizo lako si unakwenda kuipinga serikali yako mahakamani.


Hakuna JF au mtaani mwenye nguvu ya kuufuta makubaliano ya Kimataifa.

Labda huelewi au wengi wenu hamuelewi kuwa makubaliano yakishakuwa IGA yanakuwa automatic chini ya udhamini wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Maana yake huwezi kuweka au kuandika mikataba hiyo kwa kupenda kwako bila kufata sheria na kanuni za Umoja wa Mataifa zinazilinda kila nchi husika.

Hapo ndipo ukaona tulpokiuka mikataba ya wawekezaji na makandarasi wa nje, tukaumizwa mahakama za nchi tofauti duniani, yaani hapo ukikiuka masharti, au wewe Tanzania au Dubai basi kinachomlinda kila mmoja wenu ni Umoja wa Mataifa.

Sasa nyinyi kama hamziamini mahakama a Tanzania si nendeni ofisi za Umoja wa Mataifa mkapeleke malalmiko yenu kuwa kuna misingi ya Kimataifa imekiukwa.


Hivi kwa akili zenu fupi mnaelewa mnachokiongea au mnabwabwaja na kuhorola bila mpango.


Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Mou siyo mkataba? kawaulize Makanisa ya Kimataifa yrenye matawi yake Tanzania kama hayana MoU na serikali ya Tanzania.

Mpaka nnacheka mlivyo mapoyoyo.
 
Nani kakwambia Zanzibar ina mamlaka ya kuingia IGA na nchi nyingine?. Hujui kuwa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ni mambo ya muungano?. Tutakukumbusha Zanzibar ilipojaribu kujiunga na OIC kilichotokea!.

Labda kama serikali za CCM siku hizi zimeamua kufumbia macho uvunjwaji wa katiba waziwazi!
 
IGA inazungumzia English law wewe unazungumzia sheria za Umoja wa Mataifa ambazo hata hazipo. IGA inazungumzia arbitration kufanyika Johannesburg wewe unazungumzia Umoja wa Mataifa. Halafu bila aibu unawaita wenzako wajinga. Aliyekutafsiria IGA amekuchuuza.

Amandla...
 
Mou siyo mkataba? kawaulize Makanisa ya Kimataifa yrenye matawi yake Tanzania kama hayana MoU na serikali ya Tanzania.

Mpaka nnacheka mlivyo mapoyoyo.
Tangu lini MoU imekuwa ni mkataba? Seriously?
Amandla...
 
Kweli saa mbovu muda mwingine inaseme kweli

Wewe bi Mkubwa sometimes unazungumza madini

Nakupa five Kwa hili
 
Watu wa Rufiji hao.
 
Watu wa Rufiji hao.
Tena sawa kabisa, maana waalivyotoka Lake Tanganyika walifata mto rufiji mpaka Pwani. Siku hizo hakuna barabara, ni misitu tu, njia nyepesi na nzuri ilikuwa ni kufata maji.
 
Huu Muungano ni wa kisanii sana. Zanzibar wanawezaje kuwa na mipango yao tofauti juu ya uendelezaji wa bandari wakati bandari ni suala la Muungano?
 
Huu Muungano ni wa kisanii sana. Zanzibar wanawezaje kuwa na mipango yao tofauti juu ya uendelezaji wa bandari wakati bandari ni suala la Muungano?
Huu Muungano utatuletea vita ya sisi kwa sisi.
 
Huu Muungano ni wa kisanii sana. Zanzibar wanawezaje kuwa na mipango yao tofauti juu ya uendelezaji wa bandari wakati bandari ni suala la Muungano?
Sasa mtawaelewa Wazanzibari wakati miaka yote wanasema huu Muungano una mapungufu makubwa sana.
Tatizi ni serikali mbili, inatakiwa ziwe serikali tatu. Kila mmoja na yake na mengine ya Muungano. Kwa serikali mbili lazima ilete utata wa mambo kama hayo.
 
Makubaliano hayo ya IGA yamefata sheria za wapi? Unaongelea nchi mbili hapo, moja Tanzania moja Dubai.

Makubaliano ya ujengwaji bandari mpya Zanzibar yamefata IGA ys sheria za wapi?
 
Hao wanaoonekana kuwa wachache wanaofanya maamuzi ya wengi huwa na ulinzi wa katiba inayotumika.

Ni dhana ya ubaguzi kumtazama kiongozi kwa msingi wa wapi anapotokea na kuacha picha kubwa ya kile anachokifanya tena chenye kuacha urathi wa kudumu miaka ijayo.

Kwanini utangulize asili ya mtu unapotumia nguvu nyingi kuupinga mkataba wa kibiashara?. Vipi kuhusu uzanzibari wake pale anapofanya mambo chanya yenye kuyagusa maisha ya hao hao wanaoleta ubaguzi leo hii?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…