Moshi Sativa
ikijulikana kama Moshi Sativa au Elephant Stomper" au "Elephant Flattener")
Ni moja kati ya bangi chache sana duniani zilizobaki katika mfumo wake wa asili kabisa (100% Pure Sativa Landrace).
Mmea huu ulitokea na kukua kwa karne nyingi kwenye miteremko yenye rutuba ya Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania na maeneo ya mipakani mwa Kenya.
Kutokana na mwinuko wa mlima huo na mazingira ya kipekee ya kijiografia, mmea huu ulitengeneza vinasaba (DNA) imara sana ambavyo vimekuja kuwa lulu kwa wataalamu wa mbegu duniani.
Apo kale
Kabla ya Mawindo; Wawindaji wa kienyeji walikuwa wakiitumia kabla ya kwenda kuwinda wanyama wakubwa ili kuongeza umakini, stamina, na nguvu za kukimbia kwenye misitu minene.
Kazi Ngumu za Kilimo; Ilitumiwa pia kusaidia kupunguza uchovu wakati wa kufanya kazi ngumu za kilimo kwenye miteremko mikali ya milima.
Sherehe za Kimila; Ilikuwa sehemu ya tambiko na sherehe mbalimbali za kidini na kitamaduni.
Muundo wake na ukuaji
Urefu wa Kustaajabisha: Mimea hii inakua mirefu sana, mara nyingi ikivuka futi 8 hadi 10 kwenda juu, ikiwa na matawi marefu na majani membamba sana.
Muda wa Kuchanua: Inachukua muda mrefu kukua. Wakati bangi za kisasa za maabara zinachukua wiki 7-8 kuchanua, Kilimanjaro halisi inahitaji kati ya wiki 10 hadi 12 au zaidi.
Nta na Mafuta (Resin): Licha ya kuwa mmea wa mwitu, maua yake yanazalisha kiwango kikubwa sana cha trichomes (vinyweleo vidogo vinavyozalisha mafuta yenye THC).
Siri ya Kemikali na Harufu (Terpene Profile)
Kilimanjaro ina harufu ya kipekee na ya kigeni sana. Inasifika kwa kuwa na harufu kali ya limau na machungwa (sharp citrus), ikichanganyika na harufu ya miti ya mibaini (fresh pine), udongo wa kitropiki, na viungo vya ndani ya misitu. Kwenye majukwaa ya wakulima wa zamani kama vile Overgrow.com, watumiaji pia wanakubaliana kuwa aina hii hubeba ladha au harufu ya Mikaratusi (Eucalyptus).
Hey
Seran weekend hii uku. Skunk Pori 😇