Bangi: Kwanini wengine wanaifurahia, lakini wengine hupata madhara makubwa?

Bangi: Kwanini wengine wanaifurahia, lakini wengine hupata madhara makubwa?

Hola! 🙋🏽‍♀️
Ningependa kujua maoni yenu kuhusu bangi(420) pia huitwa weed, marijuana, ganja, n.k..

View attachment 3563320

Kuna watu wanasema wanaitumia kwa kujisikia vizuri, kupunguza stress au hata kama dawa. Pia nimesikia kwamba baadhi ya watu wanaofanya kazi ngumu au zenye msongo mkubwa (kama hospitali au sehemu za hatari hutumia ili kujituliza.. madakataria (theatre,morgue)

View attachment 3563321

Lakini kwa upande mwingine, kuna watu wanaosema bangi inaweza kusababisha uraibu (addiction), kuchanganyikiwa akili, au hata mtu “kuwa kama amerukwa na akili” hasa akitumia kupita kiasi. Wengine pia wanasema katika familia zao ni mwiko mkubwa, na mtu akianza kuitumia anaweza kuharibika kabisa.

View attachment 3563322

Maswali yangu ni:

* Kwa nini watu wengine wanaweza kuitumia bila matatizo makubwa, lakini wengine hupata madhara makubwa?

* Je, ni kweli bangi inaweza kuwa dawa au ni hatari zaidi kuliko faida zake?

* Ni mambo gani yanayofanya mtu awe katika hatari ya uraibu au matatizo ya akili?

Haya ni baadhi ya majinaa tofauti ya bangi yanayotumika:

  • Bangi
  • Weed
  • Marijuana
  • Ganja
  • Herb
  • Grass
  • Pot
  • Dope
  • Mary Jane
  • Joint (wakati imevutwa kama sigara)
  • Spliff
  • Hash / Hashish
  • Skunk
  • Kush
  • Blaze (slang ya kutumia)

View attachment 3563324
Nilipitwa 😁
 
Unasemaa??🤔
... Kuna rafiki yangu mmoja alianza tukiwa Secondary, na aliimudu vibaya, lakini kwenye utu uzima, akiwa daktari mwenye kituo cha afya binafsi, Bangi ilimharibia kazi, ikaua biashara yake, na mwisho akafa na umaskini na frustrations!
 
🤣🤣🤣

1000150636.jpg
 
Kumbe!! Basi kumbe sio kitu cha kuzoea kabisa!🙆🏽‍♀️

O'level tulisoma na jamaa mmoja sio vizuri kumtaja jina kwao Ukonga kule. Yaani jinsi alivyokuwa anakokotoa mathematics utadhani ni genius kumbe bangi tu, paper ilivyokuja akapata zero. Nafikiri familia yake waliamua kumrudisha Tarime yule jamaa
 
Back
Top Bottom