Bank gani nzuri kufunguA fixed au saving account?

za kuambiwa changanya na zako.. tatizo watu wanajibu tu humu wenzao kwa story za vijiweni... ukiweka milioni 20 kwa mwaka access bank riba utakayopata hata milion 3 haifiki.. na hapo kuna with holding tax

1.6m per month?????
 
Kuna mkuu moja hapo juu alitoa wazo la kuwekeza kwenye Banks ndogo nimefatilia kwa kina nimeona ni kweli tena hasa kwa mkuu huyu mwenye 20m kwa bank kama access bank wanatoa riba nzuri sana kwa depositors kila mwezi utakua na uwezo wa kutengeneza hadi 1.6m faida.

mkuu hii yako hatari, sijui km kuna faida hii, kama ingekuwepo watu wangeacha kazi zingine kabisa.
 
ni biashara halali chache sana zinaweza kulipa kwa kiwango hicho.....na hizi chache utakuta risk pia ni kubwa sana. Kilimo kwa mfano kinaweza kulipa faida kubwa lakini risk ya kupoteza pia ni kubwa mno.

Ku fix sh 20m na kupata riba ya sh 1.6m kwa kila mwezi, ni sasa na kusema riba ya 96% kwa mwaka. Hakuna benki yoyote inayoweza kulipa kwa kiwango hiki. Jiulize tu, wao watawekeza kwenye nini ili wapate ribs/faida ya zaidi ya 96% kwa mwaka?

Anyway, ni mjadala mzuri. Unapoweka fixed deposit ni muhimu pia kuzingatia mfumko wa bei. Usipokuwa makini inaweza kuwa hujapata faida yoyote maana thamani ya ile hela uliyo fix baada ya mwaka itakuwa imepungua. Inflation rate kwa sasa wastani wa 5% (oopps, ngoja nicheki NBS nsije fungwa!). So shilingi 100 ya sasa itakuwa sawa na sh 95 baada ya mwaka mmoja! Au kwa lugha nyingine, utahitaji sh 105 baada ya mwaka mmoja kununua kitu kinachouzwa sh 100 sasa hivi.
 
umesoma kipeperushi vizuri lakini haujaelewa.... ukiona riba ni asilimia 8 kwa mwezi.. haimaanishi utalipwa asilimia 8 yote.. ila utalipwa 8/100 x hela uliyoiweka fixed kisha unagawanya kwa 12 ... huu ni uhuni ambao bank haikuambiii maana wanajua utaghairi

Aisee huu ni uhuni uliokithili,aksante kwa kutujuza.
 
za kuambiwa changanya na zako.. tatizo watu wanajibu tu humu wenzao kwa story za vijiweni... ukiweka milioni 20 kwa mwaka access bank riba utakayopata hata milion 3 haifiki.. na hapo kuna with holding tax
We unaongelea mwaka mi naongelea mwezi mkuu, wanaruhusu hata kwa mwezi na ni zaidi ya 8.5% , naongea nikiwa na ushaidi mkuu.
 
umeshawai kuweka hiyo hela na ukapata faida baada ya huo mwezi mmoja au ushahidi wa kuambiwa na watu.. unajua hiyo 8.5 % inakuwa calculated vipi?
 
mkuu hii yako hatari, sijui km kuna faida hii, kama ingekuwepo watu wangeacha kazi zingine kabisa.
Haipo kwa kwa maana ipi sasa mkuu? Mi najua unabisha kwa hoja yenye mashiko , sema nikutumie form ya riba zao kwa depositors halaf uendelee kupinga
 
Jamani kuna ka hela kangu kama 20mil nimekapata ghafla... Wakati nafikiria cha kufanya nimeona nibora niiwekwe bank kwanza. Mwenye kujua bank yenye interest nzuri anisaidie ili niweze kupata kijifaida wakati naendelea kutafakari.
Mkuu wekeza na FINCA Microfinance Bank hutajuta.

Interest yao inaanza 10% hadi 15% kutegemea kiasi unachoweka.
 
ni biashara halali chache sana zinaweza kulipa kwa kiwango hicho.....na hizi chache utakuta risk pia ni kubwa sana. Kilimo kwa mfano kinaweza kulipa faida kubwa lakini risk ya kupoteza pia ni kubwa mno.

Ku fix sh 20m na kupata riba ya sh 1.6m kwa kila mwezi, ni sasa na kusema riba ya 96% kwa mwaka. Hakuna benki yoyote inayoweza kulipa kwa kiwango hiki. Jiulize tu, wao watawekeza kwenye nini ili wapate ribs/faida ya zaidi ya 96% kwa mwaka?

Anyway, ni mjadala mzuri. Unapoweka fixed deposit ni muhimu pia kuzingatia mfumko wa bei. Usipokuwa makini inaweza kuwa hujapata faida yoyote maana thamani ya ile hela uliyo fix baada ya mwaka itakuwa imepungua. Inflation rate kwa sasa wastani wa 5% (oopps, ngoja nicheki NBS nsije fungwa!). So shilingi 100 ya sasa itakuwa sawa na sh 95 baada ya mwaka mmoja! Au kwa lugha nyingine, utahitaji sh 105 baada ya mwaka mmoja kununua kitu kinachouzwa sh 100 sasa hivi.
Ni wazo zuri, umeangalia mbali kwa jicho la tatu...ila kikubwa ilikua ni kumshauri tu huyo mkuu aliyekua nataka azifix fedha zake wakati anasubiri pa kuzipeleka.
 
umeshawai kuweka hiyo hela na ukapata faida baada ya huo mwezi mmoja au ushahidi wa kuambiwa na watu.. unajua hiyo 8.5 % inakuwa calculated vipi?
Sio lazima nikuaminishe mana sio lazima uniamini mana hata hivo hukua mlengwa ...jaribu kutembelea tawi lao kwa maelezo .
 
mimi sibishani na wewe ila nataka nikuelekeze nimegundua kuna kitu hukijui.. kama hutaki ukijue kimbia... mzazi wangu ana hela access nyingi tu fixed.. na hata mimi nishawai weka fixed milion 5 mwaka huu july.. kuna kitu najua hujui ila unaleta ubishani tu.. nimekuuliza unajua riba ya mwezi inakuwa calculated vipi?

Sijui niambie.
 
Kila bank unaweza kufungua account ya dollars kwa maana hyo pesa uliyonayo uibadili kuwa ktk dollars kisha uiweke. Halafu unakua unacheck dola imepanda kwa kiasi gani halafu unawithdraw dola chache kulingana na mahesabu yako. Ilimradi isishuke au isipungue ile uliyoweka kama mtaji.
Una withdraw kivp wakati ni fixed, au mie sikuelewa vizuri?
 
kama umeweka kwa mwezi mmoja kwa riba ya asilimia 8.5% formula ni (hela uliyoweka) x 8.5/100 x 1/12 = (utakachopata jibu) zidisha kwa 10/100 kisha itoe hilo jibu ulilolipata baada ya kuzidisha kwa 10/100 ni with holding tax kitakachobaki ndio faida yako

siku nyingine ukienda bank uliza kwa umakini uelewe kijana..

fixed ingekuwa rahisi hivyo ina hela bwerere nani angehangaika kufanya kazi?

Sijui niambie.
 
Yaan ww unawaza kuweka pesa fixed wenzio wanazalushia du pole kwa kukosa maarifa ss nikuambue kanunue bitcoin ziache alf utaona nn kitatokea hutoamn ktk maisha yko yote hd unakufa tumia utandawax kupata utajil co unakaa tu ingia mtandaon now som nn bitcoin ndo utajua
 
Kila bank unaweza kufungua account ya dollars kwa maana hyo pesa uliyonayo uibadili kuwa ktk dollars kisha uiweke. Halafu unakua unacheck dola imepanda kwa kiasi gani halafu unawithdraw dola chache kulingana na mahesabu yako. Ilimradi isishuke au isipungue ile uliyoweka kama mtaji.
ongezeko la hiyo dolla ita offsetiwa pale atakapoenda kubadilisha apate madafu maana humu ndani hawezi fanyia dolla chochote
 
Back
Top Bottom